Wafanyabiashara waaswa kutumia Barcodes kuongeza wigo wa soko.

Wafanyakazi wa GS1 (TZ) National Limited wakiwapungua wadau mikono wakati wa Mkutano mkuu wa Wadau, L to R Fatma Kange (CEO), Andrew Karumuna (BArcode Executive), Pius Mikongoti (Barcode Executive) Clementine (Membership Office), Mabamba Maregesi (Barcode Executive), Judith (Accountant).

Wafanyabiashara na wajasiliamali waTanzaniawametakiwa kutumia Barcodes za Tanzaniakwa ajili ya kutanua wigo wa biashara zao kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kujiongezea masoko na faida zaidi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo alisema kuwa watanzania tumeachwa nyuma sana ukilinganisha na wenzetu wan chi jirani kama Kenya ambao wamechangamkia sana masoko ya kimataifa ukilinganisha na makampuni ya Tanzania, moja ya vigezo vya kufanya biashara kimataifa ni kuwa na Barcodes ambazo zinaweza kukutambulisha kitaifa na kimataifa.

Mpaka sasa jumla ya makampuni 98 yamepatiwa nambari za mistari yaani Barcodes kwa ajili ya kutumia kwenye bidhaa zao. Makampuni hayo ambayo yanafanya idadi ya bidhaa 1450 ambazo ziko sokoni mpaka sasa zinazotumia huduma za Barcodes za kampuni ya GS1 (TZ) National Limited.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuuu wa mwaka wa wadau uliofanyika katika hotel ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Elibarik Mmari alisema japokuwa GS1 inamuda mfupi tangu imeanza shughuli zake nchini Tanzania ikiwa na miezi mitano tu tangu ianze shughuli zake bado changamoto ni nyingi wanakutana nazo ikiwa ni pamoja na watanzania kutotambua umuhimu wa Barcode, “Bado teknolojia ya Barcode ni ngeni kwetu, watanzania wengi hawajatambua umuhimu wake kwenye biashara, hii ni changamoto kubwa kwetu kutoa elimu zaidi kwa umma” alisema Bw. Mmari.

Pia Bw. Mmari aliyataka makampuni makubwa ambayo yanatumia Barcodes za nje kubadilika na kujivunia utanzania kwani kwa kufanya hivyo wanakuza ya takwimu za kibiashara za mataifa hayo na Tanzania kuonekana haifanyi vizuri kwenye sekta ya Biashara kimataifa kwani mengi ya makampuni ambayo yana export bidhaa nje yanatumia Barcodes ama za Kenya au Afrika ya Kusini.

Aidha akitoa salamu zake mgeni rasmi katika mkutano huo Mh. Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara alisema kuwa, Serikali imefarijika sana kuona GS1 imefikia hapo ilipo ingawa inafanya kazi zake katika mazingira magumu Serikali kupitia wizara yake itaisaidia kwa kadiri inavyoweza, vile vile Bi Mapunjo alisema kuwa kuna umuhimu wa taasisi hizi zinazotoa huduma kwa wafanyabiashara ikiwemo TBS, SIDO, GS1, BRELA na TFDA wakawa na mkakati wa kufanya kazi pamoja ili kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanarahisisha mazingira ya wafanyabiashara kufanya biashara na kuongeza soko si tu kwa faida ya wafanyabiashara bali kwa nchi kwa ujumla.

Wakati huo huo GS1 wamezindua tovuti yao inayopatikana kwa anuani hii www.gs1tz.org, akiongea kabla ya uzinduzi huo mtaalamu wa mifumo ya habari na mawasiliano na mifumo ya Barcode Bw. Pius Mikongoti alisema tovuti ya GS1 imezingatia kuwaarahisishia mawasiliano na upatikanaji wa fomu kwa ajili ya wanachama wao, kwani mfanyabiashara anaweza akaingia kwenye tovuti hiyo na kuongea moja kwa moja na ofisi aliyeko zamu kama anaswali lolote, vile vile tovuti hiyo inaweza kubadilishwa katika lugha mbali mbali kama Kiingereza, Kispaniola, Kifaransa, Kiarabu, Kihindi nk, kutegemea na mtu na matakwa yake.

MC wa Mkutano huo Bw. Kibonde kiongea na wadau.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo akiongea na jumuiya ya Wafanya Biashara na wadau wa GS1 *TZ( National Ltd katika mkuwano wa wadau jana.

Mgeni wa Heshima Bi. Joyce Mpunjo akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Yakub Hasham.

Meza kuu ikiwa imeongozwa na Mgeni rasmi Bi Mapunjo Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara.

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw Mmari akiongea na wadau wakati wa Semina hiyo. Katikati ni Mr Nanyaro wa TIRDO akifuat

CEO wa GS1 Bi Fatma Kange akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo.

Mfanya biashara Dr. Mghimba wa BK Tea ya Bukoba akitoa ushuhuda jinsi Barcode zilivyoweza kumsaidia kwenye masoko.

Mmoja wa wafanyabiashara ambaye alikuwa akitumia Barcode za Kenyana sasa anatumia Barcode za Tanzania Ndugu Mlako, yeye anazalisha Ice Cubes.

Mama Ndula wa Ndula Products akipokea cheti maalumu toka kwa mgeni rasmi.

Wadau wa GS1 Wakiwa Mkutanoni.

Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF Mama Esther Mkwizu akizungumza katika mkutano huo.

Toka Kushoto Mwenyekiti wa Bodi wa GS1 Bw. Mmari, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo, Mwenyekiti Bodi ya TPSF Bi, Esther Mkwizu na Mkurugenzi mkuu wa Tirdo Bw. Nanyaro

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja.

Bi Esther Mkwizu akizindua Tovuti ya GS1 http://www.gs1tz.org

Advertisements

One Response to Wafanyabiashara waaswa kutumia Barcodes kuongeza wigo wa soko.

  1. Surkus says:

    Very efficiently written article. Thank you.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: