Ezzau Wimbo wa JB Mpiana unaotegua kitendawili cha nani mtunzi wa Mulolo??

November 1, 2011

image

Wakiongwe wa Wenge Musica toka kushoto, Adolph Dominguez, Engineer Blaise Bulla, Werrason Ngiama Makanda, Vando Mass Didie Masela, JB Mpiana Mukulu Papa Cherry na Allain Prince Makaba.

Na The Romantic

Katika siku za karibuni humu ndani kuliibuka ubishi wa hapa na pale kuhusu mtunzi wa nyimbo MULOLO na KIN E BOURGER kati ya Jb Mpiana na Werrason,nikianza na wimbo mulolo ambao ndio wenye matatizo zaidi, kihistoria wimbo huu asili yake kiukweli ni kijijini kwao werrason ndio maana ndani yake kuna mahali hawaimbi lingala, kuna lugha flani ukisikiliza kwa makini utaisikia, lugha hiyo ni “KIMBALA” ambayo ni lugha ya asili ya eneo analotoka werrason, hapo ndipo watu wanapochanganyikiwa kuhusu mtunzi wa huu wimbo ambao uliimbwa enzi hizo werrason akiwa animator/atalaku au rapper wa wenge!! (hii wengi hawaijui, ndiko alikoanzia kabla ya ekokota). Na wimbo huu huko kwa kina werra huimbwa anapozaliwa mtoto au kumsifia mtu anapofanya kitendo chochote cha kishujaa, wenge wakaubadilisha na kuutengeneza kisasa kutoa ujumbe kwa wapenzi waje waone bendi mpya wenge musica imezaliwa.

Lakini yote kwa yote swali linabaki pale pale nani mtunzi hasa wa wimbo huu mzima? adea ilikua ya nani,mashairi ya kuanzia yaliletwa na nani????? Maswali hayo pamoja na yale ya mtunzi wa wimbo KIN E BOURGER yanajibiwa na JB Mpiana katika wimbo wake “EZZAU” ndani ya album ya ANTI TERRO.

Ndani ya kibao hicho, Jb kuna mahali kuanzia dk ya 4:10 anasema maneno haya; sikiliza message

      “Histoire echangeaka te Papa Wemba aah……!

      “Histoire echangeaka te Josky Kiambukuta eeh..!

      ”Histoire echangeaka te  Presidaa Nyoshi eeh….!

      “Nzembo nangaa ya MULOLO..ebimisa wenge…!

      “Nzembo nangaa ya KIN E BOURGER  e confirma wenge..!

      “Bolinga bolinga te ba temoins nangaa bazali public na Nzambe veritee yango wana”

Tafsiri yake anasema :

Hakuna mwenye anaweza kubadilisha historia, anawataja wakubwa zake hapo…Papa wemba, Josky kiambukuta, Presidaa Nyoshi (Nyoka Longo wa zaiko).

Anaendelea kusema wimbo wangu MULOLO ndio ulioitoa wenge kusikojulikana…. baadae wimbo wangu KIN E BOURGER ndio uliokuja kuifanya wenge itambulike zaidi…..ukubali ukatae lakini wapenzi na mungu wanaujua huo ukweli….

Mwisho kabisa anasema bana congo mobimba tolingana (watoto wote wa congo tupendane)…anawataja na jamaa zake katika wenge original enzi hizo akisema yeye jb mpiana,werrason,didier masela,alain makaba,Blaize Bulla,Dominguez tolingana(tupendane)

wimbo mzima EZZAU,wa kwake JB Mpiana ndio huu,sikiliza message hapo:

 

wimbo Mulolo unaogombewa huu hapa,enzi hizo hapo ni JB Mpiana na Werrason


%d bloggers like this: