Inahitajika njia bora zaidi kuendesha mashindano ya ulimbwende.

image

Kwa takribani miaka zaidi ya 15 mashindano ya Miss Tanzania yamekuwa yakiratibiwa na kuandaliwa na kampuni ya Lino Agency,ambayo inaongozwa na HAshim Lundenga.

Mashindano haya ni makubwa na yana sura ya utaifa zaidi ambapo kama yatatumiwa vizuri inaweza kuwa tu ni zaidi ya burudani au mahala pa kujitajirisha na kuwa ngao ambayo itautangaza utangaza utalii na utanzania zaidi.

Tangu kuasisiwa tena kwa mashindano haya TAnzania imekuwa msindikizaji ingawa kiukweli Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo akina dada wake wanavutia sana (Sitaki kuingia sana ndani  kwa hili).

Pamoja na umaarufu na unyeti wa mashindano haya bado mi nakwazwa na mtindo uliopo sasa wa kuwa na muandaaji mmoja tu mashindano haya nadhani ipi haja ya Serikali kupitia Wizara husika ya Habari, Vijana na Michezo pamoja na Wizara ya Utalii kuratibu mashindano haya, yakawa yanaendeshwa na watu ambao wataomba zabuni kupitia wizara husika na kila mwaka watu wanaomba ili kuleta mawazo mapya kwenye tasnia nzima ya ulimbwende nchini.

Nasema hivi kwa sababu, sekta hii kwa sasa inapata udhamini mkubwa pengine kuliko mchezo wowote na kiukweli kama kungekuwa na jitihada za ziada kwa ajili ya maandalizi na scouting ya kutosha inafanyika hata kuwashawishi watu wengi zaidi waingie kwenye mchakato mashindano haya yasingeshuka hadhi kama ilivyo sasa na tungeweza kupata watu wenye vigezo vinavyotakiwa katika kuitambulisha na kuiwakilisha nchi yetu.

NAfikiri kama kungekuwa na wazabuni wengi wanaomba na kutokana na vigezo fulani mmoja ana chaguliwa hii ingeleta upinzani ambao ungesababisha viwango vipande tuu.

Mashindano haya yamekuwa yakilalamikiwa na wengi kwenda mbali kuona kuwa walimbwende hawa wanaopatikana kutokana na mashindano haya wanakwezwa na mashindano yakiisha wanaachwa wakihaha bila kutengenezewa programu zenye maana kwa ajili ya kulitumikia taji lao. Hali hii inawafanya kuwa hawana utayari wa kuishi ndani ya taji ambalo mwisho wa siku huishia kutafuta mbadala wa kuingiza kipato ili waweze kuishi kutokana na hadhi ya umiss jambo linalowapelekea kupata kashfa za ngono na mapenzi yasiyokuwa na tija.

Kiukweli wizara husika ingefanya mrejesho na kukaa na wadau wa ulimbwende ili kuweza kutafuta njia bora zaidi ya kuyaendesha mashindano haya kwa ngazi zote.

Ni mtazamo tuu.

Advertisements

2 Responses to Inahitajika njia bora zaidi kuendesha mashindano ya ulimbwende.

  1. I want you to thank for the time of this amazing read!

  2. Right now it looks like Expression Engine is the preferred blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: