Chandra ya Bana Ok

Wakati huo bado sijaanza kupenda miziki ya Kizaire wimbo huu ulianza kunibadilisha mawazo hasa nilipokuwa nikimsikiliza Kaka yangu mkubwa Mr. Edwin Mikongoti akiimba wimbo huu kila jamaa akiwa mchupa lazima aweze hii kanda (wakati huo ni kanda na santuri) basi nikatokea kuupenda sana.

Wimbo unaitwa Chandra uliimbwa na Ok Jaz (Bana Ok) enzi hizo wakiwa na akina MAdillu System pamoja na Josky Kiambukuta na wengineo ambao kwa pamoja walitengeneza kundi zima la OK Jaz ambalo kwa kiasi kikubwa lilizalisha magwiji wa muziki wa Congo tunaowaona leo hii.

Kaka Hadji Le Geebeeneeque na Papaa Julie We Stone Ilunga Presidaa Bana Congolee na Darisalama hebu tupeni kidogo kuhusi hawa jamaa.

Advertisements

4 Responses to Chandra ya Bana Ok

  1. Hadj Le Jbnique says:

    Hawa jamaa wanapiga muziki sio siri,mimi ninazo correction kali sana za nyimbo zao na huwa nazisikiliza sana.Ninachojua mimi Bana ok ilizaliwa baada ya wana familia wa marehemu franco kuanza kuwasumbua wanamuziki waliobaki na bendi ya TP OK JAZZ baada ya Franco kufariki kwa ugonjwa wa ukimwi!

    Jamaa walianza kudai Royalties na kiasi kikubwa cha pesa kutoka TP OK JAZZ ambayo iliendelea kutumbuiza hata baada ya mzee Franco kufariki.Ili kuwakwepa ndipo wana band wakaamua kuachana na jina la TP OK JAZZ badala yake wakasajili bendi yao wakiita BANA OK wakiwa na maana ya watoto wa OK JAZZ!Lakini ikumbukwe bendi hizi zilikua mbili,moja hii ya kina Madilu ilikua ni Bana OK ya Kinshasa na nyingine ilikua ni Bana OK ya Belgium ikiwa na makazi yake jijini Brussels!Hii ya kinshasa ya kina madilu ambae baadae alijitoa baada ya kusimamishwa kwa utovu wa nidhamu ilikua chini ya mzee SIMARO na ilianza rasmi 1994 na ndio iliendelea kufanya vizuri.Lakini baadae tena kukaja kuwa na bana ok kibao kila mtu akidai kuwa na haki ya jina hilo,ipo nyingine iliwahi kuwa LONDON ikiwa na kina Fan Fan Mosese na wenzake,Fan fan pia alishirikiana na Rondot Kasongo Kuianzisha Bana OK ya brussels na ku realese album 1993,lakini bahati mbaya kassongo akafariki 1994 huko huko brussels na ukawa mwisho wa Bana OK Brussels!

  2. Anonymous says:

    Hawa jamaa ni wajuzi ndugu yangu Piusi jaribu kututupia Mario, Mamou, Nakoma Mbanda na mama ya mobali na 12600 letters nina lyrics zake tuwape wadau.

  3. Its my good pleasure to visit your blog site and also to appreciate your fantastic posts here. I like it a lot. I can truly feel that you simply paid a great deal focus for all those articles or blog posts, as all of them make sense and are extremely useful.

  4. Incredibly great site and outstanding and articles.beneficial design, as share superior stuff with good thoughts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: