Je wamfahamu sawa sawa Awilo Longomba alikotokea na alipofikia???

Na The Romantic

Kama wewe kweli ni mpenzi wa miziki ya bana congo jina Awilo Longomba litakua si geni sana masikioni mwako, Awilo Longomba ni mwanamuziki machachari kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya watoto wa congo ambaye mwanzo alianza muziki kama drummer boy akipiga drum kwenye bendi mbalimbali kama Viva la musica ya Mzee Papa Wemba “mwalimu”, Stukas, Nouvelle Generation ambayo alikua kiongozi wake na Loketo Group kazi ambayo alidumu nayo mpaka mwaka 1995 ambapo aliachana na drum na kujikita kwenye uimbaji na utunzi ambapo mwaka huo huo 1995 aliachana na La Nouvelle Génération na kutoka solo na album yake ya kwanza  “Moto Pamba” ambayo alitunga nyimbo zote,kuimba na pia kupiga drums.Baada ya mafanikio ya album hiyo aliamua kuachana rasmi kabisa na drums na badala yake akajikita kwenye kutunga na kuimba huku akipata mialiko katika nchi mbalimbali za ulaya na africa mashariki kenya na Tanzania hususan.

Hapa Awilo akiimba wimbo Ma’ze wa mzee Tabu Ley ambao hapa ameufanyia ukarabati na kuurekodi kisasa zaidi:

Ilikua ni solo album yake hiyo hiyo ya kwanza iliyompatia heshima ya Best Central Africa Artist Awards” kwenye KORA MUSIC AWARDS 1996 and 1997 (All Africa Music Awards, held in Sun City, South Africa).

Hapa Awilo anafanya balaa…anachombeza  na mambo ya “Lopelee” ya jb mpiana

Kutoka hapo hakuna aliyeweza kuuzima moto aliouwasha Awilo,akawa hakamatiki tena,ambapo mwaka 1998 akarudi tena studio kutengeneza album yake ya pili ikiitwa “Coupe bibamba” ambayo kimsingi ilikua inaelezea umaskini afrika,katika album hiyo alimshirikisha Jocelyne Beroard.Album hii nayo ikawa maarufu sana africa na ulaya na ikapata mauzo mazuri tu sokoni.

Awilo Live ndani ya CNN international na mwana mama Aisha Sisey wa Cnn

Mwaka 2000 Awilo akarudi tena studio kwa mara ya tatu na kutoka na album “Kafou Kafou” album ambayo ilimrudisha tena Kwenye KORA MUSIC AWARD 2001 ambapo this time alipata special award iliyojulikana kama “Judges Special Awards”

Pia Awilo amekua ni mwanamuziki aliyejipatia sifa nyingi sana kutokana na uchangamfu wa live performance zake kiasi cha kumfanya kuwa  MOST WANTED Congolese artists on the African continent and Europe akipata kazi nyingi sana kwenye nchi mbalimbali barani afrika kama Nigeria, Cameroon, Uganda, Tanzania, Burkina Faso, Kenya, Cote d’Ivoire, Benin, Togo Zambia, Gabon, Mali n.k… na pia nchi za bara la ulaya kama Switzerland, Belgium, Great Britain n.k. bila kuisahau United States.

Awilo ni mtoto wa  Vicky Longomba ambae alikua  ni mwimbaji kiongozi wa “Tout puissant OK Jazz (TP OK JAZZ)  ya Franco Luanzo Makiadi,pia alikua na kaka yake ambae alikua ni mwanamuziki maarufu wa bendi za Tanzania marehemu LOVII LONGOMBA ambae ndio baba wa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya wa kenya wakijulikana kama LONGOMBAS!Kwa hiyo utaona kabisa kwamba muziki uko kwenye damu ya AWILO

Wimbo Gate le Coin

Huyo Ndio Awilo Longomba angalau kwa uchache

Advertisements

11 Responses to Je wamfahamu sawa sawa Awilo Longomba alikotokea na alipofikia???

 1. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  I LOVE U …BABY TOUCH ME X 2 …ha ha haaaa !Awilo mtundu sana,yani huu wimbo enzi hizo nikiwa darasa la pili ulishika sana hapa ujiji..kila nyumba kulikuwa na hiyo santuri enzi hizo kinshasa inawaka moto kweli kweli,nakumbuka baba kila jioni alikua anawasha redio yake na kuweka santuri za Tabu ley ,franco na wengine kisha anakaa zake barazani anapata muziki taratibu,leo umenikumbusha mbali sana bro!

  Idd mubaraka kwa wote!nimefurahi sana.

 2. Anti-werra and Jb says:

  awilo anapata mafanikio kwa kuwa amejiweka kisasa zaidi,yani anafuata nyayo za wanamuziki wakubwa wa us ambao hawana mabendi makubwa zaidi ya kuwa solo,na kukodi wapigaji kila wanapopata kazi za kupiga shows,ndio anavofanya huyu awilo,hana bendi yeye ni solo artist forever!bendi zinazingua tu sometimez,awilo utamsikia kimya lakini akiibuka anatisha japo watu wanaponda style yake ya kupiga makelele lakini ndio yamekua yakimpatia tuzo na heshima kwenye concert zake.

  sasa haya ndio mambo sio kila siku werra na jb tuuuuuu!congo inao wanamuziki wengi!

 3. Fatuma Mtanga says:

  Awilo mtu wa watu kila mahali akienda anafunika,hanaga mapozi kaka wa watu aka!sema kweli amesahaulika sana mi hata sikujua kama bado anafanya kazi,lakini hizi video nilizoziona hapo hizo 2 za juu inaonesha bado wamo,mapromota wamlete na redio na tv zipige nyimbo hizi watu wajue yupo!!

  idd mubarak wadau j2 njema,nishashiba pilau nashushia na pepsi baridi!

 4. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  Awilo sijawahi kumpenda lakini jinsi alivyoupatia wimbo maze kuuharibu inanifanya nimfikirie upya

 5. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  Sorry typing error kaupatia sana wimbo maze wa tabu ley bila kuuharibu ndiop nilichomaanisha

 6. mkigoma kkoo says:

  kuhusu awilo kuwa na ndugu yake bongo ni kweli kabisa alikuwepo kaka ake akiitwa lovi longomba na bendi yake ya afriso ngoma mzee kitime ukimtembelaea bila shaka atakua na machache kuhusu lovi ambae ni baba wa elly longomba mchezo show wa zamani wa diamond sound kibinda a.k.a dsm ikibinda nkoi pamoja na wale wakenya longombas,lovii aliishi dar na nairobi pia ambako aliwazaa longombas na mwanamke wa kikenya,awilo pia kabla ya kuwa maarufu aliwahi kuja dar na kuishi kidogo na kakake hiyo ambae tayari alikua maarufu kenya na tz,lovi alifariki kwa ajali ya basi akitokea arusha kuja dar,alizikwa dar na papa wemba aliwahi kuzuru kaburi lake alipokuja tz kwenye moja ya ziara zake hapa nchini

 7. Farid From Muscat says:

  umenirudisha nyuma miaka 21 kwa kumtaja Awilo maana nakumbuka kuna FILM ya kicongo ilikua inaitwa KURU ambayo sterling wake alikua Papa Wemba , ndani ya filamu hiyo anaonekana Awilo akiwa yanki mdogo akicharaza drums vibaya sana na wengine katika filamu hio ni akina Pepe Kalle na Emoro na mastar wengi wa wakati ule.
  na mwaka 2001 Awilo alitembelea hapa kwetu Muscat na akapiga show mbili kabambe haitosahaulika maana toka aliingia kuperfom mpaka anafunga jukwaa hakuna aliekaa chini watu wote walikua wakinesa tu si wahindi si warabu wote walijikuta wakisakata ngoma.

 8. Anonymous says:

  hamna kama awilo congo mobimba…awilo yuko kimataifa zaidi,jb na werra hamna lolote sema watu wanawafagilia for nothing,awilo anaalikwa kutumbuiza mpaka uarabuni habu niambie jb na werason wapi na wapi,nani kati yao kawahi kuhojiwa na cnn??????

 9. natamani sana ipo siku nitakuja kuonana na awilo

 10. Bila kumsahau mwana dada machachali enzi izo yondo sister miaka ya 1992_1997 sikuona wengine zaidi ya wakongo kipindi hicho nahitim elim yangu ya msingi mwaka 1994 huko puge nzega tabora

 11. PAUL MATHIAS says:

  Nashukulu sana kwa kunifumbua macho kwan nilikuwa sijui kuusu awilo. na pia tukiachana na hayo mi ni kijana natafuta mch

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: