Single myimgime ya WMMM yaingia sokoni

Hatimaye Werrason ameachia single ya kwanza inayokwenda kwa jina la Hono­rable député, Kwa mujibu wa Werrason ambaye alinukuliwa na mtandao maarufu wa Digital Congo anasema kuwa wimbo huo ambao anatumai utapokelewa vizuri na mashabiki ni jembe kwa wanasiasa wa Congo akiwakumbusha ahadi na majukumu yao huku tukielekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini Congo.

Balozi huyo wa amani amewakosoa wanasiasa ambao walitumia muda wao kujilimbikizia mali na sio kufanya kazi walizotakiwa kuzifanya na wananchi waliowachagua.

Wimbo huu umetoka huku kukiwa na biff kati yake na wanaharakati wanaopinga utawala wa Kabila wanaoishi nje ya Congo ambao wamekuwa wakivamia maduka yanayouza CD na DVD mbalimbali za Congo hasa nchini Belgium na Ufaransa.

Werrason yuko mbioni kuachia albamu yake mpya ya Malewa II albamu ambayo inasubiriwa kwa hamu hasa baada ya hasimu wake JB Mpiana kuachia albamu yake ya Soyons Serieuxe ambayo inasemwa kufanya vizuri sokoni.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: