Filamu ya I hate my Birthday kuwaweka pamoja Ray na Aunt Ezekiel.

MSANII nyota wa filamu bongo, Aunty Ezekiel, amesema kuwa baada ya kufunga mwaka sasa anatarajia kufungua na kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘I hate my birthday’, ambayo amecheza na Vicent Kigosi ‘Ray‘, huku itarajia kuwa sokoni muda wowote.
Msanii huyo kuzugumzia ujio wake mpya, alisema kuwa mbali na filamu hiyo ya kufungua mwaka pia atakuwa katika mchakato wa kazi nyingine aliyoipa jina la ‘House girl and House boy’.
Msanii hiyo alisema mwaka huu anataka kutoka kivingine kwani mashabiki wake wanahitaji kuona utofauti, ingawa watu wengi wamezoea kumuona akicheza filamu za mapenzi pekee.
Alisema kuwa yeye ni msanii hivyo anauwezo wa kucheza aina yoyote ya filamu kwani, anaweza kuuva uhusika hata wa msichana wa ndani ambapo ndiyo kazi ambayo itaonesha uwezo wake.
‘I hate my birthday’, ‘Naichukia siku yangu ya kuzaliwa’ hiyo ni filamu ambayo itakuwa na matukio mengi kwani hata Ray pia anaichukia siku hiyo hivyo watu watarajie kunaona ubunifu mkubwa ndani ya filamu hiyo kwani mwaka jana umepita na huu ni mwaka mwingine,” alisema.
Ray naye alisema ujio wa filamu hiyo ni mwanzo wa kazi nyingine kwani wanataka kutoa kitu ambacho kitawafanya mashabiki wao waone ni kweli wameingia mwaka mpya huku wakiwa na mambo mpya.

3 Responses to Filamu ya I hate my Birthday kuwaweka pamoja Ray na Aunt Ezekiel.

  1. Anonymous says:

    Poa bwana,c 2naitaji kusoma vitu kama hv.co kila cku bifu bifu co issue.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: