Je wamfahamu sawa sawa Awilo Longomba alikotokea na alipofikia???

November 6, 2011

Na The Romantic

Kama wewe kweli ni mpenzi wa miziki ya bana congo jina Awilo Longomba litakua si geni sana masikioni mwako, Awilo Longomba ni mwanamuziki machachari kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya watoto wa congo ambaye mwanzo alianza muziki kama drummer boy akipiga drum kwenye bendi mbalimbali kama Viva la musica ya Mzee Papa Wemba “mwalimu”, Stukas, Nouvelle Generation ambayo alikua kiongozi wake na Loketo Group kazi ambayo alidumu nayo mpaka mwaka 1995 ambapo aliachana na drum na kujikita kwenye uimbaji na utunzi ambapo mwaka huo huo 1995 aliachana na La Nouvelle Génération na kutoka solo na album yake ya kwanza  “Moto Pamba” ambayo alitunga nyimbo zote,kuimba na pia kupiga drums.Baada ya mafanikio ya album hiyo aliamua kuachana rasmi kabisa na drums na badala yake akajikita kwenye kutunga na kuimba huku akipata mialiko katika nchi mbalimbali za ulaya na africa mashariki kenya na Tanzania hususan.

Hapa Awilo akiimba wimbo Ma’ze wa mzee Tabu Ley ambao hapa ameufanyia ukarabati na kuurekodi kisasa zaidi:

Ilikua ni solo album yake hiyo hiyo ya kwanza iliyompatia heshima ya Best Central Africa Artist Awards” kwenye KORA MUSIC AWARDS 1996 and 1997 (All Africa Music Awards, held in Sun City, South Africa).

Hapa Awilo anafanya balaa…anachombeza  na mambo ya “Lopelee” ya jb mpiana

Kutoka hapo hakuna aliyeweza kuuzima moto aliouwasha Awilo,akawa hakamatiki tena,ambapo mwaka 1998 akarudi tena studio kutengeneza album yake ya pili ikiitwa “Coupe bibamba” ambayo kimsingi ilikua inaelezea umaskini afrika,katika album hiyo alimshirikisha Jocelyne Beroard.Album hii nayo ikawa maarufu sana africa na ulaya na ikapata mauzo mazuri tu sokoni.

Awilo Live ndani ya CNN international na mwana mama Aisha Sisey wa Cnn

Mwaka 2000 Awilo akarudi tena studio kwa mara ya tatu na kutoka na album “Kafou Kafou” album ambayo ilimrudisha tena Kwenye KORA MUSIC AWARD 2001 ambapo this time alipata special award iliyojulikana kama “Judges Special Awards”

Pia Awilo amekua ni mwanamuziki aliyejipatia sifa nyingi sana kutokana na uchangamfu wa live performance zake kiasi cha kumfanya kuwa  MOST WANTED Congolese artists on the African continent and Europe akipata kazi nyingi sana kwenye nchi mbalimbali barani afrika kama Nigeria, Cameroon, Uganda, Tanzania, Burkina Faso, Kenya, Cote d’Ivoire, Benin, Togo Zambia, Gabon, Mali n.k… na pia nchi za bara la ulaya kama Switzerland, Belgium, Great Britain n.k. bila kuisahau United States.

Awilo ni mtoto wa  Vicky Longomba ambae alikua  ni mwimbaji kiongozi wa “Tout puissant OK Jazz (TP OK JAZZ)  ya Franco Luanzo Makiadi,pia alikua na kaka yake ambae alikua ni mwanamuziki maarufu wa bendi za Tanzania marehemu LOVII LONGOMBA ambae ndio baba wa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya wa kenya wakijulikana kama LONGOMBAS!Kwa hiyo utaona kabisa kwamba muziki uko kwenye damu ya AWILO

Wimbo Gate le Coin

Huyo Ndio Awilo Longomba angalau kwa uchache

Advertisements

Shime watanzani siku zimeisha

November 6, 2011

image


%d bloggers like this: