SIKU ROBERTO EKOKOTA NA ATALAKU MOMBELE WALIPOLIGEUZA JUKWAA LA PAMOJA KATI YA WENGE MUSICA ORIGINAL NA ZAIKO LANGA LANGA NKOLOMBOKA KUWA MPAMBANO WAO BINAFSI.

Na.Hadj Le Jbnique

Kwanza kwa namna ya kipekee kabisa napenda kuchukua nafasi yangu ya thamani kabisa kumshukuru Papaa Farid na mascut kwa kunisaidia kuipata video ya onyesho la pamoja kati ya wenge musica 4×4 tout terrain a.k.a. wenge original ambayo imenipa sababu ya kuandika hapa. Kiukweli hiyo ni show ya kukumbukwa sana miongoni mwa show za wanamuziki wa congo.

Ikumbukwe kwamba kabla ya ujio wa wenge Zaiko langa langa ndani ya Kinshasa ndio bendi iliyokuwa imekamata ikiongoza kwa kupendwa na wakazi wa jiji hilo.Hivyo kishindo cha ujio wa vijana wadogo watanashati wakati huo wenge musica kiliitikisa zkwa kiasi kikubwa zaiko kutokana na wenge kuja na style ya aina ya kipekee kabisa ya upigaji na uimbaji ambayo haikupata kuonekana congo, hali hiyo ikapelekea ushindani mkubwa sana miongoni mwa mashabiki wa hizo bendi mbili,wenge ikiwa na mashabiki wengi wanafunzi na vijana kiujumla huku zaiko ikipendwa na watu wazima  kwa maana za kuanzia miaka 40 na kuendelea.

Kufuatia mabishano hayo ya nani zaidi  kati ya makundi haya mawili mapromota wakaona hiyo ni nafasi nzuri ya kutengeneza pesa,wakawashawishi viongozi wa makundi hayo kwa maana ya JB MPIANA na wenzake kwa upande wa wenge musica na mzee Nyoka Longo kwa upande wa Zaiko langa langa ili bendi hizi zifanye onesho la pamoja, haikuwa kazi rahisi lakini baada ya jitihada kubwa wote wakaafikiana kufanya onesho hilo na sio shindano la nani zaidi,ila mashabiki kama mnavyojua tena wao wakaligeuza kuwa shindano la nani zaidi.

Sitaki kuingia sana juu ya kilichitokea ila kilichodhihirika zaidi siku hiyo ni kama ulikua ni mpambano si wa nani zaidi kati ya wenge na zaiko bali ni nani zaidi kati ya marepa mashuhuri wa bendi hizo mbili ,hapa nawazungumzia “Le Grand Chibuta” ROBERTO  EKOKOTA wa wenge musica na Atalaku MOMBELE wa zaiko langa langa,kiukweli hawa mabwana siku hiyo walitoana jasho na kuwapa mashabiki burudani si kawaida, je nani alimfunika mwenzie? !!jibu tutalipata baada ya kuitazama video hii hapa chini, tazama vizuri huu ulikuwa ni wimbo mzuri sana wa zaiko lakini siku hiyo waliimba kwa pamoja na wenge muzika, ila kwenye sebene ndio vurugu za Ekokota na swahiba wake Mombele zilipoanza, hebu tuicheck hii kitu bomba sana wadau.

7 Responses to SIKU ROBERTO EKOKOTA NA ATALAKU MOMBELE WALIPOLIGEUZA JUKWAA LA PAMOJA KATI YA WENGE MUSICA ORIGINAL NA ZAIKO LANGA LANGA NKOLOMBOKA KUWA MPAMBANO WAO BINAFSI.

 1. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  huo mwimbo unaitwa petit aziza ni wa zaiko langa langa ulikuwa maarufu sana kwetu hapa kigoma enzi hizo kuna redio moja ya congo ilikua inasikika hapa hasa mida ya jioni…basi watu wote walikua hawakosi kusikiliza,nimekumbuka mbali sana,hapo naona ekokota alimfunika repa wa zaiko si unaona washabiki walivokua wakimshangilia akishika kipaza sauti?

 2. mkigoma,kariakoo says:

  kweli kabisa dada mkemimi nakumbuka enzi hizo kigoma jioni..pia unakumbuka miaka hiyo hiyo alijitokeza msanii ambae pia nyimbo zake zilivuma sana kuanzia kigoma badae tz nzima msanii akiitwa Bivons Gato,huyu jamaa alitoa album moja tu na kupotea sikuwahi msikia tena lakini album yake ili hit sana,nani anamkumbuka bivon gato?atupe kumbukumbu ya habari na miziki yake

  • Farid na Muscat says:

   Mangalibi ya leo sisi wote kumujini kunenda kuchezaa,
   wakubwa na wadogo pamoya tunaweka moto kati yetu tutacheza mpaka keshoo, wazee walisemaga kama ukingali na meno vunja mifupaa, kama uko na nguvu ya kucheza michezo cheza yako yotee, tikisa mikono na miguu kisha mwili wako woteee
   hahahahahahahaa Mkigoma umenikumbusha Gato alikua akipendwa sana sehemu za Kigoma Rwanda na Burundi na mwimbo wake maarufu ulikua ukiitwa Azalaki Awa pamoja na Ngoma ya Kwetu

   • Stivin says:

    Gato alivuma kila mahali, alitoa albam nyingine haikupata umaarufu kama ya mwanzo, baada ya hapo akapotea

 3. Mamaa Prezidenti says:

  Mi sio siri namzimikia ile mbaya makaba na ekokota….

 4. Farid na Muscat says:

  Asante sana Pius Mzee
  sisi tupo hapa kwa ajili yako na kwa ajili ya wapenzi wote wa muziki tozaa likoloo patron nangai

 5. peter says:

  ….Bana wengeclan hii ni kwa faida ya mashabiki wa FIKIN,,,kuna upigaji wa solo mbili kwa wakati moja Mi-solo na Solo…wakuu wa uchambuaji Mukubwa Pius,Farid na Muscat , Le Hadj J’QUE …tumwagieni mashabiki maana …..baadhi ya nyimbo toka kwa Jb ukiwa makini na instrumental utasikia watoto wawili (solo)wakijibishana…….inapendeza sana ukiwa mshabiki wa musiki na ukaupenda muziki….Merci mingi wadau wote wa sport starehe …mtandao burudani kabisa….eeeeh sebele sebelee…mozikiye tata …mozikiye mamaa…….

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: