HAKUNA, HAIJAPATA KUTOKEA NA WALA HAITOTOKEA KAMA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN

Leo nimefanikiwa kuipata moja kati ya video bora kabisa ya wenge musica original,kwa kweli nimepata tabu sana kuchagua kipande kipi cha video hiyo nikiweke hapa kwa sababu kila part ya live concert hii bora iliyofanyika huko Brussels , Ubelgiji au ubeleji kama wasemavyo waswahili wengine hususan wa Kigoma ujiji pale, Burundi waswahili wenzangu wa buyenzi pale pamoja na waswahili wenzangu wa congo sehemu za manyema province, Nimeona niwawekee video hii hapo chini ambayo ni just a highlight ya concert hiyo nzima.

Je bendi zetu za sasa hasa za hawa vijana wanaojitoa kwa wakongwe na kuanzisha bendi wana kipi cha kujifunza hapa? Sijui mdau utakua na kipi cha kusema baada ya kuitazama sehemu hii ndogo tu ya concert hiyo,lakini mimi naanza kwa kusema vijana na bendi za sasa zinaweza kujifunza hapa uchangamfu stejini wakati wa kuimba na kucheza, jukwaa la wenge oroginal kama tutajavyoona hapa lilikuwa vijana wa sasa wanaita full shangwe kila mtu analishambulia jukwaa kwa nafasi na style yake, hakuna kusimama kama mti jukwaani eti kisa wewe ni mpiga gitaa,keyboard,tumba,atalaku n.k.kila mtu anafanya kazi yake na kucheza pia,mtazame Makaba, mtazame Didier Masela, mtazame Patient Kusangila n.k. kila mtu amechangamka, tupate video hii angalau kwanza, then kama tutaona kuna ulazima basi concert nzima itawekwa hadharani papa hapa, ni boooonge moja la concert hili wadau mimi na ugonjwa wangu wote kwa wenge musica sikuwahi kuipata video ya concert hii wakati huo.

 

 

Kwa wale waliokuwa wanajadili kuhusu uhalali wa Makaba kama anastahili kuwa nambari one watazame na kusikiliza kuanzia dakika ya 6 na kuendelea kisha mjadala ruksa kuendelea.

Merci Mingi Papaa na The Romantic, Wenge BCBG Die Hard Member. Tuko pamoja kaka.

Advertisements

17 Responses to HAKUNA, HAIJAPATA KUTOKEA NA WALA HAITOTOKEA KAMA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN

 1. Mukubwa Shabani says:

  KAKA SAFARI HII UMEUA…HII NI BALAA SIJAPATA KUONA BIG SHOW KAMA HILI..KWELI ILIKUA FULL SHANGWE…NIMEONA MAUJUZI YA PRINCE MAKABA KAMA ULIVOELEKEZA HAPO KUANZIA DK YA 6 YA HII VIDEO YA PILI,MTU ANAPIGA GITAA ANAKUFURAHISHA MPAKA UNATAMANI UMMEZE MZIMA MZIMA,NAONA MPAKA BLAIZE BULA ILIBIDI AMKABE SHINGONI JINSI ALIVYOKUWA ANAWAPAGAMISA KWA STAGE

  NATAMANI SIKU HIZO ZIRUDI BUT HAIWEZEKANI TENA

 2. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  kaka kaka punguza speed kaka utauwa…du yani unatoa kitu kinaingia kitu utatuover dose bwana lol!yani hata sijui nisemaje wadau hii ni concert nadhani bomba kuliko zote za wenge nilipata kuziona,labda na ile walishindana na zaiko kwenye jukwaa moja,tutafutie ile,niliionaga kitambo nikiwa shule kwa nyumbani kwa marehemu mjomba wangu

  makaba hakutakiwa kuzaliwa kwenye kizazi cha kina jb,alijikuta kimakosa hapo huyu ni wa kizazi cha kina Franco!uwezo wake ulikua mkubwa kupita kiasi kulinganisha na wapiga magita wa kizazi cha kina jb,koffi n.k.

 3. Fatuma Mtanga says:

  Mimi nampenda sana Alain makaba jamani,pia huyo atalaku wao naona aliijua vyema kazi yake,hapo simuoni tutu caludji,vipi hakuwepo?

  • Farid wa Muscat says:

   Mamaa Fatuma umetaja watu wawili ambao hawatasahaulika kwenye ulimwengu wa muziki hata wajukuu zao watakuja simuliwa
   walichokifanya babu zao hao,
   Atalaku uliemtaja ni Roberto Wunda nasikia aliacha kuimba pale alipopata matatizo ya kiafya na katika show hii Tutu Caludji alikua bado hajajiunga na wenge .

  • Stivin says:

   Toutou caludgi aliingia wenge mwaka 1995, albam ya kwanza kushiriki ilikuwa pentagon!

 4. Mwalimu Mkumbe,Muheza,Tanga says:

  Hii ndio wenge bwana,kipindi hicho hata ukisikia wenge wanakuja nchini mtu hata kama uko mkoani ni lazima ujiandae kwa kuchanga pesa,na nchi nzima ilizizima sio siku hizi…mi walikua wananifurahisha wakiamua kushambulia jukwaa ni wanaume watupu na watu mnafurahi kabisa show wa wanaume wa shoka.

 5. Farid wa Muscat says:

  Mmeugusa moyo wangu kwa hii video ambayo haitasahaulika kabisa na mimi mpaka leo naiona kama ni vitu vya maajabu sana kwa hawa watu , hebu tizameni nyie wenyewe mafundi hawa jinsi wanavyopandisha watu mzuka duh , halafu mtazameni Alain Prince Makaba jinsi anavyokung’uta solo na huku yeye mwenyewe akiyarudi magoma yake mwenyewe tena kwa ufundi mkubwa na bila kukosea tena na guitar kalishika utafikiri kabeba mtoto mchanga na yuko anam’bembeleza eeeeh kitu ambacho sijawahi kuona kwa mpiga solo yeyote yule , maana kawaida hawa wapiga Solo ni lazima atulize kichwa kwenye solo ili asikosee lakini kwa Makaba sijui vidole vyake vina ubongo ? au alichanjiwa vidoleni eeeeh wenzangu hebu na nyie nisaidieni kumshangaa kiumbe huyu, halafu pia mtazameni Roberto Wunda anavyopagawisha na mpaka ameondoka wenge hakuacha kusema (tozaa likoloo)na wala si utani walifanya kazi kubwa na ikakubalika dunia nzima na hata ule usemi wao usemao BON CHIC BON GERRE yaani GOOD STYLE GOOD ATTITUDE ni sawa kabisa.
  Merci mingi Papaa Pius umenipatia kweli kweli na hivi naingia katika kabati yangu ili niitoe cd ya show hii kamili niitazame mwanzo mpaka mwisho kwa raaaaaaaha zangu

 6. Anonymous says:

  Those were the days bwana tuacheni utani haitoto kea kama wenge original tutaendelea kulia na kusaga meno lakini wapi haitorudi ile mpaka kiama

 7. Anonymous says:

  mimi hapo kilichonigusa ni hiyo quality ya big sound…yani utafikiri sio live ilivotoka bomba…yote hiyo ni kazi ya makaba kama sound engineer,akiona tofauti akawii kuzima muziki katikati,yeye huwa siku ya show anakuja ukumbini saa saba mchana anaseti mitambo yake halafu anarudi hotelini kuoga ndio anakuja na wenzake,nakumbuka walipokuja dar mara ya mwisho wakiwa pamoja wenge originala alikuja pale diamond jubilee mchana akisindikizwa na jb na blaize bula,akaseti mambo yake wakajaribu kupiga sebene moja aliporidhika hao wakaondoka zao kurudi hotelini akisema mtu asiguse tena hapa,basi ucku walipoingia makaba akakuta diamond sound ikibinda nkoi wanapiga nyimbo za utangulizi weee makaba alichukia sijapata kuona kwa jinsi alivokua mwekundu,ikabidi aanze upya kuseti mitambo kwa lisaa lizima,watu wakaanza kuzomea basi alipimaliza akashika guiter kazi ikaanza alipiga guiter alipiga guiter viti havikukaliza watu walishangilia kila dakika mwishoni kila mtu akataka kupiga nae picha!!!nakumbuka siku hiyo pia makaba alizima mziki kwenda kumnyang’anya mic na kumshusha stejini repea wa diamond sound alain mulumba kashama enzi hizo akiwa juu bongo,kisa alipanda kwenye jukwaa la wenge wakitumbuiza na kuanza kuchomekea rap zake bila ruhusa ya artistic director ambae alikua ni yeye makaba,jamaaalikua mkali kazini acha!

 8. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  kweli sound iko vizuri.kumbe ndio ilivokua siku hiyo hapo dar….i wish ningekuwepo jamani lol!

 9. Stivin says:

  Kipindi hicho Manda Chant Mweusi bado hajajichubua!

 10. Nice facts, fantastic and beneficial style, as share fantastic things with great tips and concepts.

 11. Its my terrific pleasure to visit your blog and to take pleasure in your excellent posts here. I like it a good deal. I can really feel that you just paid considerably attention for anyone articles or blog posts, as all of them make sense and therefore are very valuable.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: