KITU "Remise et reprise" a.k.a Tressor Mputu toka kwa WMMM

Na The Romantic

Hiki ni kitu kingine maridadi sana kwenye album mpya ya maison mere utunzi wake Herritier Watanabe ambacho ni zawadi yake kwa footballer TRESSOR MPUTU wa TP Mazembe. Huyu jamaa ndio yule aliyefuzu majaribio ya kuichezea Arsenal lakini Boss wake Moise Katumbi Chapwe alimgomea na kumuongeza mshahara na kumpa maisha matamu ili achezee TP Mazembe. (Gonga hapa kumjua zaidi)

Msikie mwenyewe watanabe humu akilia.Kama kweli werra kampoteza huyu kijana basi ni masikitiko makubwa sana,maana hii ni lulu.Hebu msikilizeni wenyewe huyu dogo hapo chini,kiukweli binafsi i love this song na sichoki kuusikiliza. Na mimi naitoa zawadi hii kwenu bana sport starehe.

Advertisements

18 Responses to KITU "Remise et reprise" a.k.a Tressor Mputu toka kwa WMMM

 1. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  nimekubali…kazi nzuri sana,kiukweli mputu amekua kama nembo ya soka ya congo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa hivyo anastahili heshima na zawadi nzuri kama hii nahili liwe fundisho kwa bendi na wasanii wetu wa tanzania kiujumla,waige mfano wa wazee kina mbaraka mwishehe kwa kuwaenzi wanamichezo wetu wote sio wanasoka tu palae wanapofanya vizuri kwa kuwatungia nyimbo nzuri kama hii,inatia faraja sana kwa kweli unapoona unathaminiwa kwa mchango wako kwa taifa,fikiria raha gani anayoisikia mputu na wanafamilia wake kiujumla kwa wimbo huu murua….?

 2. Mamaa Prezidenti says:

  wimbo mzuri sana umepangwa ukapangika sauti ya watanabe ni ya dhahabu ya ukweli,hii ni malewa 2 au?

 3. Anonymous says:

  Jamani mi mwenzenu wimbo huu nimeusikiliza mara tano mwanzo mwisho,sehemu iliyonishika ni hapo kwenye acapela ambapo sijui ndio watanabe mwenyewe anaimba peke yake vyombo vimesimama kwa muda..huyu kijana kweli sauti yake inauza,anafanana na fally ipupa

 4. Hadj Le Jbnique says:

  Kwa wasiomfahamu huyo mputu aliyeimbwa hapo ni huyu hapa:

  Full name: Tresor MPUTU

  Place of birth: Kinshasa, DR Congo

  Height: 1.74 m (5 ft 8+1⁄2 in)

  D.O.B: 10 December 1985

  Age: 26

  Position: Striker

  Club: TP Mazembe

 5. PDJ says:

  I gues watu wa lubumbashi nyumbani kwa tp mazembe hii album wataigombea ile mbaya sokoni kwa huu wimbo poa lakini kazi nzuri wmmm

 6. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  wameimba vizuri,hongera kwao.

 7. Presidaa ya kasumbalesa says:

  Kitu kikali sana,nimemuona tressor mputu mwenyewe kwenye video hapo mwanzo akiwa anaendesha benzi,safi sana kaka uko juu kila wakati kwa kutubeep na tuvitu twa hapa na pale kuhusu miziki ya bana congolee

 8. komba says:

  Booonge la wimbo aisee,mimi sio werrasonique lakini hapa kazi imefanyika tuache unazi,werrason sasa inaonekana ameanza kuelewa maana ya muziki ni nini na kuacha vijana watengeneza ma rhumba ya ukweli sio yale makelele ya helikopta sijui operation dragon..huu ndio muziki waukweli,safi sana kijana Heritier,hivi hawa vijana mbona wana vipaji kuliko kina jb,werra,koffi,wazekwa n.k.lakini inakuwaje wakijitoa kwa hao wazee wakisimama peke yao wanashindwa???hii hainiingii akili,nadhani wapenzi wa muziki wa congo na mapromoter wa muziki huo barani africa na popote duniani sasa tubadilike tuache mapenzi kupita kiasi for nothing kwa wakongwe niliowataja hapo juu,tuwape support hawa vijana wanaojitahidi kujikwamua kutokana na unyonyaji wa hawa wazee na kuanzisha bendi zao,wapenzi tununue album zao kwa wingi ili tuwashawishi mapromoter kuwapa kazi hawa vijana kwa kuwalipa kwenye nchi zetu kupiga live shows…sio kila siku wanatuletea watu wa mwaka 47!!!

 9. chemberra says:

  huyu dogo amehama kwa werrason? nipeni uhakika…maana kwa maoni yangu nadhani amewafunika fally na ferre gola…hawamfikii huyu kijana…anaimba kwa hisia na sauti tamu

 10. muddy washington says:

  kweli kabisa dogo yuko juu sana,hebu wadau tuhakikishieni hili la kuhama kwa wenye taarifa za uhakika toka makao makuu ya muziki afrika huko kinshasa

 11. Anonymous says:

  naona mputu mwenyewe ndani ya kitu cha mercedes benz hapo akiwa na mtoto mzuuuuuri kwenye hiyo video,kweli sports starehe mwanzo mwisho kila wakati ni ya kwanza pande hizi za muziki wa “bolingo”

 12. werrasonique wa ukweli says:

  HUU WIMBO NIMEUWEKA KWENYE SIMU YANGU RASMI TOKA JUZI NILIPOUONA HAPA,SASA HIVI MTU AKINIPIGIA SIMU INAITA KWA WIMBO HUU NA KILA MTU ANAULIZA MUZIKI UMEUPATA WAPI HUO,AKUDO HAO NINI???HA HA HAAAAAAAAA

 13. Prince Sab says:

  WENGE MUSICA MAISON MERE ITABAKI PALE PALE HATA KAMA WERRASON AKIONDOKA.

  Prince Sab – Werrasonique.

 14. Didistone says:

  wazee wa zamba playa hebu tuambieni…hivi kuna tatizo gani pale mbona vipaji havikai..je tatizo lipo kwa vijana ama kwa mzee mzima de la forret mwenyewe?mi nilisikitika sana bill alipoondoka,nikalia sana alipoondoka Flamme,juzi kusikia tena watanabe hayupo kundini,nikazimia kabisa..!wats wrong pande zile??????????!au ndio mambo ya “TATA NA BANGO MAPUMBU MALEMBELE” kama alivyopata kusema Bill Clinton..?

 15. Admiring the time and energy you put into your website and in depth information you present. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same old rehashed material. Great read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

 16. I want you to thank to your time of this superb read!

 17. Appreciating the persistence you put into your website and in depth information you offer. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Wonderful read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: