Clouds turudishieni Afrika Bambataa yetu

Wimbo huu ni utunzi wake Tshai Ngenge aka Bluetooth toka Wenge BCBG, Nyimbo hii ni kama zilivo nyingine ambazo kwa huku kwetu haikupata umaarufu kwa vile Radio Stations zilikuwa hazizichezi nyimbo za Wenge BCBG, kiukweli naikumbuka sana Afrika Bambataa ya akina OJ Njaidi, DJ Charls Mr C Charles Muhamiji, Agape Msumari hata Mamaa Sophie Kessy alijitahidi, tangia hapo kiukweli Clouds haijatutendea haki kabisa kwa kutokuwa na kipindi cha nyimbo za Bolingo badala yake wamewapa wengine vipindi vyao, kuna wakati i bet kipindi cha Bambataa kilikuwa na matangazo mengi hii ikiwa ni ishara moja kuwa kipindi si tu kinapendwa bali kunasikilizwa, na kipimo kingine ilikuwa ni idadi ya meseji ambazo zilikuwa zinasikika.

Kipindi cha Afrika Bambataa kilikuwa kikirushwa na redio maarifu ya Clouds ambayo kwa sasa inasikika duniani kote kwa kupitia mtandao (www.cloudsfm.co) hii inawafanya watanzania na wazungumza kiswahili duniani kote kupata fursa ya kusikiliza redio hii yenye ushawishi mkubwa hasa kwa vijana kutokana na mpangilio wa vipindi vyake ambavyo kwa kiasi kikubwa unagusa vijana na wapenda burudani wote (kasoro wa Bolingo).

Hakuna anayeibisha kuwa Clouds wanauwezo wa kufanya kisichokitu kuwa kitu kwa jinsi wanavyoweza kupigia debe, kama unataka shughuli yako hasa za burudani zifane washirikishe utaona balaa yake. tuyaache hayo hapa nipo kwa ajili ya suala moja la mashabiki wa muziki wa Kiafrica hasa Bolingo.

image

Mtangazaji Sophia Kessy akiwa na Mkurugenzi wa Clouds na mwanamuziki Koffi Olomide Studio za Clouds katika kipindi cha Afrika Bambataa, Kipindi hichi ndicho kilimtoa Sophia Kessy.

Tangu walipozindua mpangilio mpya wa vipindi ndipo kipindi cha Afrika Bambataa kikafa na mwisho wa kuwa na muda maalumu wa muziki huu ambao mi kwa kiasi kikubwa nachelea kusema unapendwa, maana muda wa kipindi cha Bambataa magari yote yanafungulia Clouds na hata Bar zote zinaweka Bambataa watu wanaburudika.

Binafsi namkumbuka Othman Njaidi na Mr C Charls Muhamiji hawa ndio walinibadili dini ya muziki na kuanza kuipenda miziki hii, Njaidi amerudi nchini na ana uwezo mkubwa wa kwenye muziki huu hata kama yuko na biashara zake afanye kama hobby walao mara moja kwa wiki na iwe ama ijumaa, au jumamosi ili walao tuburudike na sisi tuone mnatujali.

Bado Clouds wana madj wanapiga sana bolingo huwa nasikiliza Night Kali ya DJ Elly kama sikosei anajitahidi kupiga Bolingo lakini ili nisikilize inabidi nichukue zamu ya ulinzi shirikishi ili nisilale, Kiukweli Meneja wa Vipindi kwa hili inabidi mtusikilize na kututengea muda wetu nachelea kusema ni haki yetu kama Clouds ni redio ya Vijana na vijana wenyewe si nipamoja na sisi kwa nini burudani mtutenge? La hasha mtuambie kuna study ambayo mmefanya mkaona kuwa kipindi kile hakina wapenzi hilo nakataa kama mimi hapa tu mashabiki wangu wengi ni wa muziki huo je huko redioni?

Sisi tunaweza kuwaambia na kuwakilisha mawazo tu ya mashabiki wachache ni hiari yenu kuyafanyia kazi au kuyaacha lakini amini nawaambia kipindi cha Bambataa kilikuwa na wapenzi wengi kwani tupo wengi mashabiki wa muziki wa Kiafrika na si hivyo tu ingekuwa ni jambo jema kama redio zingekuwa zinapiga walao 60% ya muziki wa kiafrika ikiwemo 30% au hata 40% ya muziki wa nyumbani ili kukuza na muziki huu. Sikatai muziki wa kileo unapendwa lakini ndio muwape 95% ya air time jamani?

Sebastiani Maganga rafiki yangu wa kitaa (Sinza long time kitambo) tusikilize bana kama nilivyosema awali hii ni redio ya vijana na sisi ndio vijana wenyewe tunaitaka hiyo nafasi yetu. Naimani nyie ni wasikivu na hili mtalifanyia kazi, please chonde sie wadau mnatutenga.

11 Responses to Clouds turudishieni Afrika Bambataa yetu

 1. Juma Mohammed says:

  Lakini kwa kweli Clouds media you are fucking fake for real. Yaani hata hamsikilizi vilio vya wasikilizaji wenu? In TZ I can say over 80 percent ya Wa TZ si wapenzi wa fleva. People listen to fleva kwa sababu they are forced to listen to it, they have no choice. Chunguzeni when bendi zetu za asili (Msondo, Sikinde, Vijana, n.k) zikipigwa jinsi watu wanavyozishupalia. Mfano ulio hai, juzi tu hapa Twanga imefanya bonge la show kuzindua albam yao, si mliona ule umati uliojaa pale? Your presenters wako pale kwa ajili ya hela from fleva artists. Wanapewa kitu kidogo na hawa jamaa ili nyimbo zao zipigwe redioni, everybody knows that….it’s not a secret. Kwa nini msiwe fair, if you really wanna play fleva songs why not share that air time with muziki wetu wa asili si huu wa kuiga (fleva)? You guys really suck! Nilijaribu kusikiliza Clouds online hapa Marekani nimeacha kama wenzangu, maana kila mtu analalamika over the same thing that I have just mentioned. Completely useless!

 2. Hadj le Jbnique says:

  kaka kweli naungana nawewe,hebu mwenye namba au e mail ya bwana ndege aiweke hapa au anitumie mapenziclub@yahoo.com,mi nitazungumza nae,hata jos kusaga pia,kwani na yeye ni mpenzi wa lingala,nipeni e mail yake,tena kama wakikubali kukirudisha this time waweke mtu anae ujua na mwenye interest na muziki wa lingala,sio mtu mradi mtu tu,hajui nyimbo za kupiga anaishia kung’aninia nyimbo moja tu album nzima,sisi kama wadau tutasidia kupatikana mtu huyo pamoja na masuala ya kiufundi ya jinsi bambataa mpya iwe,itakua na segments mbalimbali ikiwemo taarifa mbalimbali za kinachoendelea kinshasa kwa wakati husika n.k.

 3. Farid from Muscat says:

  kweli kabisa tunaomba wahusika walishughulikie kwa makini swala hili maana wanatunyima uhondo hasa sisi tunaosokiliza clouds fm tukiwa nje ya tz.

 4. werrasonique forever says:

  sote kwa umoja wetu siku moja tuvamie ofisi za clouds tumuone director mwenyewe sio watangazaji watatuzingua wale

 5. Kapera Mwinyi says:

  Kaka Mohammed hapo juu umeongea ukweli kabisaa and big up for that. Binafsi sio kama nafagilia lingala songs bali hata nyimbo zetu yaani za bendi za kibongo ziko juu sana siku hizi. Why not give air time hizi bendi zetu? Cha kusikitisha, sikilizeni ma dj wao Clouds pamoja na presenters wao jinsi walivyo fake. Yaani mtu analazimisha kuongea english wakati its broken, sasa sijuwi wanapata faida gani. MTZ ni MTZ tu they will never be African American sasa wanaiga ili iweje wakati TZ asilimia 99.9 ya wabongo wanazungumza kiswahili, jamani si ujinga huu? Hivi hata wewe Jo Kusaga uoni haibu kweli vijana wako ndiyo wako hivyo? Sie wabongo tulio nje 90 % yetu tunataka kusikiliza miziki yetu ya asili (si fleva na fake hip hop), leteni bongo dansi, taarab, soukouss, n.k.

  • Farid From Muscat says:

   100% maneno yako sawa kabisa ……………….Sie wabongo tulio nje 90 % yetu tunataka kusikiliza miziki yetu ya asili (si fleva na fake hip hop), leteni bongo dansi, taarab, soukouss, n.k.

 6. Mfaume NP says:

  Kaka Pius namkubali Njaidi kwa vile alikuwa anakijua Kifaransa na kilingala jamaa ni machine kama yupo nchini wampe kipindi kwa siku moja walao kwa wiki.

 7. Njama UK says:

  Naipenda sana hii Blog kwa hilo tuu

 8. Sabina says:

  Mi niko India nimechoka na huo ubongo wenye fuleva Bolingo zina upigaji wake na story zake za kusisimua na ndio maana tunasoma hii blog zina uandishi wake Kaka Piua Liberko la Loi, Weeeeeeeeeeeeeee Kitoko mingi Papaaaa

  Mchizi wako Sabina
  Delhi – India

 9. Philipo Haule says:

  Usipomsikiliza msikilizaji wako utamsikiliza nani sasa? Nimecheka sana niliposoma hiki kipande “Binafsi namkumbuka Othman Njaidi na Mr C Charls Muhamiji hawa ndio walinibadili dini ya muziki na kuanza kuipenda miziki hii, Njaidi amerudi nchini na ana uwezo mkubwa wa kwenye muziki huu hata kama yuko na biashara zake afanye kama hobby walao mara moja kwa wiki na iwe ama ijumaa, au jumamosi ili walao tuburudike na sisi tuone mnatujali.” Mwisho wa Kunukuu

 10. many wonderful details and inspiration, both of which I need to have, because of give such a useful information and facts here.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: