KULIKONI WATA NA WMMM…

Na The Romantique,

Spoti Starehe Die Hard Fun

Kumekuwapo na tetesi toka mwishoni mwa mwaka jana humu ndani kuhusu mwanamuziki wa WMMM Kijana Herritier Watanabe a.k.a. WATA kwamba hayuko tena bendi hiyo;uvumi huo uliwasabishia usumbufu mkubwa mashabiki wa  WATA binafsi pamoja na wenge maison mere kiujumla,lakini ukweli ni kwamba WATA bado yumo kundini Maison Mere ingawa kulikua na kutoelewana kidogo kati yake na muajiri wake kuanzia katikati ya mwaka jana,lakini sintofahamu hiyo iliyotokana kwa kiasi kikubwa na WATA kutaka kutoka na album yake solo nje ya kundi huku akiendelea kuwa muajiriwa wa bendi ilimalizwa na uongozi wa maison mere chini yake Le Roi D e la Forret papaa na Exocee Noel Ngiama wa Makanda a.k.a. WERRASON na hatimae kijana kuamua kubaki kundini.

Kiufupi ni kwamba kijana amekua na shauku ya kutoa album yake since 2008 lakini mzee mzima WERRA inasemekana akawa akimbania kiaina kwa kumwambia bado hajakomaa;lakini sasa kibali kimeshatolewa na WERRASON na dogo amepewa opportunity aliyoililia kwa muda mrefu ya ku release solo album yake lakini WERRA amemwambia kwamba sio kwamba anataka album hiyo iandaliwe vizuri taratibu ili ishiishie kuwa “flop”…hii maana yake nini?ni kwamba kijana atalazimika kusubiri mpaka WERRA atoe album yake ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka album hiyo ya Mzee mzima WERRA sasa itatoka mwakani may be hii ni kutokana na kwamba SUITE EN FIN-MALEWA 2 imeelezwa itakua released mwezi huu wa March!!!kila siku kalenda imekuwa ikisogezwa mbele kuisubiri album hii.Lakini dogo yeye tayari anazo nyimbo za kuitosha album yake hiyo solo.

Hapo chini dogo anaeleza mambo mengi ikiwemo ajali ya WERRASON mwishoni mwaka jana na pia anaeleza pongezi mbalimbali ambazo amekua akizipokea kutoka kwa wakongwe wa muziki wa Congo kama Felix Wazekwa,Koffi Olomide na hata JB Mpiana kufuatia kibao chake kikali REMISE ET REPRISE a.k.a.Tressor Mputu,ambapo kuhusu JB dogo anasema alimpa pongezi mbele ya kundi lote la WMMM wakati Jb alipokwenda hospitali kumjulia hali WERRASON alipopata ajali last year,anasema baada ya kumuona mgonjwa Jb kabla ya kuondoka maeneo ya hospitali alitumia muda mrefu kuongea na wana maison mere ambapo alisikika akisema “Heritier hongera sana wimbo wako ni mkali” ambapo dogo anasema anajisikia furaha sana kupata pongezi kutoka kwa ma artist wakubwa kama JB,KOFFI na WAZEKWA.

Hivyo Bana MAISON MERE hamna haja ya kujisikia unyonge,WATA ambae anasema hamuohofii msanii yeyote ndani ya WMMM ya sasa isipokuwa anakiheshimu kikosi cha dhahabu cha maison mere kile cha FERRE GOLA na wenzake ambao anawachukulia kama walimu wake bado yupo kundini.
Ndani ya MAISON MERE anasema yuko karibu zaidi kiurafiki na PAPPY KAKOL ambae walifahamiana kabla ya kukutana WMMM,Pia rafiki zake wengine ni ALI MBONDA na TADDET.
Nje ya WMMM washkaji zake ni JDL,GINO,ABRAHAM MIGNON na SEGUIN MIGNON(Wenge bcbg) na kaka zake kimuziki ALAIN na BOURRO MPELA

5 Responses to KULIKONI WATA NA WMMM…

 1. mkemiemi,kigoma ujiji says:

  BANA MAISON MERE MKO JUU KAMA HERITIER BADO YUMO BASI MAMBO BIEN..

 2. Anonymous says:

  Nmapenda sana wata kwa kweli,anaibeba sana bendi..

 3. mwana zamba says:

  watu wa mpiana walikua wanatusumbua sana juu ya hii kitu bora umevunja ukimya na kuweka mambo hadharani kijana bado yupo yupo sana ndani ya maison mere kwa mzee ngiama igweeee

 4. mamaa pasteri(pastor) says:

  Ha haa haaaaa le roi de la forret ametisha..kumbakisha wata kundini bonge la achievement maana nasikia koffi alianza kumvizia lol…

 5. June Salmond says:

  Wonderful info, great and valuable layout, as share fantastic things with fantastic strategies and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: