Mustafa Hassanali Kuzindua UHURU collection Africa Fashion Week

 

  • Precision Air kumpeleka Mustafa Hassanali  Afrika Kusini
  • Ni kwa mara ya Nane kwa Mustafa Hassanali kufanya maonyesho nchini Afrika kusini.

image

Mustafa Hassanali akiwa na Manager wa Precission Air – Africa ya Kusini Bw. Ibrahim Bukenya huko Afrika ya Kusini

Ikiwa Tanzania inasherehekea miaka 50 ya UHURU, mbunifu wa kiafrika Mustafa Hassanali’s, atazindua “UHURU” collection ambayo alivutiwa na muonekano wa bendera ya taifa kama iliyopeperushwa Mt Kilimanjaro tarehe 9 Desember 1961 AFI Afrika Fashion Week iliyopo Johannesburg Afrika Kusini.

“Mkusanyiko huo wa mavazi umehusisha maliasili ya Tanzania , Ambao watu wake ni wenye ukaurimu , nchi yenye utajiri wa maliasili za taifa na pia ni nchi iliyojengeka na misingi aloiweka Baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” alisema Mustafa Hassanali

Mkusanyiko huo wa mavazi umepewa jina la UHURU. Na pia haupo tu kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bali uhuru huo kuonyesha uwito, ubunifu na utamaduni.

Kwa kuwa taifa moja, Mkusanyiko huo wa mavazi utaonyesha Amani na utengenezaji wa mavazi hayo yataielezea Tanzania kiundani kupitia mbunifu wake kutoka Tanzania Mustafa Hassanali.

Safari ya Mustafa Hassanali ya Afrika kusini imedhaminiwa na Precision Air, Shirika la ndege lenye ukuaji mkubwa Tanzania ambalo kwa sasa linafanya misafara yake mara 5 kwa wiki kwa misafara ya Johannesburg.

“Tunafarijika kuwa na ushirika na Mustafa Hassanali, ambae atafanya maonyesho ya mkusanyiko wake wa mavazi kwa mara ya nane Afrika kusini. Muungano wetu mpya unaangalia kutangaza biashara,utalii na utamaduni uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. alisema Afisa uhusiano wa Precision air Annette Nkini.

Ikiwa ni mara ya kwanza tena kwa Mustafa Hassanali, Atakuwa ni mbunifu pekee ambae atasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzanian nje ya Tanzania kwa kufanya ufunguzi wa mkusanyiko wake wa Mavazi Afrika kusini.

“Maonyesho ya UHURU collection yatakuwa ni maonyesho yangu ya pili AFI Africa Fashion Week na ya nane kwa jamuhuri ya Afrika kusini, Itakayokuza mahusiano ya pande mbili kati ya Tanzania na Afrika Kusini.” Aliongeza Hassanali

AFI Africa Fashion week inamilikiwa na African Fashion Internationals Dr Precious Moloi, itakayofanyika Sandton Convention Centre kuanzia tarehe 20-22 October. Mustafa Hassanali ndo mbunifu pekee kutoka Tanzania aliealikwa katika wiki ya kujivunia na atafanya maonyesho yake tarehe 22 October saa 10 jioni

KUHUSU MUSTAFA HASSANALI

Mustafa Hassanali ni mbunifu mjasiriamali anaeamini katika ‘daima sitashindwa’ huku akitumia kipaji chake na ubunifu wake wa mavazi katika kuleta maisha bora ya sasa na ya baadae.

Kazi za mbunifu Mustafa zimekuwa zikithaminika na kuonyeshwa kimataifa, ambapo Mustafa alifanikiwa kuonyesha ubunifu wake katika nchi kama Angola ‘Angola Fashion Business’, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Kameruni, Wiki ya Mitindo India 2009, Naomi Campbell’s fashion for relief 2009, Arise Africa Fashion Week 2009, Wiki ya mavazi Durban & Cape town, Vukani Fashion Awards Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival, Sicily, Italia, M’net Face of Africa, Msumbiji, Uganda, na Wiki ya Mitindo Kenya, ambayo kwa pamoja yamemletea heshima kubwa, ndani na nje ya nchi.

Ukikutana na Mustafa Hassanali ndipo utajua uwezo wake utokanao na kazi zake,yeye kama yeye anajiamini katika kila anachokitengeneza na anatumia karama na ubunifu wake kutengeneza kilicho bora leo na hata kesho,hasa katika swala zima la mavazi, kwasababu kila akifanyacho hutoka moyoni. Mustafa ni Fashionista wa kweli ndani na nnje

Kwa habari zaidi tembelea tovuti www.mustafahassanali.net

KUHUSU PRECISION AIR

Shirika la ndege Precision iimefungua matawi yake mapya Johannesburg na Hahaya-Comoros miezi miwili ilopita, tarehe 7th Octoba ilianza kuuza share zake katika Initial Public Offering (IPO) na ikitarajia kukuza Dolla za kimarekani milioni 20 kwa ufungwaji wa IPO tarehe 28th October.

Precision Air ilitambuliwa na African Airlines Association (AFRAA) na Best Scheduled Domestic Airline kama shirika la ndege la mwaka 2010 kutoka Tanzania katika Tanzania Society of Travel Agents (TASOTA) Awards .

Shirika hili la ndege linamtandao mkubwa nnchini ikiwemo; Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar , Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Ukiachana na safari za mikoani shirika hili lina safari zake pia Nairobi , Mombasa , Entebbe , na kwasasa Hahaya na Johannesburg .

Amisa Juma
PR and Media Manager
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)718735167
Networking : www.twitter.com/swahilifashion
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info
www.liveyourdreamstz.com
www.fashion4health.org
www.361.co.tz

3 Responses to Mustafa Hassanali Kuzindua UHURU collection Africa Fashion Week

  1. book it vip says:

    If you can, send me an email and we will discuss because I have an idea you will love. Such a deep answer! A lot of stuff to take into consideration.

  2. numerous great information and facts and inspiration, the two of which I have to have, thanks to supply such a useful facts here.

  3. I unquestionably get pleasure from just about every minor little bit of it and I’ve you bookmarked to check out new stuff of the blog a have to read through site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: