Ya Mheshimiwa Mr II na Ruge yanaongeleka

rugesugu

Mwaka jana June 30, 2010 niliandika makala yangu nikisema Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.  Mpaka leo ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili na siku kama mbili tangu makala yangu. Makala ile niliandika ikiwa ni baada ya kutokea sintofahamu ambayo ilipelekea Mheshimiwa Mbilinyi kuwekwa ndani kwa kile kilichodaiwa kusambaza CD ambayo ilikuwa ikimkshifu Bwana Ruge.

“Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi wenye utashi na mtaguso tofauti tofauti, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani kwako linawezekana na kufikiwa muafaka.”

Katika makala ile nilijaribu kuwakumbusha wote wawili wajibu wao kwa jamii ikiwa Mheshimiwa Mbilinyi Kama msanii ambaye jamii inamuangalia yeye kwa ulimwengu wa sasa vijana wengi wanakuwa wakiwafatilisha wasanii na kwa upande mwingine kwa Ruge ama yeye binafsi au kama taasisi ana mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya vijana kutokana na ukweli kwamba yupo kwenye chombo ambacho anawagusa vijana wengi sana na kirahisi zaidi.

Kwa sasa Mheshimiwa Mbilinyi si msanii tu bali ni sehemu ya chombo muhimu ambacho kinatunga sheria kwa nchi, Bunge ni taasisi nyeti na kubwa yenye heshima kubwa, kwa safari ya Mheshimiwa Mbilinyi hakika haya ni mafanikio makubwa si tu kwake bali inaonyesha nguvu ya Sanaa nzima ya muziki kwa mara ya kwanza imetoa Mbunge.

Sitaki kuongelea chanzo cha mgogoro wao hapa kama unataka kujua basi bofya hapa

Katika makala yangu ile nilijaribu kuelezea ikiwa tofauti hizi zikiachiwa nini kinaweza kuwa madhara si tu kwa wahusika bali hata kwa sekta nzima ya burudani. majuzi tulishuhudia tamko naweza sema zito toka kwa Mheshimiwa Mbilinyi akisema kwa msisitizo kuwa Mkoa wa Mbeya hawataki tamasha la FIESTA ambalo linaandaliwa na kuratibiwa na Prime Time promotion na Clouds Media Group. Bado ukiangalia hapo chanzo ni zile zile tofauti ambazo wadau wa burudani tunazijua. Tofauti ambazo zinahitaji kuongelewa ili kuzimaliza nachelea kusema hilo linawezekana kwani hata biff zao zikiendelea hakuna kinachoweza kubadilisha kilichoshatokea.

Tofauti hizi ni hatari hasa kwa sekta ya burudani na wasanii kiujumla kwani kunakuwa na mgawanyiko na kuwatia uwoga wasanii wale ambao wanahisi wangetaka kumshirikisha Sugu kwa namna yeyote iwe kikazi au kimawazo kwani kufanya hivyo ni hatari kwa kazi zao kisanii ama kwa kuogopa kuingia kwenye malumbano au kwa nyimbo zao kutopigwa redioni au kwenye TV Stesheni kabisa. Ni wazi kuwa hakuna kituo cha redio kinachomilikiwa na Clouds Media Group kinaweza kucheza wimbo wowote wa Mheshimiwa Mbilinyi kwa sasa, hapo ndipo tulipofikia na huo ni ukweli usiopingika.

Kwenye makala yangu nilionyesha wasiwasi mkubwa nilisema hizi tofauti zenu hazitoishia hapo tuu mtazipeleka au zitawapeleka mbali, Majuzi tumeshuhudia malumbano mengine na kwa wakati huu ikiwa katika chombo cha juu kabisa cha kutunga sheria pale Mheshimiwa Mbilinyi ambaye ni waziri kivuli wa Vijana na Michezo alipokuwa akichangia hotuba ya Mheshimiwa waziri Nchimbi kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ilikuwa ni muendelezo wa tofauti zile zile ambazo niliziandika hapo awali.

Ingawa mchango wa Bwana Mbilinyi ulilenga kuwatetea maslahi ya wanamuziki lakini kwa upande mwingine ilikuwa ni shutuma za moja kwa moja kwa Bwana Ruge na Taasisi ambazo zinahusiana na yeye ama moja kwa moja au kikazi.

Pamoja na kuwa Mheshimiwa Mbilinyi alikuwa anatetea maslahi ya wanamuziki serikalini, mwisho wa siku Serikali inatengeneza platform kwa taasisi binafsi kama hizo za Prime time Promotion na ukiangalia ndio zinazotoa ajira kwa wasanii hawa. Tangu tamko la juzi la Sugu Bungeni hakuna msanii yeyote aliyediriki kumuunga mkono hadhani, kwenye gazeti, radio au hata mitandao jamii !! JE unadhani hakuna ambao wanakubaliana na Sugu kwenye hili? Jibu ni kuwa wapo lakini wanajua madhara ya kuonyesha kumuunga mkono Mbilinyi. Na ndio hasa kiini cha makala yangu hii najaribu kuangalia athari za mgogoro wa mafahari hawa wawili kwa sekta nzima ya burudani ikigusa vijana zaidi.

Kwani kwa sasa Muziki unaajiri vijana wengi zaidi jambo linalopelekea kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.

Sasa kwanini tufikie hapo? ni bora kuwakalisha hawa wawili na naamini kabisa Waziri husika anaouwezo wa kufanya hili kwani Waziri mwenyewe ni kijana na jambo hili linagusa wadau wake kwa kiasi kikubwa. kwani wengi wa waathirika kwa namna yeyote ile ama iwe upande wa Mheshimiwa Mbilinyi au upande wa Taasisi ambazo zinamhusu Ruge kibinafsi au kikazi waathirika bado ni vijana.

Baada ya pale Bwana Ruge alitoa Tamko ambalo kwa walipata kumsikiliza utakubaliana na mimi alionyesha kukerwa sana na kilichotokea na binafsi yake alivunja ukimya kwa kujibu shutuma zile moja baada ya nyingine.

Katika waraha huu wa Bwana Ruge aliongelea kukashifiwa kwa Clouds Media, THT na yeye binafsi na alitoa maelezo marefu ambayo mwisho wa siku si mimi na wala wewe msomaji unaweza kubadilisha mtazamo wa wawili hawa.

Mheshimiwa Waziri alipokuwa akijibu hoja za Bwana Mbilinyi alisema kwa utani Mheshimiwa Mr Sugu ni Sugu Kweli kweli kwani hoja hizi tulishazijibu zaidi ya mara moja na bado amezileta Bungeni. Kama alijibiwa na bado amezileta Bungeni basi ujue kuwa kuna ambacho haridhiki nacho ila ni kipi inawezekana kuna anachokijua zaidi.

Hakuna wa kumhukumu mwengine hapa ila mi nasisitiza tu tofauti hizi zisiwagawe wadau wa burudani, zisiwagawe wasanii kwani sekta ya burudani ndio pekee inayoweza kuondoa tofauti za kisiasa baina ya makundi ya vijana na zinawakutanisha vijana wengi zaidi we utashi na mtaguso mbalimbali, Waziri Mheshimiwa John Nchimbi chukua hatua kulimaliza hili na naimani linawezekana na kufikiwa muafaka.

Ni mtazamo tuu.

  

Advertisements

8 Responses to Ya Mheshimiwa Mr II na Ruge yanaongeleka

 1. Rufumbu says:

  Safi kaka,
  Nimependa the way ulivyoanalyse hii isue ni waandishi wa habari wachache sana wanaoweza kufanya hivi. Umeweza kueleza kwa undani Output, Outcome na impact katika vijana na sanaa kwa ujumla wake itakayotokana/ Inayotokana na ugomvi kati ya hawa jamaa wawili (Sugu Vs ruge).

  Binafsi mimi ni mpenzi sana wa Burudani na napenda sana maendeleo ya vijana katika sanaa. hili linaniumiza sana.

 2. Mdau UK says:

  Mkuu umeandika vizuri sana na nadhani wakiisoma na wao watakubaliana na wewe na ulichoandika hapa.
  Haya yanaongeleka na yanawezekana wasiwe wagumu wa mioyo.

 3. Anonymous says:

  well said my man……hongera kwako for this…tangu hii ishu ianze, sijaona a journalist ambae ameizungumzia in this angle kaka…..respect to you……

 4. Huu ndio uzuri wa KUCHAMBUA MATATIZO.
  Ulichofanya kaka ni KUTANABAISHA kwa kina kilichotokea na suluhisho wakati wengi wa “waandishi” wa habari wamekariri kilichosemwa. Kama nilivyowahi kusema, nyumbani tuna TAARIFA badala ya HABARI.
  Asante kwa hii, nami nitaiweka “barazani” mwangu ili wengine wapate kuisoma na kutafakari

 5. Thank you for every other excellent blog.I’ve a presentation next week, and I have found what I can add in my speech. Great job!

 6. Agnus Boles says:

  The moment I thought about matters like: why such data is for free here? Once you create a guide then at the least on promoting a book you will get a percentage, simply because. Thank you and superior luck on informing people far more about it.

 7. Hiroko Borom says:

  I undoubtedly appreciate every tiny little bit of it and I have you bookmarked to check out out new stuff of one’s web site a should study web site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: