Mazoezi ya BCBG – KIN

December 14, 2011

Leo tunaitembelea kambi ya Bcbg mazoezini,hapa tunawakuta wanakifanyia mazoezi kibao MBWA cha  kwake Chai Ngenge kipo ndani ya album ya Sayons serieux,kiukweli achenini Chai aitwe hivyo yuko juu sana kwa kweli!

 

Hapa Chai Ngenge anakwambia na kitu Duo De Paris,dogo mkali sema hana bahati ya kuwika!


Happy Birthday Fally Ipupa

December 14, 2011

Leo ni siku ya kuzaliwa mwanamuziki Fally Ipupa, Fally Ipupa ambaye wiki hii alizikonga nyoyo za watanzania kwa show kabambe anazidi kujizolea sifa kem kem kutokana na kujituma kwake jukwaani na jinsi alivyoweza kupangilia bendi yake.

Inasemekana mwanamuziki huyu alilipwa dola laki moja kwa ajili ya kupiga kwenye harusi ya Didie Drogba mapema mwaka huu akiwa na mwanamuziki J Martins, kutokana na nyota yake kung’ara Drogba alimualika mwanamuziki huyu akidhani ndiye mmiliki wa wimbo wa Jukpa Remix ambao Fally Ameshirikishwa na J Martins wa Nigeria.

Wimbo huu na nyinginezo zilizidi kumpandisha chart Fally ambaye kwa mwaka huu alikuwa na show nyingi kwa mwaka huu huku akiongoza kwa show hizo kwani si Africa Mashariki bali Afrika nzima na duniani kote.

Kutoka na Olivia na wimbo alioimba na Olivia uliongeza umaarufu wa Fally Ipupa na soko lake kwa nchi na mashabiki wanaozungumza Kiingereza, ingawa inasemwa uhusiano huo haupo tena lakini ni wazi ulipandisha soko la mwanamuziki huyu ambaye anaongoza pia kupendwa na akina dada.

Fallu amekuwa ni mwanamuziki mwenye mafanikio kati ya kizazi cha nne na cha tano cha muziki wa Congo ukilinganisha na wenzie ambao walichomoka kutoka kwa wanamuziki wanaotamba kama Werasson, Koffi, JB Mpiana na wengineo.

Aliwahi kuulizwa kama anajivunia nini kwenye bendi yake kiongozi wa kundi na muasisi wa Quartier Latin Koffi Charles olomide alisema Quartier Latin ni chuo cha muziki wale wanakwenda na kukaa pale wakitoka wanakuwa ni wanamuziki hodari. awali akijiunga na Koffi Olomide Fally alikuwa akicheza zaidi show na ndipo Koffi alipogundua kipaji chake na kumuongoza kuitumia sauti yake, kadhalika Fally Mwenyewe hajawahi kumsema vibaya na anamshukuru Koffi kwa kumfikisha hapo alipo.

Katika wimbo wake wa Liputa Fally alimuimbia mwanadada Tabou Fatou Top Modelle ambaye anaishi huko Belgium, mwanadada huyu ambaye anamiliki Boutique kadhaa kwa muda mrefu ndiye anayejitolea kumvalisha Fally Ipupa ambaye mwenyewe anakiri kuwa kuvaa kunammalizia sana pesa. Nilibahatika kukaa naye kwa takribani dakika kumi tu alipokuwa hapa nikiwa Airport Dar Es Salaam “ …. nikisafiri huwa nasafiri na nguo za kazi tu ila nikirudi huwa nabeba mabegi mengi kutegemea na fasheni ambayo iko, kuvaa kwangu ni ile ladha ninayoifikiria, napenda kuwa simple ila kwenye nguo za gharama na muonekano nadhifu” alisema Fally kwenye maongezi majuzi hapa Dar.

Pia aliongeza kuwa anavutiwa sana na Dar es Salaam kwani kuna mabinti warembo wanaojua kuvaa na wachangamfu na wakarimu sana, anasema anapenda sana kuwaona mabinti “wako kama maua, usilichume ua, unaliangalia unalinusa ukilichuma litakauka mikononi mwako” aliongeza Fally kupitia kwa mkalimani wake. Kingine alisema chakula kinamvutia sana kwani kuna variety nyingi ya chakula cha kiafrika kilichonogeshwa na kuongezwa ubora, akitolea mfano anasema ukila fufu na samaki waliochemshwa ni tofauti na fufu ya tanzania (ugali mweupe) na samaki wa nazi, aliongeza Fally.

Happy Birthday Mukulu.


%d bloggers like this: