Wapenzi wa yenu hii yenu

November 9, 2011

image

Advertisements

Buriani Heavy D

November 9, 2011

image

Mwanamuziki aliyewahi kutamba sana miaka ya 90 Heavy D amefariki dunia akiwa na miaka 44.

Heavy D anasemekana alizidiwa akiwa nyumbani kwake Bevery Hills na kukimbizwa hospitali kwa matibabu lakini alifariki akiwa chumba cha wagonjwa mahututi.

Heavy D ambaye jina lake halisi ni Dwight Arrington Myers inasemekana alipokuwa akikimbizwa hospital alikuwa tayari kwenye hali mbaya.

Mbali na hiyo Heavy D alimeshiri kwenye Sinema mpya ya Ben Stiller na Eddie Murphy inayoitwa “Tower Heist”  na pia alishiriki kwenye tamasha la BET Hip-Hop Awards in October.

Soma zaidi Hapa


JB Mpiana na Dady Wemba Shumbu Wembadio Papa Wemba

November 9, 2011

Kweli Papa wemba na Jb mpiana hawakukutana barabarani!!!msikie mwenyewe hapo chini, kuanzia dk 8:30 anavosema kuhusu yeye na jb!!!Hii ilikua live concert ya wenge na papa wemba ndani ya Paris,ukiipanda video nzima ya show hii uta enjoy zaidi,hapa tunakupa kionjo tu……!kama kawaida yetu.


Wachezashow wa BCBG balaa

November 9, 2011

 

pia sikiliza hii

Wakati wenge inaanza haikuwa na stage show wa kike baadaye kwenye Pentagone tunamkumbuka Nene Sukari aka Nenee Sugar mwanadada serious hivi alikuwa hacheki mnene ila anakatika balaa alikuwa akiongoza kundi la uchezaji kwa Wenge Musica, baadaye walipoparanganyika ndipo walipoongeza Stage Show baada ya Koffi ambaye alikuwa juu kipindi hicho kuongozwa na kundi la wadada na kwa Koffi ukimtaka moja ya masharti yake ni kusafiri na Amazonia Guards wake, kwa wasiojua Amazonia Guards walikuwa walinzi wa kike wa Gadaffi, sasa Koffi hawa huwa anasafiri nao ndege moja na hukaa nao hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano.

JB Mpiana naye anasemwa kuwa anawajali sana wacheza show wake na inasemekana budget ya saloon na mavazi vipodozi huwa ni jambo si la kushauriana limo kwenye budget, humu utawaona Virginie Bukasa , Winnie Mandela, Zambrotta, Kadie Show, Bibi Sucre, wapi Papaa Hadji le Becebegeeque, Muzee ya Mapenzi Club Pamoko mkuu


Clouds turudishieni Afrika Bambataa yetu

November 9, 2011

Wimbo huu ni utunzi wake Tshai Ngenge aka Bluetooth toka Wenge BCBG, Nyimbo hii ni kama zilivo nyingine ambazo kwa huku kwetu haikupata umaarufu kwa vile Radio Stations zilikuwa hazizichezi nyimbo za Wenge BCBG, kiukweli naikumbuka sana Afrika Bambataa ya akina OJ Njaidi, DJ Charls Mr C Charles Muhamiji, Agape Msumari hata Mamaa Sophie Kessy alijitahidi, tangia hapo kiukweli Clouds haijatutendea haki kabisa kwa kutokuwa na kipindi cha nyimbo za Bolingo badala yake wamewapa wengine vipindi vyao, kuna wakati i bet kipindi cha Bambataa kilikuwa na matangazo mengi hii ikiwa ni ishara moja kuwa kipindi si tu kinapendwa bali kunasikilizwa, na kipimo kingine ilikuwa ni idadi ya meseji ambazo zilikuwa zinasikika.

Kipindi cha Afrika Bambataa kilikuwa kikirushwa na redio maarifu ya Clouds ambayo kwa sasa inasikika duniani kote kwa kupitia mtandao (www.cloudsfm.co) hii inawafanya watanzania na wazungumza kiswahili duniani kote kupata fursa ya kusikiliza redio hii yenye ushawishi mkubwa hasa kwa vijana kutokana na mpangilio wa vipindi vyake ambavyo kwa kiasi kikubwa unagusa vijana na wapenda burudani wote (kasoro wa Bolingo).

Hakuna anayeibisha kuwa Clouds wanauwezo wa kufanya kisichokitu kuwa kitu kwa jinsi wanavyoweza kupigia debe, kama unataka shughuli yako hasa za burudani zifane washirikishe utaona balaa yake. tuyaache hayo hapa nipo kwa ajili ya suala moja la mashabiki wa muziki wa Kiafrica hasa Bolingo.

image

Mtangazaji Sophia Kessy akiwa na Mkurugenzi wa Clouds na mwanamuziki Koffi Olomide Studio za Clouds katika kipindi cha Afrika Bambataa, Kipindi hichi ndicho kilimtoa Sophia Kessy.

Tangu walipozindua mpangilio mpya wa vipindi ndipo kipindi cha Afrika Bambataa kikafa na mwisho wa kuwa na muda maalumu wa muziki huu ambao mi kwa kiasi kikubwa nachelea kusema unapendwa, maana muda wa kipindi cha Bambataa magari yote yanafungulia Clouds na hata Bar zote zinaweka Bambataa watu wanaburudika.

Binafsi namkumbuka Othman Njaidi na Mr C Charls Muhamiji hawa ndio walinibadili dini ya muziki na kuanza kuipenda miziki hii, Njaidi amerudi nchini na ana uwezo mkubwa wa kwenye muziki huu hata kama yuko na biashara zake afanye kama hobby walao mara moja kwa wiki na iwe ama ijumaa, au jumamosi ili walao tuburudike na sisi tuone mnatujali.

Bado Clouds wana madj wanapiga sana bolingo huwa nasikiliza Night Kali ya DJ Elly kama sikosei anajitahidi kupiga Bolingo lakini ili nisikilize inabidi nichukue zamu ya ulinzi shirikishi ili nisilale, Kiukweli Meneja wa Vipindi kwa hili inabidi mtusikilize na kututengea muda wetu nachelea kusema ni haki yetu kama Clouds ni redio ya Vijana na vijana wenyewe si nipamoja na sisi kwa nini burudani mtutenge? La hasha mtuambie kuna study ambayo mmefanya mkaona kuwa kipindi kile hakina wapenzi hilo nakataa kama mimi hapa tu mashabiki wangu wengi ni wa muziki huo je huko redioni?

Sisi tunaweza kuwaambia na kuwakilisha mawazo tu ya mashabiki wachache ni hiari yenu kuyafanyia kazi au kuyaacha lakini amini nawaambia kipindi cha Bambataa kilikuwa na wapenzi wengi kwani tupo wengi mashabiki wa muziki wa Kiafrika na si hivyo tu ingekuwa ni jambo jema kama redio zingekuwa zinapiga walao 60% ya muziki wa kiafrika ikiwemo 30% au hata 40% ya muziki wa nyumbani ili kukuza na muziki huu. Sikatai muziki wa kileo unapendwa lakini ndio muwape 95% ya air time jamani?

Sebastiani Maganga rafiki yangu wa kitaa (Sinza long time kitambo) tusikilize bana kama nilivyosema awali hii ni redio ya vijana na sisi ndio vijana wenyewe tunaitaka hiyo nafasi yetu. Naimani nyie ni wasikivu na hili mtalifanyia kazi, please chonde sie wadau mnatutenga.


Wazekwa mashine bwana

November 9, 2011

Papa Julie We Ston aka Baba B na kati ya Kigamboni huwa kila siku ananiambia kwa Congo huwezi kuzungumzia fourth Generation ya Muziki wa Congo bila kumtaja Fellix Wazekwa, huyu bwana kimtazamao unaweza kudhani ni kijana mdogo wa rika la akina JB Mpiana la hasha Wazekwa ni Le Grand bwana ni mtu mzima na ni kaka kwa Koffi nikiwa na maana ni mkubwa kwa Koffi na ndiye aliyemfunza Koffi akaiva na kufika hapo alipo.

Bado ni mbishi na ana show ambazo anajaza sana huko France na Belgium pia, ni vile tu redio zetu zinatabia ya kupiga musiki wa bendi tulizozizoea na hata kama wanapiga ni nyimbo moja au mbili pekee.

Hebu sikiliza wimbo huu kisha uniambie maoni yako. Siku njema wadau wangu, Papaa Sisco ndani ya Kwetu Saloon Kigamboni Kitokoooo mukulu, uko juuu!!!


%d bloggers like this: