Ezzau Wimbo wa JB Mpiana unaotegua kitendawili cha nani mtunzi wa Mulolo??

image

Wakiongwe wa Wenge Musica toka kushoto, Adolph Dominguez, Engineer Blaise Bulla, Werrason Ngiama Makanda, Vando Mass Didie Masela, JB Mpiana Mukulu Papa Cherry na Allain Prince Makaba.

Na The Romantic

Katika siku za karibuni humu ndani kuliibuka ubishi wa hapa na pale kuhusu mtunzi wa nyimbo MULOLO na KIN E BOURGER kati ya Jb Mpiana na Werrason,nikianza na wimbo mulolo ambao ndio wenye matatizo zaidi, kihistoria wimbo huu asili yake kiukweli ni kijijini kwao werrason ndio maana ndani yake kuna mahali hawaimbi lingala, kuna lugha flani ukisikiliza kwa makini utaisikia, lugha hiyo ni “KIMBALA” ambayo ni lugha ya asili ya eneo analotoka werrason, hapo ndipo watu wanapochanganyikiwa kuhusu mtunzi wa huu wimbo ambao uliimbwa enzi hizo werrason akiwa animator/atalaku au rapper wa wenge!! (hii wengi hawaijui, ndiko alikoanzia kabla ya ekokota). Na wimbo huu huko kwa kina werra huimbwa anapozaliwa mtoto au kumsifia mtu anapofanya kitendo chochote cha kishujaa, wenge wakaubadilisha na kuutengeneza kisasa kutoa ujumbe kwa wapenzi waje waone bendi mpya wenge musica imezaliwa.

Lakini yote kwa yote swali linabaki pale pale nani mtunzi hasa wa wimbo huu mzima? adea ilikua ya nani,mashairi ya kuanzia yaliletwa na nani????? Maswali hayo pamoja na yale ya mtunzi wa wimbo KIN E BOURGER yanajibiwa na JB Mpiana katika wimbo wake “EZZAU” ndani ya album ya ANTI TERRO.

Ndani ya kibao hicho, Jb kuna mahali kuanzia dk ya 4:10 anasema maneno haya; sikiliza message

      “Histoire echangeaka te Papa Wemba aah……!

      “Histoire echangeaka te Josky Kiambukuta eeh..!

      ”Histoire echangeaka te  Presidaa Nyoshi eeh….!

      “Nzembo nangaa ya MULOLO..ebimisa wenge…!

      “Nzembo nangaa ya KIN E BOURGER  e confirma wenge..!

      “Bolinga bolinga te ba temoins nangaa bazali public na Nzambe veritee yango wana”

Tafsiri yake anasema :

Hakuna mwenye anaweza kubadilisha historia, anawataja wakubwa zake hapo…Papa wemba, Josky kiambukuta, Presidaa Nyoshi (Nyoka Longo wa zaiko).

Anaendelea kusema wimbo wangu MULOLO ndio ulioitoa wenge kusikojulikana…. baadae wimbo wangu KIN E BOURGER ndio uliokuja kuifanya wenge itambulike zaidi…..ukubali ukatae lakini wapenzi na mungu wanaujua huo ukweli….

Mwisho kabisa anasema bana congo mobimba tolingana (watoto wote wa congo tupendane)…anawataja na jamaa zake katika wenge original enzi hizo akisema yeye jb mpiana,werrason,didier masela,alain makaba,Blaize Bulla,Dominguez tolingana(tupendane)

wimbo mzima EZZAU,wa kwake JB Mpiana ndio huu,sikiliza message hapo:

 

wimbo Mulolo unaogombewa huu hapa,enzi hizo hapo ni JB Mpiana na Werrason

Advertisements

12 Responses to Ezzau Wimbo wa JB Mpiana unaotegua kitendawili cha nani mtunzi wa Mulolo??

 1. Stivin says:

  Mulolo ulitungwa na Mjomba ake werrason, sio JB wala Werra! Kone bouge ulitungwa na Mpiana!

 2. Farid from Muscat says:

  Nikiwa kama mwanawenge ninafuraha kubwa kisoma khabari hii na salaam zangu ziwafikie ndugu zangu wote wanawenge bila kumsahau big Bro weti Pius Mzee

 3. BABA MARTHA says:

  KWA SISI WAPENZI WA WENGE MUSICA BCBG, TUNAJUA WAZI KWAMBA MULOLO ULITUNGWA NA JB MPIANA, KWANZA KABISA KILA MTUNZI WA WIMBO WAKE, YEYE NDIYO ALIKUWA WA KWANZA KUIMBA VERSE, LABDA WIMBO UWE UMETUNGWA NA MPIGA VYOMBO, KWAHIYO UKIHANGALIA NA KUSILIZA HUO WIMBO JIBU UNAKUWA NALO WALA HAKUNA HAJA YA KUBISHANA.

 4. peter says:

  Charismatic singer !!! Inamaana kubwa Kubwa sana katika WENGE CLAN!!Naomba mashabiki kabla ya kuanza kubishana saaaana tuichambue sauiti ya JIBE MUKULU PAPA cherry BABA DAIDA TSHITUKA …ukilifahamu hilo utajuwa siri ya mjadala huuu ..TUACHE USHABIKI…..tuchimbe zaidi …Big remerciment a LE HADJE JIBENIQUE

 5. peter says:

  Charismatic singer !!! Inamaana kubwa Kubwa sana katika WENGE CLAN!!Naomba mashabiki kabla ya kuanza kubishana saaaana tuichambue SAUTI ya huyu jamaaa JIBE MUKULU PAPA cherry BABA DAIDA TSHITUKA …ukilifahamu hilo utajuwa siri ya mjadala huuu ..TUACHE USHABIKI…..tuchimbe zaidi …Big remerciment a LE HADJE JIBENIQUE

 6. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  kwisha kazi hakuna ubishi tena hapa,na werrason sasa aache kuutumia huu wimbo pamoja na djo djo ngonda kwenye ma concert zake,sio za kwake,djo djo bcbg wanahaki ya kuutumia kwa kuwa mwenye nao ficare mwamba bado yupo bcbg,mbona hatuoni bcbg wakipiga kalayi boeing?tuheshimu kazi za watu.

  asanteni kwa kunisikiliza.

 7. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  asanteni sana kwa stori nzuri jamani.mungu awabariki wote kwa kazi nzuri.

 8. Fatuma Mtanga says:

  ubishi kwishney sasa

 9. peter says:

  MWAMBA alijitahidi sana kulipiga solo katika huu wimbo mulolo onyesho la Live au Zenith ’99 aisee ni bonge la wimbo…..shai ngenge aliimba nafasi ya jibe motopamba….inapendeza sana

 10. The issue that u have discussed in this article is very much common nowadays . Thank You so much for giving me the tips

 11. At this time it appears like Expression Engine is the preferred blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

 12. Mei Wegmann says:

  I want you to thank for your time of this wonderful go through!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: