Werrason, JB Mpiana katika vita mpya.

image

image

Kitendo cha mahasimu wawili kupiga kwenye eneo moja kinafanya mahasimu hawa kuwa na wakati mgumu kwani kila mmoja anatakiwa awaelimishe hasa mashabiki wao kuvumiliana na si kuleteana fujo kutokana na kuwa na sh.

Werrason ametangaza kuachia Single yake inayojulikana kama « Honorable député ».

Kwa upande wake Werrason ametangaza ukumbi wa La salle Carlos ulioko Kinshasa kuwa ndio utakuwa ukumbi wake wa kujidai na kila jumapili atakuwa akipiga kwenye ukumbi huu ulioko complex Mwana Nteba

Mashabiki wa Wenge BCBG walikuwa wameshazoea kupata burudani kila jumapili kutoka kwa kipenzi chao JB Mpiana na bendi nzima ambapo wanafanya sho zao kila jumapili katika ukumbi wa “The Crystal” ambayo iko barabara ya 30Juin ambayo ni eneo moja na ambako Werrason atakuwa anapiga.

Inasemekana JB Mpiana amenunua ardhi jirani na hapo na ameanza ujenzi ambapo inasemekana anajenga studio pamoja na ukumbi wa kufanyia mazoezi na pia club. habari zinasema kuwa ujenzi umeshaanza kwa hiyo mashabiki watakuwa wameongezewa burudani zaidi.

Wachunguzi wa mambo wanasema Werrason amepunguza sana ziara zake za nje kutokana na mikwara aliyopewa na mahasimu wa kiasiasa wa Mh. Kabila ambao walikasirishwa na kitendo cha wanamuziki hawa kumfanyia kampeni Kabila.

Werrason kwa miaka zaidi ya mitatu amekuwa hana ukumbi maalumu wa kupiga hapa Kinshasa na hii itakuwa ni nafasi nzuri kuwarudisha kondoo walipotea.

Mashabiki wakitoa maoni wamesema kuwa inatakiwa kama ilivyo kwao wao wawaelimishe na mashabiki wao kuacha ugomvi kwani watakuwa wakipiga maeneo jirani na kwa siku moja.

Kazi kwenu mashabiki

2 Responses to Werrason, JB Mpiana katika vita mpya.

  1. Predator says:

    Saa zingine mimi hufurahia tu hivi vita.

  2. mays mangala says:

    jb mipana and werrason
    loooooooooove
    you

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: