Daddet wimbo wa BCBG ambao hauchuji

Kuna nyimbo kwangu huwa haziishi hamu kusikiliza na hata kama utakuwa karibu yangu simu yangu ikiita wimbo huu ndio Ringtone yangu.

Binafsi yangu huwa nazipenda sana nyimbo za taratibu ambazo JB mpiana amekuwa akiimba kiukweli zinanoga sana. Wimbo huu unapatikana ndani ya Albamu ya Pentagone ambayo kwa kiasi kikubwa ilileta hofu kwa miamba ya muziki wa Congo wakati huo kwani vijana walikuwa wanakuja kwa kasi kubwa na kwenye albamu hii hakuna wimbo wa ambao utapeleka mbele, nyimbo zote zinasikilizika na zinachezeka.

JB Mpiana amekuwa rafiki mkubwa wa rais Denis Sasou Ngueso na inasemekana huu ni moja ya nyimbo ambazo Mheshimiwa alikuwa akizipenda sana kwani alifanikiwa kupiga kwenye Birthday kadhaa za mheshimiwa huyu.

Hii radha ambayo kiukweli tunaikosa sasa kwani mapenzi yetu kwao kama kundi yametufanya leo hii kugawanyikakiushabiki.

Sikiliza Solo la Alain Makaba, Sikiliza Patient Kusangira alivyofanya mambo Msikilize Vando Maso Didie Masela na Bass yake humu. utapenda.

Natamani sana siku moja nije niwaone wamekusanyika pamoja kama kundi na kupiga show moja yenye akili najua ipo siku hili litatimia tuu.

11 Responses to Daddet wimbo wa BCBG ambao hauchuji

 1. Hadj Le Jbnique says:

  yap!kaka nakubali kitu hiki ambacho jb alimtungia mtu wa watu PDG Daddet Mpoko,kilipendwa na watu wengi sana,Daddet Mpoko ni kipenzi cha wanamuziki wengi ndio maana mpaka leo ukizisikiliza nyimbo za bcbg na maison mere hilo jina utalisikia sana midomoni mwa jb na werra!

 2. Stivin says:

  Inaonekana unampenda sana JB, wimbo huo ni Utunzi wake Didier Masella!

  • Hadj Le Jbnique says:

   kweli kaka naona nilichanganya mambo kidogo,Daddet mpoko hii ni utunzi wake Le FOUNDEE masella….jb aliimba na kukitia nakshi tu.

 3. Stivin says:

  Huo wimbo umetungwa na Didier Masela, nyie Jbniques punguzenu kumuabudu Mpiana

 4. peter says:

  ukisikia JBnique maana yake nikwamba tangu tuko watoto wadogo darasa la kwanza miaka hiyo ya 80 ndani ya WENGE CLAN….hatukuanza ukubwani…..

  • Anonymous says:

   Muwe wakweli basi, tatizo lenu JBnique mnamuabudu mno JB Mpiana, toka Wenge, Wenge iliposambaratika yeye ndo alibaki na nguvu kubwa, amefanya nini cha maana toka wakati huo?

 5. peter says:

  …….OYO EZA OEUVRE(live fikin)…chamutu chamutu cha NZAMBE cha NZAMBE!!!!

 6. Farid From Muscat says:

  hata mimi naupenda sana mwimbo huu na mara ya kwanza kuona video yake ilikua 1997 pale nilipokwenda kutembea TZ na mpaka leo nikiusikia basi nakumbuka sana Africa

 7. Excellent post. I was checking continuously this weblog and I am inspired! Extremely useful info specially the remaining phase 🙂 I take care of such information much. I was seeking this certain info for a very long time. Thanks and best of luck.

 8. What I have generally told individuals is that when searching for a good online electronics retail store, there are a few aspects that you have to factor in. First and foremost, you need to make sure to find a reputable along with reliable shop that has enjoyed great critiques and ratings from other shoppers and business world analysts. This will make certain you are dealing with a well-known store to provide good service and aid to their patrons. Many thanks for sharing your thinking on this blog.

 9. Great write-up, I am regular visitor of one’s blog, maintain up the nice operate, and It’s going to be a regular visitor for a long time.

Leave a Reply to Ingin Ku Selalu Berkarya Cancel reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: