Starehe Mita 1800 juu ya usawa wa Bahari

 

Sehemu ya Genting kama inavyoonekana jioni, taa zinazoonekana kwa mbali ni mji wa Kuala Lumpur unavyoonekana toka Milima ya Genting.

Mwaka 2009 Malaysia iliingiza watalii 24,540,656 kwa mujibu wa takwimu zao ukilinganisha na watalii 840,000 walioingia Tanzania na kuuingizia Tanzania $1.35 billion huku tukiwa na kila aina ya vivutio vya watalii hawa. Kumbuka hawana Serengeti, Hawana Ngorongoro, Hawana Udzungwa wala Mlima Kilimanjaro. Kilichopo ni kwamba vivutio vichache vilivyopo vimetangazwa ile mbaya na kupewa nafasi.

Kutokana na takwimu za Wizara na Bodi ya Utalii ya Malaysia, Asilimia zaidi ya 45% ni watalii wa ndani huku watumiaji wa hoteli kwa takwimu ni watalii wa ndani zaidi.

Hapa Panaitwa Genting Highland, Ni umbali wa Kilomita 50 toka Kuala Lumpur mjini kuelekea Genting Highland, sehemu ya milima nchini Malaysia, Eneo hili lina jumla ya vyumba vya Hotel elfu 15,000 ambavyo ni vingi ukilinganisha na vyumba vyote vya hoteli zenye hadhi kwa nchi yetu ya Tanzania. kwa kawaida Malaysia ni nchi ya joto kama ilivyo Dar Es Salaam lakini tofauti ni kuwa joto la malaysia ni 30c to 36c na Fukuto ila kuna mvua mwaka mzima, wastani wa mvua kunyesha ni kila baada ya siku 2 hadi tatu. Hii hufanya mji huu kuwa wa kijani mwaka mzima lakini huwezi amini kuna sehemu ya Malaysia jotoridi lake ni 12c to 20c na wakati wa baridi hasa kunadondoka barafu, Huku ndio kunaitwa Gentini umbali wa Mita 1800 toka usawa wa bahari.

Huku hasa ni mji wa mapumziko, naita mji kwani panajitosheleza kwa kila kitu kuanzia mahoteli hadi Hospitali ambapo watu hupendelea kwenda kupumzika na kupata starehe mbali mbali kama Cable Car ambazo zina urefu wa Kilomita tatu na nusu, na inapita katikati ya misitu minene ya Tropiki na ubaridi mwanana pia utaona ndege na wanyama kama nyani wakiruka kwenye miti huku ukipita kwenye kijikombe kilichobebwa na mkanda (cable) ambacho kina tembea mwendo wa wastani wa kilomita 10 kwa saa, ni burudani tosha ambayo inahitaji ujasiri kwani kama hujazoea utatamani kushuka.

Genting Highlands Malaysia

Safari ndio imeanza ndani ya “Cable Car”

 

Ndani ya Cable Car kule kwenye ukungu ndio tunakoelekea na ndio raha zote zilipo, kuzifikia sasa kasheshe.

Mara watu washafika

Siku yapili “vakesheni” inaendelea

Baadaye unafika Theme Park huku kuna michezo zaidi ya 60 ya kila aina ikiwa ni pamoja na Roller Coaster yenye urefu wa Kilometa moja, Train, Speed Car, Speed Boat, Mashua, Michezo ya Jukwaani, Maonyesho ya Wanyama mbali mbali, Muziki, Vyakula vya kila aina, utamaduni, Bustani ya Ndege, Bustani ya Mamba, Bustani ya Nyoka, kwa ujumla panakufanya ujione uko mahali tofauti.

Live Performances usiku ni sehemu ya starehe za Genting

Pia kuna ukumbi wa Concert mkubwa ambao una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 10,000 na ukumbi huu ni full kipupwe, ambapo wanamuziki maarufu wakija pia hutumbuiza huko.Usiku kuna burudani za aina mbali mbali ikianziwa na sarakasi toka kwa akina dada ambao nadhani hawana mifupa, ije ngoma na utamaduni wa Wamalay (kama taarab) hadi Vikundi vya Kizazi kipya na nyimbo za kimagharibi pia, Kwa ujumla ni raha yaani mpaka unaona unapewa zaidi kuliko gharama halisi.

 

Pia kuna uwanja wa Golf kwa wenye mchezo wao, ambao wengi ni wageni mahoteli zaidi ya 30 yaliyopo kwenye kijiji hiki cha maraha. Mbali na hiyo kuna Casino kubwa, hii ndio Licensed Casino kwa Malaysia na inakusanya wacheza kamali toka Singapore, Malaysia, Indonesia na Brunei ambao wote hufika kucheza kamali hapa.

Advertisements

One Response to Starehe Mita 1800 juu ya usawa wa Bahari

  1. I absolutely take pleasure in just about every very little little bit of it and I have you bookmarked to test out new things of your site a need to study site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: