Mabanga Style, Style mpya ya Kuimbwa inayoshika kasi Congo

 

Mabanga Style ni mtindo ambao kwa sasa umemea kwa kasi ya ajabu kwa wanamuziki wa Congo pale mtu mwenye pesa zake anataka kutungiwa wimbo mbali na kutajwa kama ilivyokuwa hapo awali. Hii imepelekea Albamu nyingi za Wanamuziki maarufu wa Congo kuwa na nyimbo nyingi ndani yake zenye majina ya watu fulani maarufu.

Kuna dadaangu mmoja aliuliza Allain Kutula ni nani ambaye Werrason amemtungia wimbo, Dadangu hilo lisikusumbue sana huyo Alain kutula atakua ni mtu mwenye vijisenti vyake ambae alimlipa werrason ili adedicate mwimbo kwa ajili yake, kinachotokea ambacho mimi naamini kinaushusha hadhi muziki wa congo kwa sasa ni hii mabanga style, ni kama nilivyosema hapo juu, yaani watu wenye pesa kuwalipa wanamuziki wawaimbe, tena ukiona mtu kaimbwa wimbo umepewa jina lake kabisa tofauti na kutajwa tu, ujue amemlipa mtu na pia kalipia gharama za studio za huo mwimbo, wanamuziki wa congo hii wanaipenda sana kwa sasa kwa kuwa inawarahisishia gharama ya kurekodi na pia inawapatia pesa nyingi na kubadilisha maisha yao, unaweza kuamini kijana mdogo kama Abraham Mignon wa BCBG juzi juzi kanunua na anaendesha JAGUAR Car! do u think jb anamlipa kiasi hicho? if u do u’re very wrong, hiyo ni pesa ya mabanga baada ya kumtungia mtu wimbo ndani ya album mpya wa bcbg.

We jaribu kufuatilia album za Jb, Werra, Koffi, Fally n.k.lazima utakuta nyimbo za mabanga, na kwa sasa naona Claudia Sassou (mtoto wa rais wa congo brazzaville) ndio hottest
mabanga maana anaimbwa karibu na kila mwanamuziki, mfano jb kalipwa pesa nyingi sana na huyu mama ikiwemo kununuliwa sports car kwa ajili ya wimbo huu hapa chini.

10 Responses to Mabanga Style, Style mpya ya Kuimbwa inayoshika kasi Congo

 1. peter says:

  MPUNDA…….

 2. peter says:

  ZADIO……

 3. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  Kumbe Claudia aliyeimbwa ni mtoto wa rais wa congo mzee Sassou Nguesso!huyu mzee ana mabinti wazuri sana,mmoja nasikia aliolewa na rais wa GABON enzi hizo marehemu Omar Bongo,Kaka P unayo picha ya huyu mwanadada?naomba uiweke hadharani,na je hii ya dadake kuolewa na rais bongo ni kweli?na kama ni kweli baada ya omari bongo kufariki huyu mama yuko wapi kwa sasa,kati ya Gabon kwa marehemu mumewe na congo brazzaa kwa babake,ni hayo tu kaka,otherwise tunashukuru kwa kazi nzuri,kiukweli spoti starehe imekua kama home page yangu toka niijue kupitia stori ya wenge,mimi ni mmoja wa walioletwa huku na michuzi blog

 4. Mariam says:

  Tafsiri yake ni nini hata kama alitoa mabanga mimi unanikuna sana huu wimbo

 5. Mdau sokomatola,mbeya says:

  unayo video yake?hebu iweke hapa tuusikilize kwanza….

 6. dj papa upanga says:

  toka enzi za wenge original miaka hiyo mambo ya mabanga yalikuwepo japo siku hizi imekua too much,si mnawakumbuka mabanga hawa

  Daddet mpoko-aliimbwa kwenye pentagon na jb n dominguez
  Jose kongolo- aliimbwa sana na wenge
  Tabou fatu top modele- aliiimbwa kwanza jb na baadae fally
  Kayembe Shentembaa-aliimbwa na defao na wengine
  mamaa sagi sharufa-aliimbwa sana
  wapo kibao….hata mbongo mwenzangu ukitaka jamaa wakutungie wimbo kama iko chapaa watakutungia tu,chapaa ya ukweli sio kwenda stejini pale wakija na kuwatunza dola hamsini hamsini kwa fujo,ile ukifanya inakua ni gharama ya kutajwa ukumbini siku hiyo tu,gharama ya kuimbwa ni makubaliano maalum.

 7. mbongo says:

  mbona hamumtaji joseph kusaga..nae ni mabanga wetu hapa bongo si mnakumbukwa aliimbwa na jb kwenye anti terro

 8. PDJ says:

  kumbe ndio ilivyo?mimi kila siku huwa naota nije kuimbwa sio na wabongo hapana bali na wacongo nilikua sijui nifanyeje mpaka nikawa nafikiria nikipata mkwanja wa kutosha nihamie kinshasa,sasa kwishajua ngoja nitafute pesa nitimize ndoto yangu ya kuimbwa mwanamuziki maarufu wa congo

 9. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  naweza kuipata picha ya claudia sassou nimuone jinsi alivyo maana hata fally ipupa alimtungia wimbo huyu mwana dada sijui mwana mama..

 10. Sonia Skufca says:

  Great facts, fantastic and beneficial style and design, as share good things with very good ideas and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: