WENGE,KIGALI,RWANDA.

WENGE MUSICA ORIGINAL NDANI YA KIGALI RWANDA

Na Hadj Le Jbnique,Boston,USA.

Huu ni wimbo “voyage” utunzi wake Le Big Tata Mobitch Adolphe Dominguez ambao video yake hii wenge waliifanyia jijini Kigali, nchini Rwanda kwa mzee Paul Kagame siku hizi, enzi hizo Rais wa Rwanda alikua Juvenal Habyarimana ambae Mobutu alikua akimtambulisha kama ni mdogo wake na hata alipouwawa kwenye ajali ya ndege akitokea Dar mwili wake inasemekana Intrahamwe walikimbia nao na kuupeleka Congo kwa maelekezo ya Mobutu kwenda kuuzika huko,hii inaonyesha jinsi gani Kinshasa na Kigali zilivyokuwa na mahusiano mazuri enzi za Mobutu na Habyarimana, uhusiano ambao ulikuja kulegalega sana baada ya Mzee Laurent Kabila kuingia madarakani Congo kinshasa huku Kagame akiingia madarakani Rwanda Kigali, Pia nchi hii ya Rwanda inasemekana ndio nchi ya asili ya Werrason na werrason amekuwa na wapenzi wengi sana huko kutokana na wapenzi wa muziki wa huko Kigali ku feel connection na werrason kutokana na muonekano wake ambao unafanana na watu wa huko kwa maana ya watutsi,japo werrason mwenyewe mara kadha amekua akikana kuwa na uhusiano wowote na Rwanda na amekuwa akisisitiza yeye ni mtoto wa Congo!

kwenye video hii naomba mumtazame Ficare Mwamba gitaa lake alivyokuwa enzi hizo na alivyo sasa,pia mtazameni Roberto Ekokota ndani ya sweeming pool sebene linapoanza kuchanganya anavocheza hiyo style yake maarufu ndani ya maji,wadau kiukweli mtanisamehe mi wenge naipenda sana….nikiangalia video za dizaini hii huwa najisikia raha lakini pia uchungu sana!

11 Responses to WENGE,KIGALI,RWANDA.

 1. Farid From Muscat says:

  bonini yekosalase boyee ….voyaage …yekotika mutu na sousii voyaage.
  Naam hizi zilikua ni golden days of wenge musica b.c.b.g 4×4

 2. PAPA NELSON NA MAKAMBAKO, IRINGA says:

  le jbnique unatisha….hii video wala sikujua kama iliwahi kurekodiwa,jamaa walikua wanapendana sana inavyoonekana!sijui mdudu gani mbaya aliwaingia

 3. Didistone says:

  kumbe boda boda zilianza kitambo pande hizo,naona wazee ndani ya boda boda in kigali….safi sana mkubwa jbnique,nice stuff kaka!

 4. Anonymous says:

  Hivi wadau kwanini nyimbo nyingi za wenge enzi hizo jb ndio amekuwa akitawala jukwaa kwa kuimba sehemu kubwa ya wimbo mzima hata kama hajatunga yeye???ina maana watunzi wa nyimbo wote walikua wanaona nyimbo zao asipoimba hazitanoga au???maana wimbo huu mi siku zote nilikuaga najua labda alitunga jb kwa jinsi alivyoubeba na sauti yake,leo ndio nimejua kumbe ni wa dominguez kumbe…

  • Stivin says:

   JB ana sauti nzuri na ya kuongoza, hata hapa nyumbani zamani Bichuka alikuwa anaimba nyimbo nyingi japo hajatunga yeye, hata enzi ya vijana Jazz nyimbo nyingi nzuri alitunga Adam Bakari lakini aliimba Eddy sheggy.

 5. peter says:

  BIG REMERCIMENT a …MUKULU Hadj Le Jbnique,…!!!sipati picha kama ungekuwa studio za hapa kwetu bongo!!halafu ukatumwagia vitu kama hivi….huku ni ukame tupu…kifupi hatuna Djs wenye kuilewa Lugha hiii tunayoitaka!!!again Big remerciment Mukulu

 6. mkemimi says:

  voyage mboso i luv this song kiukweli,asanteni sana kwa kumbukumbu kina kaka!

 7. mwanakombo,tanga says:

  wenge walitisha jamani…..huu wimbo wawezadhani umetoka wiki iliypopita kumbe ni miaka ishirini iliyopita karibu,yani kila nikiwasha computer ktoka juzi kitu kwanza nauplay huu wimbo ndio mengine yanafuata

 8. Anonymous says:

  jb anatisha sio siri alikua anaibeba bendi tukubaliane tu wajameni,hapa ukisikliza sauti yake ndio iliongoza wimbo mzuri na kuutendea haki

 9. Anonymous says:

  Hakuna kama wenge dunia muzima na haitotokea tena,kama ilivyokua kwa michael jackson alikuwepo mmoja tu na hatotokea mwingine tena anaemkaribia angalau!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: