Umewahi kuiona "TSHOBO" ya Fally Ipupa na MJ 30?

Mwaka juzi JB Mpiana alipiga show pale Ubungo Blue Pearl Hotel akishirikiana na Tshala Muana, Alipopanda Tshala Muana alimtambulisha kwa mara ya kwanza hapa Tanzania mwanadada MJ 30 (Meje Thate) kibongobongo, Tshala muana alisema kwa muda mrefu alikuwa akisumbua kichwa kwamba kikiondoka kizazi chao yeye, Mbilia Bell na wengineo nani mwanamuziki wa Congo Mwanamke angekuja kuwabeba, na ndipo alipompata huyu mwanadada.

Hebu msikilize kwenye kibao hiki akishirikiana na Fally Ipupa kisha niambie.

Pata kitu………..

Advertisements

3 Responses to Umewahi kuiona "TSHOBO" ya Fally Ipupa na MJ 30?

 1. Predator says:

  Kwa muda mrefu miziki ya Congo imemilikiwa sana na wanaume hadi kukawa na pengo kubwa sana kati ya Generation Mbilia-Tshala na wanamuziki chipukizi kina dada wa sasa. Najua hapo awali kulikuwa na akina Yondo, Skola Miel, Pierrette etc lakini hawakutia muhuri ya umaarufu ya kudumu. Wanadada Congo wamejulikania tu kudance pekee lakini hakujatokea talanta ya kutushawishi kwamba akina dada wapo kiwanjani sawia na wanaume. MJ ni talanta mpya lakini kwangu mimi bado hashiki, bado nangoja kumuona mwanadada Congo atakayecheza kwenye ligi ya generation Mbilia-Tshala

 2. Hadj Le Jbnique says:

  mwanadada anajitahidi sana lakini aliwaudhi sana watu baada ya kukaa uchi kwenye show huko uganda walipokwenda kutumbuiza yeye na mama mokonzi tshala muana kwa mwaliko wa balozi wa congo nchini uganda,hali ilikua mbaya sana

  gonga hapa kama una kifua uone balaa la mej 30,ambae wamesoma na kuanza muziki mtaani pamoja na yule Cindy wa Koffi Olomide,otherwise kama huna kifua pita zako

  http://afriqueredaction.over-blog.com/article-36646744.html

 3. mamaa prezident says:

  meje alijidhalilisha na kumzalilisha mwanamke wa kiafrika,nampendaga lakini kwa hili nimemtapika!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: