Ezau wimbo uliomaliza ubishi wa umiliki wa wimbo wa Mulolo na Kin Ebouge

Kwa wafuatiliaji wa Muziki wa Kongo wanajua utata uliokuwepo kati ya umiliki wa nyimbo mbili za Mulolo na Kin ebougee ambazo zilibeba majina ya albamu huku wengine wakimtaja Ngiama Makanda kama mtunzi wa na mmiliki wa nyimbo hizo.

JB Mpiana alikuja na wimbo wa Ezzau ambao ulikuwa kwenye albamu ya Anti Terro ambayo kwa kiasi fulani haikutamba hapa nyumbani kwa kutokupata si tu promo bali hata airtime ya kutosha haikupata. Katika wimbo huu JB Mpiana anajifanananisha story yake sawa na story ya  Esau wa kwenye Biblia ambaye alikosa baraka za baba yake ambaye alikuwa kipofu na na alikuwa na manyoya mengi siku Baba aliomba aletewe mwanaye Ezzau ili ampe baraka kwa vile Esau alikuwa hapendwi na mama yake basi mama alimtuma porini na kumpaka manyoya kaka yake ambaye ni Yakobo na Baba alipomshika akajua ni Ezzau na akambariki.

JB Mpiana kwenye wimbo huu anasema histoir eshanjaka te zembo  nanga ya mulolo ebimisa wenge zembo nanga ya kin ebouge ekofirma wenge bolinga bolinga te yango wana akiimaanisha Story haitobadilika wimbo wangu wa Mulolo ndio ulioitoa Wenge, kisha wimbo wangu wa Kin Ebouge ndio ukai komfemu Wenge mtake msitake Stori haitobadilika, na kabla ya hapo JB Mpiana aliwataja mashahidi ambao anasema wanaujua ukweli huku akimtaja Papa Wemba, Presidaa Nyoshi aka Nyoka Longa na Josiki ya Mbukuta kuwa wanaujua ukweli huo.

Hivyo Wimbo huo unamaliza ubishi huo, Maneno yaliyokwenye Wimbo huu ni kama mahubiri ambayo kiukweli kila mtu na muumini anapaswa kuyasikiliza. Kwani anasema kuwa baraka zake zimetoka kwa Mungu ana kusisitiza Binadamu wapendane hakuna sababu ya kuchukiana.

JB anasema ukila pamoja na watu wanakuita ndugu mshkaji lakini siku ya siku unabaki kama Yesu Masia peke yako.

JB anasema Yesu alimfufua Razaro na watu hawakuamini, Mapenzi ni ya Mungu ingawa Mwili unarudi udongoni, mtafanya kila mfanyavyo akisema Mungu yatakuwa. Sichekagi matatizo ya mutu wala kutangaza ubaya kwa sababu nayajua yapo, mlitangaza kwamba nilikuwa Kichaa ili mniharibie kwa watu.

Anaongeza hata leo nikifa mtanikumbuka kwa kitu kimoja yule mwenye deni lake kwangu aseme hapa nimlipe… Kiukweli maneno ya Wimbo huu ni mazito sana. nitamtafuta Papaa Julie we Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama ili niwaletee wimbo huu mwanzo mwisho.

Anasema ukiwa na pesa wanakuja kwako wanajaa mnakula na kunywa zikiisha nyumba inakuwa kama iko Jangwani hakuna anayekuja, ukiwa unamatatizo na kuumwa hakuna anayekuja kukusalimia au kukusaidia wakisikia umekufa wanakuja na magari ya kifahari na michango wanatoa kukusindikiza kaburini, Kisha anaongeza kuwa yeye si kama Ezzau yeye ni kama Noah aliyeokoa viumbe vya dunia hivyo atawaokoa wote.

Merci Mingi Papaa Julie Weston Ilunga ntakutafuta tumalizie hii kazi.

Advertisements

9 Responses to Ezau wimbo uliomaliza ubishi wa umiliki wa wimbo wa Mulolo na Kin Ebouge

 1. Anonymous says:

  …naanza kupoteza hamu ya kusoma hii blogu maana naona ni ya mashndano kati ya jb na werrason,…hata hivyo mwandishi naona ni mshabiki mkubwa wa JB, kwani promo yake ni kubwa kuliko werrason,sijifichi ni mshabii mkubwa wa werrason,ingawa hatendewi haki humu…ukweli unabaki palepale jb kafulia…..siku hizi hana kitu

 2. Anonymous says:

  Sasa na wewe si uanzishe Blog yako ebooooo
  sisi tunafurahia habari tunazozipata humu hulazimishwi mtu na mapenzi yake anachambua MAn Cg=hester we unasema we Arsenal sasa unafata nini humo?
  KAka Pius tupe utamu vinginevyo kama una habari za Wera mtumie ataziweka
  Samahani mi si msemaji wa kampuni ila umenikera

 3. Anonymous says:

  Mdau hii ni blog iliyo na uwezo pengine kuliko zote,ndio maana hata wewe ukiwa na stori yako inayomhusu werra mradi iwe ya ukweli ukimtumia blogger kupitia e mail address yako akiisoma na kuiona ni ya ukweli inapata airtime hapa kwa kuwa published,jaribu kumtumia stori ya werra uone,tatizo watu wa werra walalamishi sana kama werrason mwenyewe…zikiwekwa stori za werra humu hata hamchangii ikiwekwa ya jb washabiki wake wanajitokeza kwa wingi kuchangia werrasonnique mnanuna…juzi tu iliwekwa stori na video ya werra akipewa dola 50,000 na mfadhili wake DIDI KINUANI,lakini hamkujitokeza hata kucomment kitu,leo kawekwa jb mnalialia..acheni hizo afterall kwa sasa hamfanyi vizuri,wanamuziki wengi kama Herritier wata ambao walikua wanaibeba maison mere wamemkimbia werrason kwa sababu ya uzurumaji wa pesa,inabidi mjipange,mpunda ya jb bado iko juu sana,malewe suite yenu imekosa mashiko kwa mashabiki…

 4. peter says:

  safiiiiiiiiiiiiiii

 5. Anonymous says:

  Hahaha, wimbo uliomaliza ubishi, kisa? umeimbwa na Mpiana Mungu mtu wa Majbinque, hivi kama wimbo ungekuwa wake kwa nini alalamike mpaka kutunga wimbo? hivi wewe mtanzania mkiimba na Mchina wimbo wa kiswahili anaweza kusema ni wake, Mulolo ni wimbo wa kabila la Werrason hiyo iko wazi, JB hajui lugha hiyo sijui aliutungaje? JB ni bwana mdogo sana kwa Werra, saizi ya Werra Kongo Ni Kofi Olomide na sio Petie Frere, hahahA! Ukitaka kuamini Werra ni wa Kimataifa Juzi alikuwa Harare kwenye Birthday ya Mugabe mbona JB hakualikwa? JB bwana mdogo sana kwa Werra, mpaka leo anangangania Mulolo kwa sababu hajawahi toa Wimbo wa maana toka Wenge isamabaratike, kama upo wimbo niambieni!!

 6. Larae says:

  Excellent post. Keep writing such kind of info on your blog.
  Im really impressed by your site.
  Hello there, You have performed an incredible job.
  I’ll definitely digg it and for my part recommend to my friends. I’m sure they will be benefited from this website.

 7. With this said, I would like to share with you camera bugs a few pointers that I have learned over the years.

  Because I have found that as a basic guideline, men do not invest in the type and style of photography
  I create. A professional photographer can assure clear
  and very well produced photographs compared to an average camera user when the aspects of consistency or
  extensive imaging options is at stake.

 8. obviously like your web-site but you need to take
  a look at the spelling on several of your posts. Several of them are rife with spelling problems
  and I to find it very bothersome to tell the reality on the other
  hand I’ll definitely come again again.

 9. Tashia Golab says:

  I want you to thank for the time of this fantastic study!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: