AMIDA SHATUR VS SYLVIE MAMPATA

Nadhani majina haya mawili si mageni masikioni mwa wapenda muziki hususana wapenzi wa muziki wa  CONGO ya Joseph kabila wa kabange zamani ikiitwa ZAIRE,Naamini mmekua mkiyasikia sikia sana katika nyimbo mbalimbali za JB mpiana Tshituka na Werrason Ngiama Makanda.
image

Mamaa Amida Shatur, Amida Mpiana

Nikianza na AMIDA SHATUR,Huyu ni mwanadada mrembo sana mwenye asili ya Lebanon,monekano wake ni kama mwarabu fulani hivi,huyu ni mke wa LE SOUVEREIGN PREMIER SALVARORY DE LA PATRIA JB MPIANA TSHITUKA,Mwanadada huyu walitengana na JB kwa takribani miaka nane mpaka mwaka ndipo waliporudiana tena ili kuwalea watoto wao watatu waliowazaa pamoja ambao ni DAIDA MPIANA,SORAYA MPIANA(WA KIKE) na wakiume mmoja aitwae MPIANA JUNIOR.

Lakini  Kama utaitizama vizuri picha hapo chini ya JB akiwa na familia yake utaona kuna mtoto mdogo wa kiume amebebwa kwa pamoja na JB pamoja DAIDA,Basi huyo ni mtoto wa AMIDA Aliemzaa na DIDI KINUANI(DIKIN),mtoto huyo anaitwa DIAM,jina ambalo kirefu chake ni DIDI AMIDA,upo hapo mzee?
19436_100192180015309_100000735813655_2578_437s2194_n

Kwa kumbukumbu tu,AMIDA alipotengana na JB aliolewa na tajiri mmoja mkubwa wa almasi mzaliwa wa sehemu moja maarufu kwa upatikanaji wa madini mbalimbali hususana almasi,sehemu hiyo ipo ndani ya congo inaitwa KAFUFU,tajiri huyo si mwingine bali ni DIDI KINUANI a.k.a.DIDI STONE(Kibongobongo didi mzee wa mawe), kama umewahi kusikia KOFFI OLOMIDE anataja kwenye nyimbo zake Jina DIDI STONE,Basi asili ya hilo jina ni huyu bwana japo KOFFI pale anakuwa anamtaja mwanae kipenzi aliempa jina la DIDI STONE ili kumtukuza huyu bwana DIDI KINUANI,

Lakini mwisho wa siku penzi la ukweli halinunuliki hata uwe na pesa kiasi gani unaweza kununua kila kitu lakini si penzi la ukweli,hicho ndicho kilichotokea kwa DIDI KINUANI,AMIDA akaamua kurudi kwa mwanaume ambae pengine ndio wa maisha yake,i don’t know!

Exoce Ngiama Makanda


Tuachane na Amida,tuje kwa Mwanamama SYLVIE MAMPATA “mama pastor”,huyu ni mke wake NOEL NGIAMA MAKANDA “WERRASON” ambae ni mtoto wa  tajiri mmoja mkubwa sana ZAIRE enzi hizo akiitwa SACRAMENTO MAMPATA,kama mmewahi kusikia MZEE TABU LEY kuna nyimbo alimuimba mzee huyo,alikuwa mfadhili mkubwa wa TABU LEY NA AFRISO yake.,WERRASON na Mkewe huyo wanae binti yao mkubwa anaitwa EXOCE NGIAMA,mtoto mzuri pua ya kitutsi kama mzee wake,mpaka sasa nataka kuamini werra kweli ana asili ya KITUTSI kama ambavyo imekua ikivumishwa ndani ya KIN na CONGO kiujumla.

HAO NDIO AMIDA SHATUR NA SYLVIE MAMPATA,WATU WASISHANGAE KUONA WANATAJWA SANA NI WATU MUHIMU SANA KWA JB NA WERRA.

Shukrani kwa BeeCeeBeeGeeQue nambar one “The Romantic” CIAO.

Hizi habari zimekuwa zikiombwa tena na tena, kwa ushauri tu kama kuna ulichowahi kukisoma na kikakuvutia unaweza kukipata kwa kutumia search box kulia kwa blog hii ukakisoma tena.

Advertisements

32 Responses to AMIDA SHATUR VS SYLVIE MAMPATA

 1. Hadj le Jbnique says:

  ASANTE SANA.NAOMBA IKIWEZEKANA,UTUWEKEE WIMBO WA BCBG ULIOTUNGWA NA MTAALUM WA SOLO BURKINAFASOO UITWAO SERGE PALMI UPO KATIKA ALBUM YA TITANIKE(TITANIC),BONGE LA WIMBO JAPO NASIKITIKA HAUKUPATAGA PROMO YA KUTOSHA KAMA TITANIC WENYEWE NA RDC AMBAZO ZILIKUA KATIKA ALBUM MOJA NA HUU SERGE PALMI,HEBU TAFUTA UUSIKILIZE KWANZA THEN UTANIAMBIA,JINSI WAZEE WA MASAUTI WA UKWELI JB,EMELIA NA AFANDE MPELA WALIVYOKAMUA KIUKWELI NAD THEN USIKIE KITU CHA SOLO GUITAR MZEE MZIMA MWENYE WIMBO WAKE BURKINABEE ALIVYOFANYA KAZI,ACHA KAKA,MTU AKIUSIKILIZA WIMBO HUO HALAFU ASITIKISIKE KWA KUCHEZA BASI JINI,ATAKUA SI BINADAM WA KAWAIDA,MFIKISHIE SALAMU HIZI YULE MAMAA WA BAMBATAA AKICHEZE KIBAO HIKI AKIPE PROMO,WATU WANAWEZA DHANI KIPYA WAKIKISIKIA

 2. Dr. Maige says:

  Mi ni mpenzi mkubwa sana wa Blog hii hasa habari hizi za Wera na JB huwa zinanifariji sana.
  Shukrani za pekee kwako Papaa Pius kwa support.
  Dr. Maige – Bruxells.

 3. bidada says:

  mie ni moenzi mkubwa wa blog yako ila ningekushauri uwe unaongea na watu wa karibu wa jb na werra kabla haujaweka hizi habari zao. stori ni karibia na ukweli lakini picha ya silvie mampata ni ile ya kwanza werra ameketi. hii ya pili baada ya amida sio. pili ni baba yake alikuwa anaitwa sacramento,,,,mampata ni jina werra alimpa mke wake mampata inaashiria pesa….kwa lugha ya kwao.

 4. Hadj le Jbnique says:

  Bi dada naona hujaelewa,picha ya sylvie sacramento ni ile ya juu akiwa na werra hii ya chini baada ya picha ya amida shatur na pamoja na ya chini yake ya familia ya jb,hakusema ni picha ya syvie jaribu kutizama vizuri,alichosema hiyo ni picha EXOCEE NGIAMA,Huyu exoce ni binti yao werrason na Sylvie wala sio mke wa werra,na haijaandikwa popote kwamba huyo ni mkewe.Haya mambo ukiwa unayapenda tu utayajua wala haihitaji kuwa karibu na wahusika,ndio maana leo unaona kuwa watu wanakuelezea habari za christian ronaldo au david beckam ama JAY Z licha ya kwamba hawako karibu nao abadan,

 5. Hadj le Jbnique says:

  Na hapo kwenye picha ya jb na familia yake,kutoka kushoto kwenda kulia,wa kwanza ni DAIDA MPIANA(Binti ya Jb na Amida),JB MPIANA mwenyewe,AMIDA SHATUR(mkewe JB)na SORAYA MPIANA(Binti yao mwingine).Aliyechuchumaa anaitwa MPIANA JUNIOR ambae ni mtoto wao wa kiume.Najua wengi mtajiuliza aliebebwa ni nani?jibu hili hapa huyo aliebebwa anaitwa DIAM DIDI KINUANI,Huyo ni mtoto wa Amida aliemzaa na DIDI KINUANI pindi walipooana,na hilo jina DIAM ni kifupi cha majina DIDI + AMIDA = DIAM

 6. bidada says:

  hio pia sio picha ya excosee kabisaaaaa…. na pia stori sio kama unavose,a we hadj.

 7. Hadj le Jbnique says:

  Nimekusoma bi dada,japo sijaelewa stori ipi sio,pengine ungekuwa specific ni stori ipi?kuhusu picha naweza kukubaliana na wewe kwa kuwa huyu mdada anaonekana mkubwa na pia hafanani sana na werra,exocee ninaemfahamu mimi ana pua ya kitutsi kama mzee mzima werra na wamefanana sana na babake so hapo kidogo naweza kubali blogger alikosea kidogo,ila kama mtu anataka kumjua ama kupata picha nzuri ya EXOCEE NGIAMA MAKANDA pamoja na ya DAIDA MPIANA TSHITUKA nenda kwenye GOOGLE then search DAIDA MPIANA AND EXOCEE NGIAMA utaipata picha nzuuuuri bi dada ondoa shaka

 8. sadiki tiger says:

  Kweli JB ana mapenzi ya kweli kwa Mama Shatur yaani pamoja na kumsaliti kwa Didi Kinuani bado kaweza kumrudia! ni wanaume wachache wenye huo moyo!

  Hivi Burkinabe yupo wapi siku hizi? Mimi ndiyo maana zaidi ya African Bambataa na baadhi ya vipindi siku za weekend nilishaachana na vipindi vya watoto na bongo fleva zao!

  Ukweli ni kuwa siyo tu ni vitu ambavyo havikupata umaarufu kwenye Titanic mbona vipo vingi kutoka DRC toka kwa manguli wengi lakini hawa watoto wa siku hizi wanavijua?

  Any way wamekaa kibiashara zaidi lakini ukweli TVs na Radio zetu zimetupiga bao. I wish tungekuwa na TV channel kwa ajili ya hizi ngoma za ukweli ukweli siyo hizi Za kichina za kwenye studio au hawa mavuvuzela wanaonakili kazi za watu toka DRC kisha kazi kuita majina ya watu kwenye steji ili wajipatie Riziki zao.

 9. jamali sisi says:

  safi sana blog yako iko poa kwetu tunao jua mangoma ya ukweli hivi wapi walipo m2mzima BUKINAFASO KASONGO,EMILIA ELONGO,fIKARE MWAMBA NA WILIE BWAPAPA WA WENGE EL PALRIS BILA KUMSAHAU SUZUKI WA AKADEMIA NAITWA JOMARI

 10. Hadj le Jbnique says:

  Papaa Jamali ndenge nini papaa,ozali malamu?merci papa.

  Mbokalia a.k.a.Burkinafaso kassongo kwa sasa anaishi London akipigia bendi moja yenye makazi yake huko ikiitwa GRUPO LOKITO.Ni bendi inayojumuisha wanamuziki wa kicongo,kilatin na waingereza pia.Inapiga congo rhumba na sebene pia nyimbo za kilatin ikiongozwa na muimbaji mcongoman JOSE HENDRIX NDELO.Aimeli Lyase “Demingongo” yeye yuko WMMM ya Le Roi De la Forret werrason,Maitre Ficare Mwamba bado yuko na JB MPIANA ingawa kwa sasa anajiandaa kutoa album yake kama solo artist lakini still yupo BCBG jamaa hajawahi kutunga wimbo mbaya toka Djodjo Ngonda mpaka kitu Le spoir de chicago ambacho binafsi nakikubali sana,lakini kwenye hii album mpya ya BCBG soyon serieux hajatunga wimbo hata mmoja kati ya nyimbo 19!labda kwa kuwa amebanwa na album yake binafsi,SUZUKI baada ya kupiga deiwaka BCBG Baadae alitoa album yake binafsi akimshirikisha YOMBO LUMBU a.k.a.Tutu kaludji le number one,haikufanya vizuri sana sokoni japo ilikua nzuri,baadae akapumzika kidogo then swahiba wake Koffy olomide alipokimbiwa na FALLY IPUPA alimfuata suzuki na kumrudisha kundini QL.Suzuki 4*4 ana uwezo mkubwa sana sema tu hana bahati,Hebu click link hiyo hapo chini upate kitu chake “GALERIE” uone alivyocheza na sauti,mwenyewe utakubali.

  Tikala Malamu papaa!ciao

  • Stivin says:

   Aimelia Lyase alishaondoka WMMM siku nyingi sana! alishindwa kukimbizana na vijana!

  • Mwalimu Mkumbe,Muheza,Tanga says:

   Huu wimbo nilikua naupenda sana lakini nilikua sijui jina lake,kumbe unaitwa Galerie….suzuki 4×4 aliimba vizuri sana kwenye huu wimbo.Nashukuru kujifunza mengi hapa

 11. Hadj le Jbnique says:

  DAIDA MPIANA (BINTI WA JB)na EXOCE NGIAMA(BINTI WA WERRASON)HAWA HAPA,WAANGALIENI VIZURI HAWA MABINTI WALIVYOFANANA NA BABA ZAO.

 12. Jamali says:

  Nimekukubali kwa ku2tuchimbulia mambo yaliyochini ya kapeti! Kwani napenda sana kujua,kwa undani habari zao wanamuziki wa kikongo hasa wale ma* nilikuwa sifahamu mambo ipo huku.endelea ku2pa uhondo kila siku by jamali tomaa

 13. MAMA TABU FATOU LA TANZANIANE says:

  kweli nimekubali mamaa amida shatur anatisha yuko juu,ni mrembo sana,pia ni kweli daida mpiana na exoce ngiama makanda kwenye video ya mdau hadj hapo juu ukiiplay wanaonekana vizuri walivyofanana na jb mpiana na werrason.

  Merci mingi bana Tanzanie

 14. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  Msaada tutani wadau wa lingala music,eti ni kweli jb mpiana alipokimbiwa na Amida alichanganyikiwa kiasi nyimbo zake nyingi alizotunga kipindi hicho zilikua ni za kumlilia mkewe huyo?

 15. muddy washington says:

  kweli jb anampenda huyo mwanamke yani licha ya kumkimbia na kwenda kuolewa na kuzaa na mwanaume mungine bado kamrudia…huo ni ubwege na udhaifu mkubwa tena na mtoto kaja nae kamwita Diam Kinuani,yani didistone amida kinuani bado jamaa halistuki tu

 16. mwajuma zungu says:

  Kumbe jb mpiana na werrason wana mabinti wakubwa na wazuri namna hii,nashukuru kwa taarifa nampenda sana mpiana japo siku hizi amekua kimya

 17. Jb Hanzuruni says:

  Mbona haujatuwekea picha ya mke wa werrason?nasikia ni pastor huko kongo hii ni kweli?

 18. Anonymous says:

  Ni kweli kabisa mamaa silvie mampata ni pastor huko congo,hapa chini utamuona akifanya mambo yake ya u pastor kwa wake mbalimbali wa wanamuziki wa zamani wa congo

 19. papa kasapira nakati ya london says:

  kwa mara ya kwanza katika ushabiki wangu wa muziki napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza werrason ngiama kwa kitenda cha kumkatalia mfadhili wake mkubwa didi kinuani kwenda kupiga live kwenye harusi ya didi kinuani na bibie amida shatur hapo phenomena umeonyesha utu

 20. Hadj Le Jbnique says:

  kweli kabisa kaka,unajua hata dunia ingemshangaa kama angeenda kwenye hiyo sherehe,si unajua wakati jb anamuoa huyo huyo Amaida yeye werra ndio alikua mmoja wa washenga!

  haya ndio mambo ya didi kinuani a.k.a. Dikini kwa wasiomjua wamuone hapa PDG huyo bilionea,hapo akitoa zawadi ya ng’ombe kwa ajili ya chrismas kwa walemavu wa kinshasa

 21. Anonymous says:

  ezamae naloki libala

 22. batAlAP says:

  439309 754664I believe other website proprietors ought to take this web site as an model, extremely clean and fantastic user friendly style and design, as nicely as the content. Youre an expert in this topic! 4910

 23. Anonymous says:

  Asante sana namsikiaga sana siliv

 24. Anonymous says:

  NAKUPENDA SANA

 25. Anonymous says:

  Silivi.mapata

 26. rolly kiala says:

  simplement que j’ai vu des phos sans rien comprendre à propos des texte pour plus de meilleur publication la traduction à toutes les lagues pourrais propulsé bien l’information.

 27. endjala bernhard says:

  hai werrason/noel ngiama m

  am in namibia now and i want to have your email address so that we can contact each other anytime. please reply me.

  thanks
  endjala.

 28. jacob majale says:

  you’ve enlighten me

 29. Anonymous says:

  exoce soit sage,

 30. derasonn maf says:

  nice family god bless you and protect all your family and everything you doing, like you so mutch. Thx bay.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: