Ruge na Sugu mmemaliza tofauti vipi Wafuasi wenu?

image

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.

Niliwahi kuandika makala yangu juu ya umuhimu wa Ruge Mutahaba na Joseph Mbilinyi aka Mr II aka Sugu kumaliza tofauti zao na mstakabali mzima wa muziki huu wa kizazi kipya. Kama hukuwahi kusoma gonga hapa usome zaidi.

Katika makala yangu ile wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa juu ya makundi ama wafuasi ambao wako nyuma ya makundi haya. Nawaongelea Mabagafresh, Mkoloni, Dannymcmamo, Sumag, DWA Gheto, Mapacha, Hardmad, Soggy Doggy, Peenlawyer, Rama D, Adil, Sister P na Zay B, Mr Simple, nk watakuwa ktk hali gan? nauliza hivi kwa sababu hawa wote ni Antivirus ambao walikuwa ama kwa kujua ama kwa kutokujua wakiwa upande wa Sugu ambao walikuwa wanagombea haki ambazo Sugu alikuwa muwakilishi wao.

Leo hii wao wamepatana nani atawatetea hawa? Kimsingi unatakiwa kuwepo mkakati wa pamoja wa kuangalia ni jinsi gani kundi hili limewakilishwa kwenye mgogoro huu nia iwe si tu kumaliza mgogoro wa wakubwa wao bali makubaliano yao yawanufaishe na hawa ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza kuwa waathirika wa uliokuwa mgogoro.

Hivyo basi wakati bado habari hizi ni breaking news kwa wapenda burudani ingekuwa vizuri tungeelewa hawa mabwana wako kwennye kundi gani.

Vinginevyo napenda kuchukua nafasi hii kama mpenda burudani na mwana starehe kuwapongeza Mheshimiwa Nchimbi na Mheshimiwa Tindu Lissu kwa jitihada zenu kuwapatanisha hawa mabwana ambao kwa kiasi fulani wana ushawishi mkubwa kwenye sekta nzima ya burudani hasa kwa vijana.

5 Responses to Ruge na Sugu mmemaliza tofauti vipi Wafuasi wenu?

 1. Anonymous says:

  lakini piu we si ulisema vizuri sana tena kwamba ya RUGE na SUGU yanazungumzika,ndio yamezungumzika sasa,tatizo nini tena?

 2. Hadj Le Jbnique says:

  Hii ndiyo taarifa ya SUGU baada ya usuhishi na RUGE/CLOUDS FM

  Taarifa:kwanza poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa za ghafla za usuluhishi kati yetu na ruge/clouds fm,ni kutokana na unyeti wa issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa…kwanza naomba tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa vinega kwa maana kwamba ma…dai yetu yote ya msingi ndio yalikuwa msingi wa majadiliano na ruge amekubali kuyatekeleza yote…kuanzia suala la studio ya rais kurudishwa kwa basata ili iwe ya wasanii wote,pia t.f.u ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii yaani t.u.m.a kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na kukubaliwa kwa utekelezaji…haikuwa kazi rahisi,kwanza ilianza kwa wao kumpigia mwenyekiti wangu mbowe kutaka tukae chini,ambapo kamanda mbowe alinishauri tukae nao chini kama kweli wana nia ya kuyamaliza…baadaye wakampigia mr shigongo ambaye ni wazi kuwa ni kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na mr. Kusaga tu alinipigia na kunishauri hivyo hivyo…na kama haikutosha wakalifikisha hili suala kwenye kamati ya bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini…na hatimaye suala hili likaishia mikononi mwa waziri nchimbi pamoja na mhe. Tundu lissu(mp) kuwa wapatanishi wetu…waziri nchimbi akaanza kwa kumuita ruge dodoma na alikuja tukakaa kwa hatua ya kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya wizara ya utamaduni chini ya dr nchimbi na mhe tundu lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo…vita yetu ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanajaribu kuiweka,kwahiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa tunatakiwa kushukuru na kufurahia…lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa anti-virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wengine kama mameneja masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi lake… Asanteni sana…

 3. yenda rais says:

  ndio nyie mpatana sawa je awo wafuasi wako wananufaika na nini

 4. por favor, clique no próximo post

  Ruge na Sugu mmemaliza tofauti vipi Wafuasi wenu? | Spoti na Starehe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: