ALIVYOTOKA WAZEKWA!

Na The Romantic

Baada ya kuwa muandishi tu wa nyimbo za wanamuziki wakubwa wa Congo hususan Mzee Wembadio Shungu Mwalimu PAPA WEMBA na Papaa na Didistone Le Rambow Du Zaire KOFFI OLOMIDE katika chake chote akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka 1990-1995 ambapo alipata shahada ya pili ya uchumi (Masters in Economics) FELIX NLANDU WAZEKWA a.k.a.”Mokua Bongo”- (Part of the top portion of the skull which protects the brain) a.k.a.ambayo amepewa na mashabiki wake kuelezea kiwango cha busara za kisomi alizonazo mtaalam huyu wa uchumi, alianza kujiingiza mzima mzima  kwenye muziki akiwa solo mwaka 1996 baada ya kushauriwa sana na MZEE PAPA WEMBA na akafanikiwa kutoa album yake ya kwanza kwa msaada wa PAPA WEMBA na MADILU SYSTEM na baada ya hapo akaanza kukusanya wanamuziki katika jiji la Kinshasa ili kuunda bendi yake.Baadae akaendelea kutengeneza album lakini hazikuwa zenye mafanikio kutokana na muziki wake kuwa mgumu(ulikaa kisomisomi sana)kiasi kutopata umaarufu sana kwa wapenzi wakubwa wa muziki ambao ni watu wa kawaida ingawa aliweza kutambulika na wataalamu wa music kwamba anafanya muziki wa ukweli lakini sokoni hali haikua nzuri.

Hakukata tamaa akaendelea kuproduce albums chini ya JPS PRODUCTIONS kama producer wake lakini hali ikawa ile ile isiyo ya kuridhisha ama mbaya tu sokoni kutokana na sababu iliyotajwa hapo juu na pia kulikua na hujuma ambazo inasemekana alikua akifanyiwa na mzee wa fitna KOFFI OLOMIDE,JPS hawakuridhishwa kabisa na kusuasua kwa album za WAZEKWA sokoni lakini kwa kuwa walikua wakijua anafanya muziki wa ukweli bado wakaendelea kumvumilia na kumpa muda zaidi.

Baadae rafiki yake mmoja wa karibu akiitwa KAFFE ETIENNE TSHIMANGA akamfuata na kumuweka kitako kisha akamg’ata sikio kwamba muziki wa CONGO bila ushirikina hutofanikiwa kamwe,ni lazima uanze kutumia uchawi,lakini bwana TSHIMANGA alikumbana na upinzani mkali sana kutoka kwa msomi huyu wa uchumi ambae ni mtu mwenye imani kali sana katika dini yake ya kikristo ingawa baada ya ushawishi mzito inaelezwa alibali ushauri huo na album yake baada ya kufanya ushirikina ilitoka 2001 kidogo ikapata mafanikio,lakini bado WAZEKWA hakuridhika na mafanikio hayo madogo akawa anapanga kuachana na muziki baada ya kuona amejitoa sana lakini mafanikio hayaridhishi kabisa,lakini rafiki yake TSHIMANGA akawa anaendelea kumtia moyo akomae kwenye game atatoka tu.Baadae kidogo akapata deal la mkataba na PRIMUS,hapo akapata moyo wa kufanya kazi zaidi na kuanza kuona mwanga wa mafanikio huku washabiki nao wakianza taratibu kumfuatilia na kumkubali japo wanamuziki wakubwa wa Congo hawakumhesabu kama ni mmoja wa wanamuziki tishio au mshindani kwao.

Likaja Tamasha la FIKIN 2004,hapo kamati yake ya ushindi ikiongozwa na rafiki yake wa karibu bwana TSHIMANGA ikajipanga vilivyo kwenye mambo ya ushirikina wakiamini hii ndio nafasi ya mtu wao kutoka na kuheshimika na wanamuziki wakubwa wa CONGO kama ni mmoja wa wanamuziki wakubwa pia na pia sponsors wakawekeza pesa nyingi kwake kwa lengo la kushindana na wapinzani wao wakubwa wanaozalisha product kama ya kwao SKOL(Primus na Skol ni kampuni za bia).Lengo kubwa likiwa ni kumfunika WERRASON ambae alikua akidhaminiwa na SKOL.

Lakini kama kawaida WERRASON nae sio mwepesi kwenye mambo ya juju akawa na mambo yake lakini inaonekana TSHIMANGA ambae alikua werrasonique mzuri tu alizijua “nguvu” za WERRASON zilipo amabzo alikua akizitumia kwa miaka kibao kumfunika JB MPIANA Kila wanapokutana kwenye maonyesho face to face kwani siku hii walipokutana face to face WAZEKWA alimfunika mbaya WERRA na MAISON MERE yake kwa kuwapa kibano cha  ukweli (watoto wa kin wanaita FIMBU,Kiswahili FIMBO)kitu ambacho kilimuudhi sana WERRASON ambae siku moja baada ya hiyo face to face ya WERRA na WAZEKWA alimtumia ujumbe mzito KAFFE TSHIMANGA kwamba asifanye tena mchezo alioufanya jana yake,TSHIMANGA akawa anasakwa na Mawerrasonique ikabidi aikimbie Kinshaa lakini huku nyumba tayari kamuachia ushindi mnono WAZEKWA ambae kutokea hapo wanamuziki wote wakubwa wakaanza kuhofia kupambana nae ana kwa ana stejini.

WAZEKWA na TSHIMANGA hata hivyo si marafiki tena.
Muziki wa CONGO mpaka uwe star una mambo mengi sana, msione vijana wenye vipaji wanaachana na wanamuziki wakubwa kuanzisha bendi zao lakini wanapotea kwenye ramani, sio rahisi kiivyo.

Advertisements

26 Responses to ALIVYOTOKA WAZEKWA!

 1. Stivin says:

  Hahaha! nasikia wakati Wenge inavunjika JB Mpiana alimuita Werra pembeni akamwambia unataka kuwa kiongozi wa Wenge? fanya ntakalofanya, akatapika chura halafu akammeza, Werra mbio!

  • mwana paris says:

   Ni hadithi za mitaani hakuna ki2 kama hicho japo ni kweli ushirikna upo sana,nadhani unaelewa kwanini werrason hapatani na ndugu zake wakijiji kimoja ambao walipata kuwa watu wake wa karibu mno alipoanzisha wmmm yeye na kina adolphe,ndugu zake hao ni Jean Marie paul “le roi pelee” na kakake King Kester Emenea,fuatili kisa cha ugomvi wao ndio utajua kwenye ushirikina kwa wanamuziki wa congo hakuna aliesalimika.

 2. RICHARD MALEWA says:

  Unajua hawa jamaa wanachekesha saaana bwana Stivin halafu huyu jamaa nafikiri ni mwepesi wa kusahau. Katika blogs zake za nyuma yeye mwenyewe aliandika kwamba Werrason Mke wake ni Mlokele na kabla ya Kutoa Album yake Lazima awekewe mikono na Askofu pamoja na kupata maombezi matakatifu toka kwa Mkewe pamoja na yeye mwenyewe ili ALBAM yake ifanikiwe!

  Kataa na hilo na huo ukurasa tutautafuta na kuweka hapa mambo hadharani.

  Ila kama alivyosema Bwana Stivin huko nyuma inasemekana Werrason, JB Mpiana, Blaise Bula walipelekwa kwa Mganga ili wapate mafanikio na Mganga akasema inabidi Mmeze Chura aliye hai. Werrason na Blaise Bula pamoja na Domininguez walikataa ila JB Mpiana alimeza chura hai na jamaaa wakamwogopa kweli kweli na kumwachia awe Rais wa Bendi.

  Hiii msg usi-delete wala kuificha kwa faida ya wasomaji wasio jua habari za muziki wa Congo-Kin. Kama “imbwai imbwai tu!”

  • Hadj le Jbnique says:

   KWANINI ALIPOAMBIWA NA “MUNGU WAKE” DIDI KINUANI AENDE KUSHIKANA MKONO NA KOFFI ALIKATAA NA KUSEMA KAKA UNATAKA NIKASHIKE MOTO?
   SIO HADITHI KAMA UNAJUA LINGALA TAZAMA VIDEO HII MPAKA MWISHO,UMSIKIE,TENA DIDI KINUANI AKAMSHANGAA WERRA KUSEMA MANENO HAYO,AKAWAMBIA WERRA,WEWE MKE WAKO SI NI PASTOR,MKUBWA WAKO SI NI MTUMISHI WA MUNGU NA WEWE SI HUWA UNADAI MTU WA MUNGU MBONA UNAAMINI USHIRIKINA SASA KWAMBA KUSHIKA MKONO WA KOFFI NI SAWASAWA NA KUSHIKA MOTO???WERRA KIMYA,FUATILIA HAPA KWENYE VIDEO,”TOZALI BISO NYONSO BANA MBOKA MOKO”HAYO NI MANENO YA DIDISTONE,KAMA HUNA MUDA TIZAMA KUANZIA DK 9:42..!TENA NA NYIE WAPENZI WA WERRA DIDI STONE AMEWATAKA NA NYIE MUENDE MKASHIKANE MIKONO NA MASHABIKI WA KOFFI,ONA WERRA ANAVOTIA HURUMA BAADA YA AGIZO HILO LA BOSS WAKE..

 3. Anonymous says:

  kwani lini habari ilifichwa hapa?we ndio huwa unajificha leo sijui umeibukia wapi sijui,tatizo nyie wewe na huyo mwenzako steven ni watuu wa werrason sio watu wa muziki,that is the problem,utaona wazi kwamba leo issue hapa ni jinsi wazekwa alivyosota mpaka kuja kutoka kimuziki kitu ambacho ni cha kweli kabisa lakini hamumjadili wazekwa mnamuota werra na jb,kazi mnayo

 4. MPENDA MUZIKI WA CONGO says:

  WADAU STIV NA MALEWA ASIWADANGANYE MTU HAKUNA MWANAMUZIKI WA CONGO ASIYETUMIA UCHAWI TOKA ENZI ZA KINA FRANCO ATAKUWA HUYU WERRASON?

  LICHA YA WACONGOMAN KUWA WATU WENYE IMANI KALI SANA YA UKATOLIKI LAKINI MAMBO YA ASILI HAWAACHI KWENYE KILA JAMBO IWE MPIRA,NDONI,MUZIKI NDIO ZAIDI N.K.HUYO FALLY IPUPA UKIAMBIWA BALAA ALILOFANYA MPAKA MKAJUA VILE ALIVYO UNAWEZA KUZIMIA

 5. RICHARD MALEWA says:

  Ahaaaaa! Mkuki kwa Nguruwe! Alivyosema kushika moto maana yake kwanini ufanye suluhu na “Mchawi” wa maendeleo yako maana Koffi kafulia na alikuwa anataka ku-force kolabo na Werrason ambaye yupo matawi ya juu.

  Kwa nini mpaka leo naye JB Mpiana hajafanya Kolabo licha ya kuombwa na Papa Fololo Quadra Korra Man.

  Ninyi wenyewe ndiyo wenye kigeu kigeu mara “Tolingana”, “Tolingana” mara Cha Mutu Cha Mutu!

  Kijembe kinajibiwa na Kijembe wala siyo Koleo!

  • Rutashubanyuma says:

   mna tatizo la kuchanganya mambo,kwenye hii topic jb anahusika vipi????issue hapa ilikua mumzungumzie wazekwa na jinsi alivyofanikiwa kwa kumcharaza bakora werrason akiwa juu enzi hizo,kitu ambacho ni kweli kilitokea na ikawa ndio sababu ya werra na wazekwa kuwa madui mpaka leo.

   werra hapendi kushindwa ukimshinda kidogo anakununia moja kwa moja..niambie ukiacha jb werra sasa hivi anapatana na mwanamuziki gani mungine mkubwa wa congo????

   • Stivin says:

    Wanamuziki wakubwa wa Kongo wote hawapatani! Koffi alikuwa mshikaji wa Werra enzi ya BCBG, na inasadikiwa alimsaidia wakati werra, anaanza, shida ilitokea pake Werra alipoanza kumfunika Koffi, Koffi akaanza kuiga mambo ya Werra, Kumbuka Werra alikuwa na Best combination ya animation in Bill and Celeo, Koffi nae akatengeneza ya kwake kama hiyo ya Kerrosene na Brigade. Koffi ana ana Wivu sana, alikuwa adui wa Mpiana wakati Mpiana yuko juu, Mpiana alipofulia na kuanza kutoa malbamu ya hovyo kama Anti Terro uadui ukaisha, kumbuka ant- terro ilikuwa mahsusi kwa ajili ya Monde Arab

 6. Hadj le Jbnique says:

  Hata hivyo koffi sio mtu wa kumbeza jamani,licha ya matatizo yake yote bado ni mwanamuziki mwenye kipaji cha hali ya juu,mimi namuheshimu sana…

  Hebu tizama na kusikiliza kipaji hiki hapa anachokionyesha hapa bila ya msaada wa machine za studio,halafu niambie werra anaweza hii…tuwe wakweli tu…

 7. Hadj le Jbnique says:

 8. Hadj le Jbnique says:

  Sasa hebu fananisha na huu muziki wa werrason…je nani kati ya koffi na werra anafanya muziki kwa kutizama hizo video za koffi na hii ya werrason,wakati mwingine msidhani tunamchukia werra no,tatizo ni aina ya muziki wake…haueleweki…!Hata mkikasirika mawerasonique mi sijali lakini huo ndio ukweli

 9. Hadj le Jbnique says:

  Hata aina ya washabiki wake mnaodai huwa wanajaa ukiwatizama tu mwenyewe unaona ni watu wa aina gani………

  • Stivin says:

   Hadji sawa, lakini Werra ana mashabiki wengi kuliko mwanamuziki yoyote wa Kongo naongelea fact, tazama kibao cha temps present kimeangaliwa na watu 1,549, 000 niwekee cha mpiana hapa kilichofikia idadi hiyo ya mashabiki acha abdakadabra zaq Koffi!

 10. Hadj le Jbnique says:

  msikie tena hapa papaa na didistone papaa na delpirlo na muziki wa wastaarabu…

 11. RICHARD MALEWA says:

  He is the best kwenye MUZIKI wake wa Tchacho! kwa hilo tu hana mpinzani !

 12. mchambuzi wa muziki says:

  koffi yuko juu sana,kamuacha werra kwa umbali wa kifo na usingizi,hii unaweza kuiona tu kama utaweka usahbiki pembeni na kutizama hizi video live za wote hapa,mwanamuziki wa ukweli utamjua kwenye live,hii nakubali ni kweli kabisa,muziki wa studio unawabeba hata wasio na vipaji

 13. ALLY says:

  Hivi jamani koffi mnamjua au manongea tu kwa Congo hii Mopao Mokonzi yuko juu kwa kila kitu yaaani kimuziki, faranga etc usifananishe Manchester UTD na LIPULI ya iringa jamani

 14. Anonymous says:

  hivi mewahi kumsikia werrason akiimba wimbo mwanzo mpaka mwisho peke yake?

 15. Right now it appears like Drupal is the preferred blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

 16. Ellyn Thury says:

  Great facts, exceptional and precious design, as share great things with excellent tips and ideas.

 17. Trena Grove says:

  By my observation, shopping for electronics online may be easily expensive, nonetheless there are some tricks and tips that you can use to acquire the best products. There are usually ways to locate discount offers that could help to make one to buy the best electronic devices products at the cheapest prices. Great blog post.

 18. The when I read a weblog, I’m hoping which it doesnt disappoint me approximately this. After all, Yes, it was my method to read, but When i thought youd have something interesting to say. All I hear can be a number of whining about something you could fix if you werent too busy in search of attention.

 19. Thanks for your personal marvelous posting! I really enjoyed reading it, you may be a great author.I will always bookmark your blog and will eventually come back from now on. I want to encourage yourself to continue your great posts, have a nice morning!

 20. Admiring the dedication you put into your site and detailed information you present. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed material. Great read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

 21. This would be the right blog for everyone who hopes to be familiar with this topic. You already know a great deal of its practically difficult to argue together with you (not too I personally would want…HaHa). You actually put a fresh spin on the topic thats been written about for years. Great stuff, just excellent!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: