Mkasi wa Salama Jabri

December 12, 2011

Kipindi cha Mkasi cha Salama Jabri tayari kimeanza kuruka angalia na usikilize hapa jinsi Bi Dada huyu anavyoweza kumudu mahojiano.


Msikilize Aimelia hapa.

December 12, 2011

Anaitwa Aimelia Liase Doming’ong’o ambaye aliwahi kutamba sana akiwa na Wenge Musica kwa sauti yake tamu na kali, huyu bwana anasemwa ndio bingwa wa pitch kwamba anaweza kuivuta sauti yake hivi eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh hata kwa sekunde 20 kama unabisha sikiliza Live ya Bercy utaniambia.

Jamaa aliondoka Wenge lakini bahati ni kuwa pengo lake na kila walipoimba nyimbo zake JB Mpiana aliimba sauti ya Aimelia na kuipatia vilivyo. Aimelia aliondoka Wenge BCBG na kujiunga na Werasson kabla hajaamua kutoka kivyake, Kama ulipitwa Aimelia aliondokaje Wenge BCBG gonga hapa. Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne


le Combattants waisambaza Album ya Koffi kila mahali kabla haijatoka

December 12, 2011

Kundi la Wanaharakati wa Congo linaloishi Ufaransa, Belgium na Canada wameisambaza kwenye mtandao albamu nzima ya mwanamuziki Koffi Olomide ili watu waweze ku dopwnload bila malipo.

Albamu hiyo ya Koffi aliyoiita ABRACADABRA ilikuwa ndio itoke wakati wowote kuanzia sasa, lakini kwa mshangao haijulikani jamaa ameipataje alikaririwa akisema Olomide kwa masikitiko baada ya kupiga kura wiki iliyopita.

Koffi ni mmoja wa wanamuziki waliokuwa wakimuunga na kumfanyia kampeni Rais Laurent Kabila ambaye ametangazwa mshindi kwa asilimia 48%.

Albamu hiyo Koffi amemshirikisha Cindy na waliosikiliza wanasema ni nzuri sana. Koffi anajulikana kwa kutumia gharama nyingi kutengeneza albamu zake na zinakuwa katika ubora wa hali ya juu sana.


Werasson anaendelea vizuri

December 12, 2011

image

Kwa mujibu wa msaidizi aliyeongozana na Werrason anasema kuwa Mwanamuziki Werrason Ngiama Makanda anaendelea vizuri licha ya maumivu makali aliyokuwa akilalamika siku mbili zilizopita.

Werrason ambaye alikimbizwa India kwa matatibabu alipokelewa na mara moja kuanza matibabu ambayo ilibidi madaktari wakae naye zaidi ya masaa mawili kwa ajili ya kuurudishia mkono wake ambao unasemekana umeumia sana kwa ndani.

Aidha habari ambazo zinasemekana kuenezwa na kundi linalojiita Le Combattants ambalo linapiga vita wale wote wanaomsupport raisi Kabila wanasema kuwa Werrason hiyo ni janja yake ili akimbie nchi kutokana na machafuko ambayo yalifikiriwa kutokea baada ya uchaguzi.

Werrason ni mmoja wa wanamuziki waliokuwa wakimsupport Rais Kabila yeye pamoja na Koffi na wanamuziki wengine kama Didie Lacoste ambao kwa sasa wanapata taabu kwa CD na DVD zao kuharibiwa sokoni huku show za wanamuziki hao zimefutwa kabisa.

Wanamuziki kama Ferre Gola, Flamme Kapaya, Celeo Scam, Fally Ipupa, Felix Wazekwa na kidooogo JB Mpiana wamekuwa kwenye wakati mzuri kwa kusoma amala za nyakati kwa kutofungamana na upande wowote na wao show zao na CD zao zinapeta tuu huko Ufaransa na Belgium ambako ni maskani ya Ma diaspora wengi wa Congo kutokana na nchi hizo kuongea Kifaransa ambayo ni Lugha ya pili ya Congo.


%d bloggers like this: