Koffi Olomide ashtakiwa nchini Ufaransa.

image

Mwanamuziki Koffi Olomide amefikishwa mahakamani kwa mara nyingine kwa makosa matatu yakiwemo udhalilishaji na kuwabaka wanamuziki wake wa kike.

Akiongea na shirika la utangazaji la AFP wakili wa Koffi Bw. Manuel Aeschlimann, Aidha habari zinasema kuwa Olomide alijipeleka mwenyewe kwa Judge siku ya jumatatu huko Nanterre ambako mashtaka hayo yamefunguliwa.

Habari zinasema kuwa Olomide aliondoka kurejea Kongo bila kusubiria hukumu yake kutokana na makosa yaliyotajwa. Pia wakili huyo alisema kuwa Olomide hana la kujibu kwa kuwa wanamuziki hao mashtaka yao hayana ukweli wala ushahidi ndani yake, kisha akaongeza kuwa wanamuziki hao walitaka kupata vibali vya kuishu nchini Ufaransa kwa kumchafulia mteja wake.

Advertisements

6 Responses to Koffi Olomide ashtakiwa nchini Ufaransa.

 1. Didier says:

  Tuache utani, huyu Koffi a.k.a. Mopao Mokonzi ni mbakaji kweli. Koffi hii tabia anayo sana!

 2. paul samara says:

  ukifanya utafiti wa kutosha utagundua kuwa tabia hiyo ya koffi ni ya wanamuziki wote,karibu kila mwanamuziki huwa anatembea na wanenguaji wake,haya malalamiko utayasikia kwa wanenguaji wa bendi zote,kwa kuwa mwanamuziki anakuwa ni bosi wa kundi anaamua kutumia cheo chake kuwataka kimapenzi wanenguaji au waimbaji wake wa kike,sio koffi peke yake.hata bendi za hapa bongo ni ivo ivo,mathalani fm academia kila mnenguaji ana bwana mle mle kwenye kundi,kazi ni kuchukuana tu,wakishaitilafiana tu, ndo utasikia mnenguaji kafungashiwa vilago.

 3. Stivin says:

  Hahaha! hata Werra kamchezo hako anako, amezaa na Gissele Yamamoto na Inadaiwa kuwa alitembea na Linda kabla ya kumpasia Kakol

 4. Anonymous says:

  na tafautiana na hayo koffi olomide ana nidhamu hawezi kufanya jambo kama hilo nini ame kosa seti yuko nazo ..marafiki yuko nao wapenzi wakimataifa..hawezi kuchukua mrembo gizani mashambani alafu amuvishe nguo nzuri kwa madhumuni ya mapenzi

  • Hadj Le Jbnique says:

   Vipi kuhusu cindy le coeur mbona kamchukua toka gizani tena kakiwa katoto sawa na watoto wake lakini kamfanya kama mkewe mpaka sasa?hii unaizungumziaje,na vipi watoto aliozaa na zina bilao yule mcheza show wake kibonge wa zamani enzi za ALTIMATUM na LOI,Koffi mchezo huo yeye ndio kazidisha akifuatiwa na werrason kwa karibu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: