Zaiko Langa Langa, wakongwe wa muziki Congo.

image

Huwezi kuzungumzia Congo pia bila kuwataja Zaiko Langa Langa chini yake Nyoka Longo.

Zaiko wamekuwa maarufu na kuendeleza umaarufu wao tangu kuanzishwa kwake miaka ya sabini huko wakati huo Congo ikiitwa Zaire. Kwa mtu asiyejua na kwa we msomaji kwa taarifa yako watu kama Papa Wemba, Bozi Boziana, Dindo Yogo, Evolocko Jocker na Nyoka Longo wote ni kizazi cha Zaiko Langalanga.

Kama ilivyo Wenge Musica na makundi yake, Zaiko nayo imefanikiwa kuzaa bendi nyingi kama Isifi Lokole, Viva La Musica, Langa Langa Stars, Zaiko Familia Dei, Anti Choc, Choc stars, and Zaiko Nkolo Mboka.

Ilianzishwa rasmi mwaka 1970 wakati huo ikijulikana kama Orchester Zaiko, baadaye kidogo washabiki wakaanza kuwaita Langa Langa wakimaanisha “Kulewa” kwa kuwa nyimbo zao zilikuwa zikipigwa sana kwenye vilabu vya pombe kila kona. Waanzilishi wakiwa ni Papa Wemba, Evolocko Lay Lay, Zamungana na  Nyoka Longo.

Zaiko ndio waanzilishi wa sebene la leo ambapo wao walichukua mtindo wa kiasili na kuingiza ala kama magitaa, Chants, na rap kwa mbali jambo lililonogesha muziki wao na kuufanya kupendwa na rika lote.

Mwaka 1973 Zaiko walikuwa maarufu sana si tu kwa Zaire bali hata kwa nchi za jirani huku mwanamuziki wake Evolocko Jocker akiwa ni maarufu sana kwenye bendi hiyo ambapo aliweza kuingiza mtindo maarufu wa cavacha wa uchezaji ambao ulikuwa maarufu sana na kupendwa kote.

Miaka ya kati kati mwa sabini bendi hii ilianza kumong’onyoka ambapo waliondoka walikuwa wanamuziki wake maarufu kama Papa Wemba ambaye aliondoka na Bozi Boziana, Evolocko na  Mavuela ambao kwa pamoja walianzisha Bendi iliyoitwa Isifi Lokole, ambayo hata hivyo haikukaa sana kwani nayo ilimeguka na kutoa bendi mbili Yoka Lokole, na  Viva La Musica ya Papa Wemba.

Mwishoni mwa miaka ya sabini Bendi ilikuwa iko juu si mchezo huku wanamuziki wake wakiwa wanasifika kwa kila kitu, inakumbukwa wanamuziki kama Nyoka Longo, Lengi Lenga, Bimi Ombale, Dindo Yogo, Evolocko walileta laha sana kwenye bendi hii.

Ilienda mpaka miaka ya mwanzoni mwa 80 ambapo bendi ilimeguka tena. Hii ilitokana na wakongwe kama Meridjo, Nyoka Longo na  Dindo Yogo kutokubaliana na mambo waliyoyaita mageuzi ambayo yaliletwa na vijana wapya kama Lengi Lenga, Ilo Pablo na Bimi Ombale. Hii ilipelekea kusambaratika na kundi la akina Nyoka Longo likajiita Zaiko Langa Langa Nkolo Mboka, na lile la Bimi likajiita   Zaiko Langa Langa Familia Dei. Makundi yote kwa pamoja yanamafanikio na mchango mkubwa kwenye ulimwengu wa Muziki wa Congo.

Post hii imewekwa tena baada ya maombi ya mdau papaa Julie Weston nakati ya Kigamboni Tajiri mtoto Julie Magold, Julie wa Mawe

Hizi hapa ni baadhi ya kazi zao toka mwaka 1970

 • 1970 : Pauline
 • 1972 : L’amoureux decu
 • 1973 : Mete la vérité, chouchouna
 • 1974 : Liwa ya somo
 • 1981 : Sarah Djenni
 • 1983 : La Tout Neige
 • 1985 : Zaiko Eyi Nkisi
 • 1985 : Eh Ngoss! Eh Ngoss! Eh Ngoss!
 • 1986 : Bongoville
 • 1986 : Pusa Kuna… Serrez! Serrez!
 • 1987 : Bongama Kamata Position
 • 1987 : Subissez les conséquences
 • 1988 : Nippon Banzai au Japon
 • 1989 : Jetez l’Eponge
 • 1990 : Zaiko Langa-Langa F. D.
 • 1992 : L’Autentique Zaiko Langa Langa
 • 1993 : Jamais sans nous
 • 1993 : Zaire-Ghana (recorded in Accra in 1976, produced by Henri Bowane)
 • 1995 : Avis de recherche
 • 1995 : Zekete Zekete
 • 1996 : Sans issue
 • 1996 : Pacha labaran
 • 1997 : Papa Omar
 • 1997 : Onassis
 • 1997 : Muvaro
 • 1997 : Le beau temps
 • 1997 : Bongo bouger
 • 1997 : Bacline Lesson One
 • 1997 : Poison
 • 2000 : Etumba ya la vie
 • 2001 : Legend
 • 2002 : Anthologie
 • 2003 : Sentiment Awa / Essesse
 • 2003 : Eureka!
 • 2004 : Empreinte
 • Zaire Congo Dance
 • Zaiko Langa Langa
 • Saisie en Douane… 20 Ans Déjà
 • Ici Ça Va… Fungola Motema
 • Out of Africa

2 Responses to Zaiko Langa Langa, wakongwe wa muziki Congo.

 1. Hadj le Jbnique says:

  Amani juu yenu waungwana wote humu ndani,leo naona tuna zaiko hapa,nimefurahi mzee kutukumbusha Bendi hii yenye historia ndani ya KIN na CONGO kiujumla.Kwangu mimi Zaiko ndio baba ya Muziki ya Congo Kinshasa,imepita vipindi vingi vigumu na kufaulu kubakia kama ZAIKO,hakuna kipindi ambacho mimi kwa maoni yangu nadhani watu wengi waliamini ingekuwa mwisho wa Zaiko,hicho ni kile kipindi kigumu kwao walipoondokewa na wapigaji solo mahiri BENIKO POPOLIPOO,JIMMY YABA na PETIT POISSON.Hawa waliondoka pamoja na waimbaji na watunzi wa kutegemewa kama kina LENGOS,YA OMBALE na YA JP BUSE.Lakini kamanda mkuu “mpiganaji asiyechoka” wa kikosi cha ZAIKO,muzee NYOKA LONGO aliwaleta vijana vijana underground wenye vipaji vya ajabu ambao ni wapiga solo kama SHIROO MVUEMBA,”Fundi Mtaalam” BAROZA na wengine ambao waliifanya ZAIKO kuwa moto mara mbili zaidi na kufikia kuwa bendi bora CONGO kwa kipindi hicho,kwani baada ya kuwa recruit vijana hao wapya ikafika siku ambayo zaiko walipiga show kwa ajili ya kuwatambulisha vijana,basi vilipopigwa vibao vya zaiko vya zamani ambavyo magitaa yake yalipigwa na kina POPOLIPOO,Huyo kijana BAROZA ambaye ndio alikua mpiga solo mpya badala ya POPOLIPOO Alibadili ile mitindo ya kizamani ya popolipo na kupiga kwa style yake mpaka kuwapagawisha wapenzi waliojazana hapo KIPWAZA BAR ndani ya KIN Mpaka watu kufikia kuasema mki lingala “Bora kina popolipoo waliondoka,hawa ndio wapigaji tunaowataka”,huku NONO ATALAKU yule repa wao mahiri nae kwa jinsi alivyopagawishwa na gitaa la BAROZA alisikika akitomboka katikati ya sebene maneno haya “BAROZAAA,TIKA KOLELA MWANA YA MAMAA!BAKOKI PE KOKENDE NA NAIROBII…AAH MAWA TROP!” Akimaanisha mkiswahili BAROZA mtoto wa mama acha kuliza hilo gitaa,wenzio wameishiwa ndio maana wamekimbilia Nairobi…aah shida tupu!.Hapo alikua anawapiga dongo kina popolipoo ambao walikuwa Nairobi wakipiga muziki huko.Kuanzia hapo BAROZA Akatukuzwa na kuitwa “LE ROI LION” yaani mfalme simba,kaja watu wamekimbilia kenya.Kinshasa moto jamani nyie acheni tu,KIN raha.Pia naikumbuka ZAIKO enzi zile WENGE MUSICA ORIGINAL ilipokuwa imeshika hatamu kuna siku walipiga show ya pamoja,mzee ilikua balaa,maana ulikua ni kama mpambano wa marepa MOMBELE wa Zaiko wakati huo na “LE GRAND CHIBUTA” ROBERTO EKOKOTA WUNDA,Yule repa bora kabisa kupata kutokea wa wenge musica ambae maskini alilazimika kuacha muziki akiwa bado kijana mdogo kutokana na matatizo ya kiafya na kumuachia jahazi YOMBO LUMBU A.K.A.TUTU KALUDJI.Stori ndefu ngoja niishie hapa niwapishe na wengine.sorry kwa kuwachosha.

 2. Alain Kabangu says:

  Hadj le Jbnique, Pius ngoja niwape undani zaidi juu ya zaiko kutoka hapa kinshasa.

  Mmeongea na kuchanganya vitu hivyo ngoja niwasahihishe.

  Zaiko ilianzishwa mwaka 1969, na waasisi wake ni kina Ya Nyosh (Nyoka Longo alias Ya Jossart, Evoloko Lay Lay (Jocker), Manuaku Waku (Pepe Felly), Bimi Ombale, Andre Bita, Gege Mangaya (baadaye akaenda O.K. Jazz kisha akarudi Zaiko miaka ya 90), President na founder wa Zaiko D.V. Moanda, Ya Enock Zamuangana, Mbuta Mashakado, Teddy Sukami, Marry Djo, etc.

  December 1969 Wakati Zaiko ilipokuwa inafanya mazoezi ya nyimbo zake (za kukopi) nyumbani kwa kina Andre Bita, Gege Mangaya alimchukua rafiki yake (Jules Shungu wembadio Pene Kikumba “Papa Wemba”) kwenda kumtakia hali rafiki wa Gege Mangaya ambaye alikuwa amekuja toka Ubelgiji. Huyu rafiki wa Gege alikuwa ndugu na kina Andre Bita na alifikia kwao ambako ndiyo ilikuwa sehemu ya mazoezi ya Zaiko wakati wanaanza muziki. Kufika kule wakakuta Zaiko wanafanya mazoezi katika chorus huku wakiongozwa na Nyoka Longo na Evoloko Lay Lay. Bahati mbaya wale jamaa kila wakitia sauti kulikuwa na itilafu fulani ndipo Papa wemba akaomba aimbe na kupewa nafasi. Papa wemba aliambiwe aimbe ule wimbo wa Adios Tete wa Tabu Ley. Jamaa akaimba mpaka mwenye bendi ya Zaiko D.V. Moanda akawafukuza wale waimbaji na kumchukua Papa Wemba azibe nafasi zao. Ndio hapa zaiko ikajipanga upya na waimbaji wafuatao: Nyoka Longo, Papa Wemba, Evoloko Lay Lay, Mavuela Somo, pamoja na Bimi Ombale. Vijana walijitahidi kimazoezi mwaka 1970 ndipo wakatoka rasmi.

  Manuaku Waku (soloist) ndiye aliyesema kuwa wawe tofauti na wenzao maana kwamba wawe bendi ya sebene na siyo rhumba, hivyo wakaachana na upulizaji wa matarambeta na sax. Wakapata sifa sana mpaka Franco akaanza kuwachukia na kuwachochea ili ife. Zaiko ikaendelea kutamba na kuchukua mashabiki kila kona ya nchi. Mwaka 1972 wakapata mwanamuziki machachari mwimbaji Gina Wa Gina ama Efonge. Huyu jamaa alikuwa na mbwembwe jukwaani mpaka akawa anampita Nyoka Longo kwa mwembwe. Mwaka 1974 akaja Bozi Boziana na mwaka huo huo Zaiko ikawa bendi bora zaire. Mwaka Uliofuatia 1975, baada ya kupata sifa nyingi kina Evoloko, Papa Wemba, Bozi Boziana, na Mavuela (wote waimbaji) wakatimka kwenda kuanzisha Isifi Lokole chini ya star wao Evoloko. Kule hawakudumu kwani kila mmoja alitaka kuwa kiongozi kutokana na wote kuwa mastaa yaani kama vile kuwe na Blaise Bula, JB Mpiana, Dominguez, na werrason bendi moja kipindi kile cha wenge.

  Baada ya kuondoka hawa jamaa yaani kina Evoloko na wenzake, Zaiko ikawa juu sana kupita mwanzoni kwani nafasi za Evoloko na Papa wemba zilizibwa na kina Lengi Lenga, na Likinga, hawa waliingia Zaiko mwaka 1975 baada ya kutoka kina Evoloko. Hivyo safu ya uimbaji ikawa Nyoka Longo, mbuta Mashakado, Lengi lenga, Bimi Ombale, na Likinga. Hapa ndipo Zaiko ilikuwa moto wa kuotea mbali kwani mwaka 1976 ikawa tena bendi bora ya Zaire.

  Baada ya isifi kugawanyika na Papa Wemba kwenda jela baada ya kubaka. Mwaka 1977 Papa wemba akarudi jela baada ya mwaka huko na kuunda Yoka Lokole ambayo haikukaa muda, ndipo akaanzisha Viva La Musica mwaka 1978. Mwaka 1977 Bozi akarudi zaiko, na hatimaye Evoloko baada ya kuishiwa akarudi zaiko mwaka 1979.

  Mwaka 1980 Manuaku aliondoka Zaiko na kumchukua Mbuta Otis kwenda kuunda Grand zaiko. Mwaka 1981 Evoloko tena baada ya kurudisha sifa zake za mwanzoni akamchukua Bozi, Petit cachet, Djomali, kwenda kuunda langa Langa Stars.

  Mwaka 1984 ndipo akaja Dindo Yogo (huyu jamaa alikuwa na bendi yake miaka ya 1970 ikiitwa Ngwaka Aye, alikuwa na mwimbaji ambaye huko TZ mnajuwa sana akiitwa Lovy Longomba kaka yake na Awilo baba yao Vicky Longomba aliyekuwa na OK Jazz) miaka ya 1960’s mpaka 1970’s mwanzoni kabla n yeye kuanzisha bendi yake.

  Mwaka 1988 ndipo Zaiko ikapata ten mtafaruku baada ya swahiba mkubwa wa Nyoka Longo Lengi Lenga na Bimi Ombale kuondoka na kwenda kuanzisha Familia dei (Zaiko langa Langa – Familia dei). bendi iligawanyika kwani nusu ya bendi iliondoka na kwenda huko Familia Dei. Hapa mze mzima Nyoka aka recruit kina Adamo, malage, Cele mbonda, Baroza, Shiro, Petiti Aziza, Alpha Kopeya, Tylon, na wengine wengi kuziba yale mapengo yaliyoachwa. Cha kushangaza Zaiko ndipo ikaja juu zaidi na kutoa albam yao ya kwanza ya Jetez l’eponge. Kwa kweli hiii bendi kila inapopata misukosuko ndipo inapata nguvu zaidi.

  Ikumbukwe kuwa ni Zaiko ndiyo iliyoanzisha haya masebene ya cavacha mpaka na huu upigaji wa drums mnaousikia sasa muasisi akiwa Merry Djo “Machine Ya kauka”,

  Na sasa Adamo na wenzake wamebaki Ubelgiji na kuunda bendi yao ikiitwa zaikas (watoto wa zaiko). nyoka longo na wenziwe hapa Kin wamerecruit vijana wapya hivyo subirini mapigo ya nguvu toka kwao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: