Koffi chante Kabila, Concert ya Koffi Kumpongeza Kabila

December 22, 2011

image

Baada ya kumpigia kampeni Rais Kabila mwanamuziki Koffi olomide anatarajiwa kupiga Concert kubwa ya aina yake kwa ajili ya kumpongeza Rais Kabila.

Koffi ambaye anajulikana kama mtu wa maelfu ya aidia (L’homme aux milles idées ) alishiriki kwa kiasi kikubwa wakati wa kampeni za Rais Kabila na sasa ameamua kukamilisha kwani Rais Kabila ameshinda na tayari ameapishwa kwenye uchaguzi uliokuwa na malalamiko toka kwa mpinzani wake wa siku nyingi Etiene Tshekedi ambaye kwa upande wake amejitangaza yeye ndio Rais wa Congo.

Koffi ambaye alitamba na kibao chake cha remix de Affaire d’Etat ambacho alikibadili kwa ajili ya kampeni amejizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wa kabila na kupunguza mashabiki kwa uapnde ya tshekedi, Koffi amekuwa muathirika wa kwanza wa kuchanganya muziki na siasa Kongo kwani kundi ambalo linampinga Rais Kabila limefanikiwa kuisambaza Albamu mpya kwa Koffi kwenye mtandao na kuwaacha watu wa download bure.

Kundi hilo linalojiita Les Combattants ambalo linajulikana hivi karibuni kwa kuziharibu kazi za wasanii wote waliomuunga mkono Rais Kabila akiwemo Werrason, Koffi na wengineo kama Tshala Muana na Mpiana.

Koffi anasema atafanya show hiyo kwa ajili ya kumpongeza Kabila na kuwashukuru mashabiki wake kwa Kumpa Kura Kabila.

Koffi ambaye anaachia albamu mpya hivi karibuni amemshirikisha mpenzi wake Cindy ambaye kwa hakika ameshiriki vyema na kuipamba albamu ya Abracadabra ambayo ina nyimbo 10. Koffi anaongoza kwa kutumia pesa nyingi kutengeneza video zake hivyo inategemewa video ya albamu hii itakuwa yenye ubora wa hali ya juu.


Daddet wimbo wa BCBG ambao hauchuji

December 22, 2011

Kuna nyimbo kwangu huwa haziishi hamu kusikiliza na hata kama utakuwa karibu yangu simu yangu ikiita wimbo huu ndio Ringtone yangu.

Binafsi yangu huwa nazipenda sana nyimbo za taratibu ambazo JB mpiana amekuwa akiimba kiukweli zinanoga sana. Wimbo huu unapatikana ndani ya Albamu ya Pentagone ambayo kwa kiasi kikubwa ilileta hofu kwa miamba ya muziki wa Congo wakati huo kwani vijana walikuwa wanakuja kwa kasi kubwa na kwenye albamu hii hakuna wimbo wa ambao utapeleka mbele, nyimbo zote zinasikilizika na zinachezeka.

JB Mpiana amekuwa rafiki mkubwa wa rais Denis Sasou Ngueso na inasemekana huu ni moja ya nyimbo ambazo Mheshimiwa alikuwa akizipenda sana kwani alifanikiwa kupiga kwenye Birthday kadhaa za mheshimiwa huyu.

Hii radha ambayo kiukweli tunaikosa sasa kwani mapenzi yetu kwao kama kundi yametufanya leo hii kugawanyikakiushabiki.

Sikiliza Solo la Alain Makaba, Sikiliza Patient Kusangira alivyofanya mambo Msikilize Vando Maso Didie Masela na Bass yake humu. utapenda.

Natamani sana siku moja nije niwaone wamekusanyika pamoja kama kundi na kupiga show moja yenye akili najua ipo siku hili litatimia tuu.


%d bloggers like this: