Breaking News: Werasson apata ajali,avunjika mkono

image

 

Na Mabrook, Montreal Canada
Habari zilizotufikia punde zinasema wanamuziki wa WMMM wamepata ajali na inaripotiwa kuwa kiongozi wake Igwe Ngiama Makanda alias Werasson amevunjika mkono.

Kwa sasa habari hazijaeleza chanzo cha ajali ila habari zinasemakuwa Werrasson alikuwa akitokea mji alikozaliwa Wa Bandundu.

Aidha habari zaidi zinasema kuwa kiongozi wa Wenge BCBG JB Mpiana na Adolph Domibguez walikuwa kati ya watu wa kwanza kwenda kumfariji, habari zinasema JB Mpiana alikuwa wa kwanza kufika na alikwenda hospitali huku akibubujikwa na machozi kwani aliyempa taarifa alimwambia Werasson amefariki, “…Kwanza tulishangaa JB alipataje taarifa mapema vile… na alipofika alikuwa akitokwa machozi kwani aliyempatia taarifa alimueleza kuwa Werrason amefariki dunia” alisema Yanki Mpuyi ambaye alikuwepo wakati wa ajali.

Kisha waliwaacha wao wawili tu (JB na Werrason) humo chumbani hospitali kwa zaidi ya nusu saa wakiongea na kisha JB alitoka nje huku bado akibubujikwa machozi aliendelea kueleza Yanki na Heritier pamoja na Kakol ambao walikuwepo Hospitali muda wote, kisha waliingia Frere Patrice pamoja na mama yake mzazi ambaye alikuwa amehamaki na kumbusu mwanaye aliyekuwa akigugumia kwa maumivu makali.

Inasemekana kuwa mashabiki walifurika hospitalini na katishia kuichoma hospitali kama kipenzi chao atafariki ndipo Local Authority walipokaa na kuamua kuwa Werrason apelekwe nje ili kulinda usalama kwani ni kipindi cha uchaguzi hivyo mashabiki wangeweza kutumia nafasi hiyo kuleta fujo.

Kwa sasa Werrason amepelekwa India kupitia Afrika ya Kusini kwa matibsbu zaidi kwa ndege ya kukodi ya Ethiopian Air Line ambayo imelipiwa na Rais Joseph Kabila. Wengine walikwenda kumfariji ni pamoja na Didier Lacoste na Koffi Olomide. Kisha Werrasson ataenda USA ambako atakwenda kumsalimia mwanae Exocee ambaye yuko huko na mkewe na mwanaye mwingine Glady.

Ikumbukwe kuwa Werrason ni mmoja wa wanamuziki waliokuwa wakimkimkampenia Rais wa sasa Joseph Kabila.

Wananchi wa Congo jana walipiga kura kuchagua Rais na Wabunge ambapo wanamuziki kadhaa wameripotiwa kuomba baadhi ya nafasi.

Advertisements

14 Responses to Breaking News: Werasson apata ajali,avunjika mkono

 1. Salama says:

  Mukulu unanifurahisha sana Nimesikitika sana kupata habari hizi na jinsi ulivyokuwa una update hizi informations.
  Mungu akujalie nguvu Igwee

 2. Mfaume NP says:

  Pole Sana Werrason tuko pamoja nawe.
  Habari imejitosheleza mukulu uko juu.

 3. Hadj le Jbnique says:

  Poleni sana bana maison mere….mawerasonique dunia muzima nawapa pole,upinzani wetu uko kikazi za wasanii tunaowapenda zaidi lakini bado tuko wandugu!wote sisi ni kizazi cha wenge musica 4×4 tout terrain!

  Nawafariji kwa wimbo huu wa majonzi toka kwa koffi olomide na Cindy Le Coeur walipomuimbia mdau mkubwa wa muziki wacongo mamaa EDITA OMARI BONGO aka EDITA MWANA YA SASSOU,alipofariki,huyu mama amaesidia sana wanamuziki wa congo,alikua mke wa rais wa Gabon Marehem mzee Omari Bongo lakini pia alikua mtoto wa Rais wa congo brazza ville mzee Denis Sassou nguesso

 4. peter says:

  Mimi ni wenge CLAN pure kama JIBE MPIANA ametokwa na machozi sembuse mimi !!!!!! sina ubaguzi hata Kaka JIBE aliimba yuko chini ya ..papa wemba nk na hii anadhihirisha kwamba Ngiama…na Jibe MACHOZI YANAMTOKA….sasa kwanini sisi TUNAKUWA WABUGUZI…hata falsasa ya wenge CLAN hatuichimbi??TUKO PAMOJA NGIAMA MUNGU AKUJALIE UPONE!!! NA SPORT SRAREHE TUACHE UBAGUZI ……BABA DAIDA KATUONYESHA UKWELI KWAMBA …KAKA WERA NA MPIANA NI WENGE CLAN KAMA SISI…………lebig merciment …Le hadje jbnique, Kaka Farid , kaka Mukulu PIUS na mashabiki wote wa sport na STAREHE!!

  lekamanda pierre A town!!

 5. Anonymous says:

  Pole saana werrason na sisi wana wenge tuko na wewe jb mpiana ameonyesha kuwa hatuna biif tunakuombea utapona condoleance harindintwari theonest le jbenique

 6. Stivin says:

  JB mpiana na Werra ni wanamuziki wawili walioubadilisha muziki wa Afrika, pamoja na kutengana kumuziki lakini hawa jamaa ni ndugu. Kila mmoja amefika hapo alipo kwa sababu ya mwenzake, bana Wenge Tolinganaaa!

 7. Hadj le Jbnique says:

  OUT OF TOPIC:

  wadau mlioko bongo mbona hamtujuzi kinachoendelea?si nasikia fally ipupa yuko huko na leo ijumaa tarehe 2 dec atapiga bonge moja la show mlimani city?je show hiyo itavunja rekedi ya ile show maarufu ya fally in dar aliyowahi kupiga huko nyuma kwa mwaliko wa hao hao club E,Show ambayo VIDEO yake imekua ikinunuliwa kama njugu duniani kote mpaka kesho?ni suala la kusubiri na kuona!

 8. Anonymous says:

  Sidhani maana safari hii wamekosa publicity kabisa. Shuhuli ni watu na siyo members. Kila mtu anayekuja hapa lazima arudi. Lakini mara ya pili inakuwa siyo kivile. Hata Papa Pius hakupost humu kama jamaa anakuja.

 9. Hadj le Jbnique says:

  hata kipindi kile nadhani ilikua ni kwa memberz naona si ni jamaa hao hao wa club E ndio walimleta,na mwaka jana pia walimleta jb mpiana hapo bongo kwa style hiyo hiyo ya kimya kimya na kualika memberz wao tu,nilikua dar siku hiyo,japo sio member nili fight mpaka nikapata nafasi ya kuingia kwa kuwahonga wale walinzi ths 30,000 za kibongo,wengi walifika pale na kurudi home,mimi sikukubali

  • Hadj Le Jbnique says:

   YAP THANX FOR THAT KWELI NI DEC 2009 NILIJICHANGANYA,I WAS THERE,NAKUMBUKA NILIKUTANA MALOU STONCH PALE NJE NAE ALIKUJA HAKUWA NA TKT LAKINI ALIPOONA HAZIUZWI PALE MLANGONI AKAAMUA KUTIMKA MIMI NIKAMWAMBIA LAZIMA NITAINGIA TU SHOW KAMA HIZI NI VERY RARE,NA NILIINGIA KWELI KWA KUTUMIA MLANGO WALIOINGILIA WANAMUZIKI,WAKATI TSHALA MUANA NA WANAMUZIKI WAKE WANAINGIA NIKAUNGA TELA KAMA MMOJA WA WANA DELEGATION YAKE,LAKINI NILIKATA 30 CASH KWA BOUNCER!

 10. Anonymous says:

  Ni kweli haya maonesho yamekuwa mahsusi kwa wanachama wa club e lakini huwa kunakuwa na matangazo kidogo nani anakuja na lini event itafanyika na huwa wanauza tickets chache kwa mashabiki. lakini this time naona aidha wamefanya supriseili kuwaengua wale wanaopania lakini ndiyo ukweli wanaochangamsha shuhuli au hawakuwa na uhakika wa kuja wa huyo jamaa mpaka last minute.Lakini yote kwa yote si rahisi kufunika bovu kama first time. ila what i know last year walimleta Chack Khan , i think 2009 ndiyo ilikuwa Tshalla Mwana na JB Mpiana pale Ubungo Plaza.

 11. peter says:

  wadau …naomba kuuliza swali pale FIKIN namaanisha PRIMUS..JE NIMAKABURU KAMA HAWA CLUB E!! wananikumbusha nikiwa kuleeeee enzi za form one …jamaa siku nyeti za Disco walituzuia sana!! TUPELEKE KILIOCHETU TBL LABDA WATALETA SHOW KAMA ZILE ZA FIKIN…MTEJA KUGAWANA MAPATO NA MASHABIKI!!

 12. yohana says:

  Haya jamani werrason apata ajali, tumwombee

 13. kakole says:

  jan asa kori balo aso

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: