Siasa za Congo zawaathiri wanamuziki Congo.

Leo hapa tuna habari mbaya kwa wapenzi wa muziki wa congo hasusan wapenzi wa Jb Mpiana,Werrason na Koffi.Kama mnavyofahamu nchi ya DR CONGO inaelekea kwenye uchaguzi wake wa pili baada ya ule wa kwanza  mwaka 2006. Kuna kikundi kimezuka katika nchi za ulaya cha vijana wacongomani ambao wanaupinga uongozi wa sasa wa DR CONGO

Chini ya rais JOSEPH KABILA,vijana hao wanajiita Le COMBATTANTS. Vijana hao wamekuwa kero kwa wapenzi wa muziki na hasa wacongo wanaoishi ulaya,wamekua wakiendesha Operation za vurugu dhidi ya wote wanaowahisi kuwa nyuma ya utawala wa rais KABILA wakiwemo wanamuziki, operations hizo wanaziita kwa jina la OPERATION DES COMBATTANTS. Mara ya mwisho moto ulimuwakia Werrason mwanzoni mwa mwaka huu alipokuwa Bruxells, Belgium, vijana hao wahuni walimvamia Le Roi De La Forret akiwa mamejipumzisha kwenye mgahawa wa wacongoman eneo la matongee jijini Bruxells, vurugu kubwa ikazuka na werrason inasemekana alijeruhiwa ila shukrani kwake kwa kuwa na utaalam wa sanaa za mapigano ” martial arts”  ambao ndio ulimsaidia kupambana nao katika kujitetea.

Sasa oparation za wanaharakati hao zimechukua sura mpya kwa vijana hao kuanza kuvamiwa maduka ya muziki huko ulaya na kushinikiza wapewe cd zote zilipo kwenye duka husika za wanamuziki Jb Mpiana, Werrason na Koffi Olomide kwa madai wanamuziki hao wamekuwa wakiutumia umaarufu na ushawishi wao kumsaidia kisiasa rais KABILA ili ashinde uchaguzi ujao wa congo.Vijana hawa imekua ikionekana kama vile wako above the law na hakuna wa kuwazuia kiasi wamekuwa wakifanya uharamia wao huo hadharani tena bila kificho kama mtakavyoona hapo chini kwenye video hiyo walipolivamia moja ya maduka maarufu ya muziki na kuanza kushinikiza wapewe cd husika zote ili wakazi destroy, kiukweli mimi binafsi hii imenikera sana inakuwaje nchi ya ulaya kama Belgium au France ishindwe kukidhibiti kikundi hiki?je nani analifadhili genge hili?maana sidhani kama vijana hao wanaoonekana hapa wanaweza kuwa organized kiasi hiki bila kuwa na mkono wa mtuau watu wazito  nyuma yao.

Mtamuona na kumsikia hapo mwanzo wa video Werrason anavyosikitika na kuwasihi vijana hao wasiwahukumu kwa kumpigia debe Kabila kwani hawakuanza wao toka enzi za Mabutu kina Franco walikua wakiimba nyimbo za kumsifu rais.

All in all hii ya kupora cd na dvd madukani itawaathiri sana wanamuziki husika, kwani hakuna mfanyabiashara ya muziki atakubali kuweka kazi za wasanii hawa kwani itakua ni hasara kwake Le Combattants wakivamia duka lake. Mimi nadhani serikali ya kabila inatakiwa ifanye kitu,iwasiliane na serikali husika France na Belgium kuwadhibiti hawa wanaharakati, walianza kama utani sasa wanaelekea kubaya,na kama utawasikia utaona wanavyojaribu kutishia kwamba kila mahali mcongoman alipo akae mbali na jb,werra na koffi na kazi zao,wanasema wako kila mahali,canada,us ,uk,france,Belgium na nyumbani congo.

 

Issue ni serious wadau,hapa chini wamevamia duka lingine la  luxene Musengi na kumnyanyasa mwenyewe vibaya sana

Advertisements

3 Responses to Siasa za Congo zawaathiri wanamuziki Congo.

  1. Anonymous says:

    hawa jamaa bwana wanaboa sasa…siasa na muziki wapi na wapi,ndio maana siku hizi ziara za wanamuziki huko ulaya zimekua haba

  2. Fatuma Mtanga says:

    huu ni ushenzi mtu unawezaje kuingia dukani kwa mtu na kushinikiza akupe malia anazouza kwa mambo ya siasa?no sijapenda kabisa hii

  3. muddy washington says:

    HAO JAMAA WATAKUWA WASHAMBA HAYO MAMBO YA RAIS ALIYEKO MADARAKANI KUIMBWA MBONA KAWAIDA SANA,TOKA ENZI ZA MOBUTU KINA MZEE FRANCOO WALIKUA WAKIMUIMBA,NDIO INAVOKUA,WAACHE USHENZI WAO KWANZA WANA MAKARATASI HAO KWELI MAANA WANAONEKANA VIPERA TU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: