Liberez utunzi wa Sunda Bass wa Wenge BCBG

Kuna tatizo kubwa sana hata kwa Radio station zetu kupiga nyimbo moja tuu toka kwenye Albamu fulani na kufanya nyimbo nyingine zisijulikane kwa wapenzi isipokuwa wale wanaopenda kununu Albamu nzima wakapata bahati ya kuisikiliza.

Nasema hivi kutikana na kasumba yetu ya kusikilizishwa na kutokuwa na utamaduni wa kununua Albamu nzima na wengi wetu tukipendelea Compilation zaidi ambazo zinakuwa na nyimbo zinazoheat kwa wakati huo, hii hupelekea wapenzi kutozijua nyimbo nyingine maana hata ma Dj na watangazaji huigana pindi wanaposikia mwenzao hupiga nyimbo fulani.

Wimbo huu Liberez uko kwenye Albam ya Quel Est Ton Probleme?

ya JB Mpiana na Wenge BCBG umetungwa na Sunda Bass mmoja kati ya wakongwe kwenye vyombo katika bendi ya Wenge BCBG na kuimbwa kwa pamoja na wanamuziki mahiri wa BCBG, utakubaliana nami hizi ni kati ya nyimbo zinazompa JB Mpiana chat kila uchao, kwani wimbo huu bado uko kwenye chat ya miziki ipigwayo sana Redio DRC. Umepigwa kwenye mahadhi ya Rhumba na kuchukua mirindimo ya kizamani, ninachotaka usikilize humu ni mpangilio na muingiliano wa sauti toka kwa vijana wa Baba Daida Mukulu Bin Adam Motto Pamba.

Salamu zangu za kipee kabisa kwa wadau na wasomaji wa habari za Spoti na burudani humu pia kwa heshma na taadhima ziwafikie Mukubwa Batty Mwafrika, PDG MukubwaLing’ande wa SS Ling’ande (nisikutaje we mi nani bwana mnanini bwanaaa), Papaa Six, Big Producer Maghambo Phillipo Baba Martha (tuko pamoja sana tuu huko uliko), Hadj JBnique, Steve BCBG Muzee ya Airport, Richard Malewa, Sadik Tiger umekuwa kimya sana Papaa,  Ali Tandika tajiri mtoto, Juma mlugulu (mtu haishi kwa maji tuu mlugulu wahedi wewe hehehehe), Tameem wa Kibanda Kicheba kwa Semkope, Tom Baba Maya, Roger na Frank parteners in Business, Mengi masimu, Lyimo fundi wangu wa Simu, Ommy guy, Sanja, Ken Sarowiwa, Robby Msemo mzee wa hekima, Obbasanjo Zeno, Bob, Osagyefu Ulimwengu na wadau wote wa UK Gerald Kitima na kati ya Londone, Mzee Khalid kizunguzungu Nzee, Freddy Ndarima, Jordan Kitima Cha Doktaaa!! hehehe , Neema Kiss, Salma Mtambo wangu, Jose Mwasandube CA, Jeff Msangi, Malaysia Jimmy Mlay, Saleem, Kilonzo Noel, Suvereign le grand Pa Mopao Dailoo Dr. Kiiza, Andy, Mwaimu, Mujuni Baba, Jacob Jordaens, Haroun Papito Mbala “Cha Doktaa”, Mkubwa Manyota Baraka na wengineo wote Desa Kiara nzima, mdau wangu tangu utotoni, huwezi kutaja wote ila salamu kwenu kama nimekusau, usijali tuko pamoja. Nwaacha na kibaop Liberez toka kwa JB Mpiana

Usikilize kisha nipe maoni yako.

Merci Mingi

NB: Post hii imerudi kutokana na maombi ya mdau Rahma Msinde wa DRC, NAdhani umefurahi dada Rahma.

Advertisements

11 Responses to Liberez utunzi wa Sunda Bass wa Wenge BCBG

 1. Mshazy says:

  Leo Kaka Pius umesma kweli kuna nyimbo nyingi sana watu hawazijui kwa sababu hazipigwi kwenye maradio zetu
  hii husababisha sisi tusizijue kabisa, mi mwenyewe kuna nyimbo nyingi za Ferre Gola sizisikii radioni kabisa.

  Wakati ule tunaenda Tazara kila mtu aliijua Kidekule kwa vile inapigwa kule lakini sasa hakuna Disco la Mayenu la ukweli.

  Nasubiri kusikia toka kwa Hadji na Sadiq.
  Nampenda sana Ferre Golla huniambii kitu ila kwa marhumba kwakweli Mukulu ananiach sana, Nai miss sana sauti ya Aimelia na Allain Mpella wangekuwepo kitu kingekuwa Bomba sana.
  Heshima yako kaka Pius

 2. Hadj le Jbnique says:

  Kwenye muziki wa ukweli “RHUMBA” Souverain Leadeur ya ba wengee BCBG JB Mpiana hana mpinzani kiukweli ila heshima kwake Ferre Gola,yule kijana anajua muziki sijui kwanini mzee wa “malewa” kakaetu Le Roi De La Forret alimuachia kijana wake huyu,kama mtafutilia mtaona kijana alijaribu kumbadilisha mzee wa malewa na kumfanya apige muziki,hapa naizungumzia album ya kwanza solo ya mzee wa malewa ile KIBUISA MPIPA,Tafuteni album ile halafu muusikilize wimbo mmoja unaitwa “BLANDINE”,Ooh!my God,that was a song,na ilionyesha kumbe mzee wa malewa muziki wa ukweli anaanza kuuweza,mara ghafla nasikia kazinguana na dogo.

 3. Hadj le Jbnique says:

  HAPO TUNAACHEZA TARATIBU EEEH!SIKIA MPINI WA SOLO HUO HA HA HAAA!WATOTO WA “HEAD OFFICE” MMESIKIA HIYOO…..ASANTE SANA PAPAA P,KIBAO SAFI SANA!

 4. Eric Tisho says:

  Kwa hakika Liberez ilipangwa vizuri sana.baba Daida hana mpizani kwa upande wa rhumba.Zakoko anachipuka vizuri sana.

 5. Hadj le Jbnique says:

  Pia itakua si vibaya mkiicheck liberee live on stage ilivyowapawisha bana paris,hapo ndio utauona vizuri uwezo wa kijana Sakoko,yuko juu sana huyu mtu,gonga hapo down kama uko interested,please subiri mpaka ifike sehemu anayoimba sakoko ufurahi na roho yako this week end.

 6. Richard Malewa says:

  Ahaaaa! haya bwana wacheni na nyie mfurahi bwana msije mkaitia nyongo bure nafsi yake.

  Ila kusema ukweli kuna tatizo kubwa sana hapa kwetu siamini kweli kwamba watu hawapendi miziki ya bakurutu.

  Mashabiki bado wengi tu si Dar wala mikoani hata nchi jirani hasa Kenya. Nikiwa Nairobi huwa nafurahi sana ni kama nipo Kin.

  Tuna tatizo kubwa la Promo kwenye Tvs na FM Radios.

  Hii ni Business Idea lakini naiweka hapa mwenye kutaka n aichukue. Hivi kwa nini bendi zetu zinaanza kupiga muziki saa tano za usiku?

  Kwa nini siku kama hii ya ijumaa kusiwe na sehemu kama city centre ya kiustaarabu watu wanatoka makazini wanapata vitu vikali sound quality, hakuna kiingilio, lakini bei za vinywaji na vyakula ndivyo vinachangia, iwe ni katikati ya jiji lakini siyo kwenye casinos saa nne saa tano watu wanarudi zao kupumzika?

  Kwa nini hakuna TV Station ya Mama Afrika ya Muziki wa Kiafrika halisi. No Bongo Fleva, No R&B, no Hip Hop. Ni Rhumba, Sebene, Soukous, Zouk, Muziki wa Dansi. Why hakuna?

  • benny says:

   tazama african beats star tv jumatatu saa 7 kamili mchana live na alhamisi soukouss vibration same time then rekebisha kauli yako

 7. jordan says:

  kazi imesimama si mchezo mukulu mzee pius mikongoti pius

 8. peter says:

  …merci mingi … Hadj le Jbnique nimeburudika sana na libereeee!!!

  Hapa kwetu ma DJ wotee kwenye vituo vya redio na TV na hata kwenye CLUB wana fanya kazi kwa kukariri hawaijui Africa kwanza hata neno FIKIN kwao ni msamiati namaanisha giza(COVERAGE FINYU!!Sababu hawachimbi kwenye mitandao wao wamekalia bongofleva..wangepata darasa hapa SPORT STAREHE kuna mabingwa wa kuchambua….kama akina papa PIUS,Hadj le Jbnique ,Farid nk

  Nawashangaa hata hizi kampuni za bia za hapa kwetu….wenzetu Kin…primus inagawana mapato na wadau….angalia Live zinazo pigwa pale FIKIN…..muda mzuri ….kiingilio buree bia bei powaa ulinzi wakufa mtu…hakanyagwi sisimizi…..wanamziki wako KIKAZI….hakuna usharobaro……KAZI KAZI. moja …TUUUU….KUSHAMBULIA JUKWAAAA…….

  kaka Hadj le Jbnique SAKOKO anafaa kikosi cha kwanza kikubwa ZAIDI anaimba kwa nidhamu sana na yuko kikazi zaidi namkubali dogo….YUKO SIMPLE……

  Sebooooo!!

 9. We stumbled over here coming from a different page and thought I might as well check things out. I like what I see so now i am following you. Look forward to looking at your web page yet again.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: