GROUP DIKIN YAMPA SAPOTI WERRA!

WERRASON ALIPOPEWA MSAADA WENYE MASHARTI “MAGUMU” NA BOSI WAKE!

Na Hadj Le JBnique,Revere,Massachesetts,USA.

Tukio hili lilitokea miaka miwili iliyopita huko kinshasa ndani ya Le Grand Hotel ambapo mfadhili mkubwa wa Werrason n Koffi Olomide PGD Didi Kinuani wa Group Dikin alipopanda juu ya stage ya WMMM na kusimamisha muziki kisha akashika kipaza na kuutangazia umma kwamba yeye Didi kinuani baada ya kuombwa  msaada na mdogo Werrason alipoenda kupiga show huko nyumbani kwa Didi kwenye mji wa KAFUFU ndani ya DRC kwa ajili ya kutunisha mfuko wa foundation yake (werra) ameamua kumsaidia mdogo wake huyo (werra) kiasi cha fedha taslim dola za kimarekani elfu 50 palepale stejini.

Baada ya kumpa kiasi hicho cha pesa anamuagiza werrason usiku huo baada ya show akalale asubuhi akiamka anamuagiza(katumia neno cammande yo) awashe gari toka nyumbani kwake aende moja kwa moja nyumbani kwake Koffi Olomide  akamshike mkono koffi na kumwambia kaka naomba ugomvi mimi na wewe uishe kuanzia leo tuwe kitu kimoja tena aonekane kwenye tv akimshika mkono koffi kumuomba yaishe!

Baada ya kusema hivyo ukumbi mzima ulizizima kwa kuzomea na kupinga kitendo hicho kwa nguvu zote lakini Didi kinuani hakujali akaendelea kuwapasha mawerasonique ugomvi hauna mpango hata wao mashabiki wawatafute mashabiki wa koffi na kuwapa mikono ya heri kuwaeleza uhasama uishe wapendane wawe kitu kimoja;akaendelea kusema koffi ni mkubwa kwa werra hivyo werra anapaswa kumfuata koffi sio koffi amfuate yeye werra hiyo sio heshima kiafrika na pia kutia msisitizo akamwambia werra yeye mwenyewe pamoja na ukaka wake kwake lakini yeye Didi binafsi koffi ni baba yake kwa kuwa Koffi ana mtoto aliyempa jina Didi stone kwa ajili yake yeye Didi kinuani hivyo anamuona koffi kama kamzaa!!!!

hivyo basi yeye werrason kwa kuwa ni dogo wake anamuagize aende kwa baba yake(koffi) akamuombe yaishe,werra utamuona analeta ubishi kwa kujitetea akimuuliza didi,kaka hivi unaweza kumwambia mdogo wako ashike moto???yani kwa werra kupeanan mkono na koffi ni sawa na kushika moto!!hata hivyo utetezi wa werra haukukubalika kwa Dikin.hayo ndio mambo ya huko kinshasa na watu wenye pesa zao na masharti juu.Pata video ya tukio hilo zima kuanzia dk 02:35 uone dola elfu hamsini (50,000)zinavyokuwa cashed….

Baada ya hapo burudani zikaaendelea kama ifuatavyo mpaka asubuhi, Kinshasa raha bwana asikwambie mtu.

11 Responses to GROUP DIKIN YAMPA SAPOTI WERRA!

 1. Anonymous says:

  werra anaharibu na li sauti lake hapo kwenye video ya pili,angemuachia watanabe amalize mwenyewe na wenzake.

 2. Anonymous says:

  werrason kama kampoteza Heritier watanabe basi tena dogo ana kipaji sana huyu…

 3. Anonymous says:

  Burudani za wata zinaendelea hapa…

 4. Heritier says:

  Kinshasa kuna raha ni kweli ila wa kinois karibia ya wote ni washamba sana, miaka ya nyuma nilikuwa nawaona wacongo ni wajanja kumbe hamna lolote. Dar na Nairobi ni wajanja mno na hii miji inaipita Kinshasa tena saana tu.

  • Anonymous says:

   kweli kabisa jamaa sio wajanja wala nini halafu wenyewe wanakwambia kinhsasa ndio mji mkuu wa africa…wacongo bwana!ila kweli kiburudani raha sana,bendi kibao yani kuko live flani hivi

 5. Anonymous says:

  jamani jamani kumbe hizi bendi zetu za hapa bongo zinatuibia sana,hebu sikilizeni hiyo video ya pili anapoimba huyo watanabe kunazia dk 8:08 halafu mniambie wenyewe TWANGA PEPETA walivyotuibia bila kujua kwa kulichukua hilo sebene kama lilivyo kwenye nyimbo yao moja nimeisahau kidogo,wizi mtupu

 6. bcbg forever says:

  Naona wana “ZAMBA” siku hiyo watanabe aliwarusha mbaya…hngereni ma werrasonique mlikua juu sana kipindi hicho

 7. Faith Kollar says:

  I’ve bookmark your site and in addition add rss.

 8. Aide Merrih says:

  Extremely good web site and great and articles.beneficial design, as share good stuff with excellent strategies and ideas.

 9. You are a very persuasive writer. I am so glad I found your website.

 10. Currently it looks like BlogEngine is the top blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: