Muziki kuwagawa wapiga kura wa Congo

November 3, 2011

image

Kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini Congo zimewagawa wanamuziki kiasi kwamba uhasama wao unaingia kwa mashabiki. Kwa mujibu wa uchunguzi wa mtyandao wa Digital Congo zaidi ya Bendi au wanamuziki ishirini na tano hivi wanamuunga mkono Rais Joseph Kabila, ikiwa ni pamoja na majina makubwa kama Papa Wemba, Koffi Olomide, JB Mpiana, Werrason, Felix Wazekwa, Tshala Muana na kulindwa Meje 30, pia kuna Blaise Bula, Karmapa, Dakumuda, Lofombo, Tsaki Kongo, nk.

Wanamuziki wanaomuunga mkono Kabila wanaainisha mafanikio ya Rais huyo kwa kipindi chake cha Utawala nchini humo.

Ikumbukwe kuwa KAbila aliwahi kupiga marufuku mtindo wa Mabanga na kukataza wanasiasa kuimbwa kwenye nyimbo na kesi ya hivi karibuni ni ya Bado anakumbuka kesi moja kati ya Papa Wemba na Waziri wa Fedha Matata Ponyo. Yeye alikuwa ameamuru mwimbaji Papa Wemba kuondoa jina lake kutajwa katika moja ya nyimbo katika albamu ya “Baba yetu”. Isipokuwa kwamba inathibitisha wimbo huo ungetumika kuelezea utawala bora. Naye Papa wemba alimjibu kuwa wao ni viongozi na vioo vya jamii hivyo wanamuziki ni bure kwa kujitolea nyimbo zao kwa wagombea wakati wa kampeni hiyo.

Wakati baadhi ya wanamuziki na kuweka macho yao juu ya Joseph Kabila wa urais, wengine wamechagua kwa washindani wa aliyeko madarakani. Hivyo, mkuu wa Wenge El Paris, Marie-Paul Ashish Beles alikuwa na upande mmoja na upinzani.

Na kwa mwisho wa kampeni uliopangwa kufanyika Novemba 26, wimbo wa sifa kwa kiongozi wa Umoja wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii (UDPS) itakuwa tayari baadhi ya matangazo kwenye njia TV.

Ikumbukwe kuwa jitihada na harakati hizi zimesababisha wanamuziki hao hasa wale wanamuunga mkono Rais Kabila na kumtupa Etiene Tsisekedi ambaye anapendwa na wapinzani maisha yao kuwa magumu hasa nje ya Congo miji kama Bruxelles, Paris, Africa ya Kusini na Canada ambako wacongo wengi wanaishi kumeripotiwa matukio ya ghasia dhidi ya mashabiki wa Upinzani ambao hutembelea maduka yanayouza santuri, CS, DVD za wanamuziki hao na kuzichoma moto.

Ndoa ya wanamuziki hao na wanasiasa ni ya muda na ikumbukwe kuwa muziki ni aina ya starehe ama burudani ambayo inakusanya watu wengi wa rika zote na inakuwa na mguso kwenye jamii nzima.

Sasa oparation za wanaharakati hao zimechukua sura mpya kwa vijana hao kuanza kuvamiwa maduka ya muziki huko ulaya na kushinikiza wapewe cd zote zilipo kwenye duka husika za wanamuziki Jb Mpiana, Werrason na Koffi Olomide kwa madai wanamuziki hao wamekuwa wakiutumia umaarufu na ushawishi wao kumsaidia kisiasa rais KABILA ili ashinde uchaguzi ujao wa congo.Vijana hawa imekua ikionekana kama vile wako above the law na hakuna wa kuwazuia kiasi wamekuwa wakifanya uharamia wao huo hadharani tena bila kificho kama mtakavyoona hapo chini kwenye video hiyo walipolivamia moja ya maduka maarufu ya muziki na kuanza kushinikiza wapewe cd husika zote ili wakazi destroy, kiukweli mimi binafsi hii imenikera sana inakuwaje nchi ya ulaya kama Belgium au France ishindwe kukidhibiti kikundi hiki?je nani analifadhili genge hili?maana sidhani kama vijana hao wanaoonekana hapa wanaweza kuwa organized kiasi hiki bila kuwa na mkono wa mtuau watu wazito  nyuma yao.

Mtamuona na kumsikia hapo mwanzo wa video Werrason anavyosikitika na kuwasihi vijana hao wasiwahukumu kwa kumpigia debe Kabila kwani hawakuanza wao toka enzi za Mabutu kina Franco walikua wakiimba nyimbo za kumsifu rais.

All in all hii ya kupora cd na dvd madukani itawaathiri sana wanamuziki husika, kwani hakuna mfanyabiashara ya muziki atakubali kuweka kazi za wasanii hawa kwani itakua ni hasara kwake Le Combattants wakivamia duka lake. Mimi nadhani serikali ya kabila inatakiwa ifanye kitu,iwasiliane na serikali husika France na Belgium kuwadhibiti hawa wanaharakati, walianza kama utani sasa wanaelekea kubaya,na kama utawasikia utaona wanavyojaribu kutishia kwamba kila mahali mcongoman alipo akae mbali na jb,werra na koffi na kazi zao,wanasema wako kila mahali,canada,us ,uk,france,Belgium na nyumbani congo.

Issue ni serious wadau,hapa chini wamevamia duka lingine la  luxene Musengi na kumnyanyasa mwenyewe vibaya sana

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=e3t1H8QkzYk

Advertisements

Thomas Ulimwengu azidi kung’ara TP Mazembe

November 3, 2011

image

Thomas Ulimwengu akiwa ndani ya Jezi ya TP Mazembe ya Congo

Mchezaji wa Tanzania Thomas Ulimwengu anazidi kung’ara huko TP Mazembe.

Kwa mujibu wa mtandao wa TP Mazembe ambayo Ulimwengu anachezea, kwa takribani miezi mitatu sasa  Ulimwengu amekuwa akigonga vichwa vya habari na kusifiwa kwamba anaweza akawanyima wakongwe namba.

Ulimwengu ambaye ametimiza miaka 18 mwezi Juni mwaka huu aling’ara sana akiwa na timu ya Taifa ya chini ya miaka 17 kwenye michuano ya CECAFA 2009 alipokuwa mfungaji bora. Baadaye Ulimwengu aliitwa na Maximo kwenye kikosi cha tiumu ya wakubwa .

alipokuwa katika timu ya U-20 bado anakumbukwa kwa mabao tisa aliyofunga kwenye mechi tano katika michuano ya Copa Coca Cola 2010 nchini Afrika ya Kusini.

Baadaye walitakiwa kujiunga na Academy huko Sweden ya AFC kisha TP Mazembe waliwachukua huko mpaka leo ambapo washakuwa wachezaji tegemezi.

Ulimwegu alifunga bao kwenye mechi yake ya kwanza kuichezea TP Mazembe.

Kwa sasa Ulimwengu yumo kwenye kikosi cha Taifa Stars kitakachopambana na Chad baada ya kuitwa na kocha Paulsen wa Taifa Stars.

image

Picha zote kwa hisani ya TP Mazembe Website.


%d bloggers like this: