Mdau anauliza, Papy Kakol na Titina Alcapone nani zaidi?

Kaka kati ya Papy Kakol na Titina Alcapone nani mkali maana mimi naona kma kakol akifanya recording anakuwa hatishi sana kama live na Titina katika live hajamfikia kakol na tofauti nyingine ni kwamba titina anatumia all pieces za drumset wakati Kakol mostly anapiga snare zaidi hebu nisaidieni jamani.
Othuman Rolenza
Advertisements

11 Responses to Mdau anauliza, Papy Kakol na Titina Alcapone nani zaidi?

 1. Farid from Muscat says:

  Bila wasiwasi Titina Alcapone ndio mkongwe na best katika drums na yeye ndie anaeongoza band nzima yaani wapigaji na wachezaji ,sitaki kukutajia mengi inakutosha tu nyimbo ya ndombolo ya solo sikia anavyoungurumisha halafu nenda katika live show zake utajob100.

 2. Philipo Haule says:

  Kakol hamfikii Titinaa hata akae miaka 100

 3. BABA MARTHA says:

  Naomba nianzishe ubishi, Mimi ni Mnazi wa Wenge Musica BcBg, namkubali sana Titina Alcapone, lakini Sebondo ya Mashine(Papy Kakol) ukisikiliza drums za Titina ni kama nyepesi sana, nafikiri alikuja kubadilika alipokwenda kwa Koffi. Lakini kila mtu ana mapenzi yake kwa upande wangu Papy Kakoli zaidi ya Titina, Kakol na Champion Mwanza na mimi nauliza nani zaidi.

 4. Predator says:

  Saa zingine huwa nashangazwa namna watu wanareason, km. wanaweka ukongwe mbele ya utendakazi. Titina kumtangulia Kakol kwenye jukwaa huu haimanishi hapitiki na hashindwi. Sababu ziliwafanya WMMM kushinda tuzo nyingi Africa (Kora et…al) ni team performance, classic African drums za Pappy Kakol zikinukuliwa pakubwa. Tuwe objective saa zingine.

 5. Hadj Le Jbnique says:

  mi naona wote wakali sema titina anweza kumzidi dogo kutokana na experience tu na zaidi titina anafanya mambo mengi hususan kwenye music arrangement,ukimuacha makaba titina kwenye arrangement yuko juu na siku hizi anaimba pia..

 6. Baraka says:

  Titina yuko juu sana na kitendo cha Koffi kumchukua Wenge BCBG ya Mpiana kilizidisha uhasama. Kama wengine walivyoeleza Titina baada ya kuonoka kwa JB Mpiana alikuwa nguzo kuu ya Quarter Latin kitu ambacho ni tofauti kwa wanamuziki wengi ambao huweza kupata umaarufu kutoka bendi moja na umaarufu huo kufa akihamia bendi ingine. Hakuna kundi litakalokuja kutokea kutingisha kwenye anga za Sebene kama Wenge Musica BCBG .Ukiacha Zaiko Langa langa na TP OK JAZZ ya Grand Maitre Luambo Luanzo.

 7. peter says:

  another addition..AWILO LONGOMBA….SEGUIN MIGNON

 8. Stivin says:

  Papy Kakol Mobali ya Linda Mundele ni noma! Titina ilikuwa zamani!

 9. BABA MARTHA says:

  Titina ni mpigaji mzuri wa Drums, na alikuja kubadilika alipokwenda Q. Latin, lakini Pappy Kakol, yupo hivyo tangu mwanzo, na ukitaka kujua angalia live concert zao. Tukizungumzia Sebene labda tuelekezane Sebene la namna gani.
  Uwezi kuniambia Wenge Musica BcBg wanapiga Sebene zaidi ya Koffi(Q. Latin) au Werra Son(MM)
  Kwa mimi Awilo na Sequin, Awilo ni zaidi, kama mfuatialiaji mzuri wa huu muziki, Sequin alikuwa anapiga tumba alikuwa ana nafasi kufa kufaana, baada ya kutoka Titina ndiyo akapata nafasi.

 10. peter says:

  Uwezi kuniambia Wenge Musica BcBg wanapiga Sebene zaidi ya Koffi(Q. Latin) au Werra Son(MM)……………..!!!!!!!!!!!

 11. John mtemi says:

  Wakubwa achana kabisa na Kakol ni moto wakuotea mbali

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: