Bill Clinton alipovamia jukwaa la BCBG

Hii ilikua 2004/2005,Hiki kilikua ni kipindi ambacho uhusiano wa JB Mpiana na Werrason ulikua mbovu,Hapa Bill Clinton alipanda kwenye jukwaa la Wenge BCBG na kumponda bosi wake wa zamani werrason hadharani kwa hiyo rap yake anaposema “tata na bango **** malembele”.Wadau mnaionaje combination ya Bill Clinton na Genta (huyo rapper atalakuwa bcbg)hapo,mnadhani wakifanya kazi pamoja itakuwaje? toa maoni yako, jb anaweza kuyafanyia kazi.

24 Responses to Bill Clinton alipovamia jukwaa la BCBG

 1. Anonymous says:

  na wewe nawe na mambo ya zilipendwa labda hapa siyo kwangu hakuna vitu moto moto zaidi ya kuelezea history! history! history! au wewe kijana wa Kale!

 2. Mariam says:

  Jamani hivi ALAIN KUTULA anayemwimba werrason ndiyo nani pale zaire sijui tafsiri yake nini lakini napenda huu mwimbo mpya wa huyu ngiama werrason.mimi naona bado yumo huyu jamaa.

  • Hadj Le Jbnique says:

   Dadangu hilo lisikusumbue sana huyo Alain kutula atakua ni mtu mwenye vijisenti vyake ambae alimlipa werrason ili adedicate mwimbo kwa ajili yake,kinachotokea ambacho mimi naamini kinaushusha hadhi muziki wa congo kwa sasa ni hii mabanga style,yaani watu wenye pesa kuwalipa wanamuziki wawaimbe,tena ukiona mtu kaimbwa wimbo umepewa jina lake kabisa tofauti na kutajwa tu,ujue amemlipa mtu na pia kalipia gharama za studio za huo mwimbo,wanamuziki wa congo hii wanaipenda sana kwa sasa kwa kuwa inawarahisishia gharama ya kurekodi na pia inawapatia pesa nyingi na kubadilisha maisha yao,unaweza kuamini kijana mdogo kama Abraham Mignon wa bcbg juzi juzi kanunua na anaendesha JAGUAR Car!do u think jb anamlipa kiasi hicho?if u do u’re very wrong,hiyo ni pesa ya mabanga baada ya kumtungia mtu wimbo ndani ya album mpya wa bcbg.We jaribu kufuatilia album za jb,werra,koffi,fally n.k.lazima utakuta nyimbo za mabanga,na kwa sasa naona Claudia Sassou(mtoto wa rais wa congo brazzaville)ndio hottest mabanga maana anaimbwa karibu na kila mwanamuziki,mfano jb kalipwa pesa nyingi sana na huyu mama ikiwemo kununuliwa sports car kwa ajili ya wimbo huu hapa chini.

 3. Anonymous says:

  Wewe anaon wa 6:26 unajua ni kweli kabisa ili habari iwe kwenye ubora unaotakiwa ni lazima iwe relevant na timely. labda ndiyo sera ya mwenye blog hii kupenda mambo ya kale kale. sisi wadau wa bolingo tunataka issues mpya siyo utuambie mambo ya mwongo mmoja yaliyopita. labda huyu jamaa kaanza kuyajua mambo ya akina werrason na jb mpiana siku hizi. watuleteee vitu kama Champion Kutula aliyoimba Fabregas ambaye anasemekana eti amehama bendi na vitu kama hivyo. kama mambo ya zamani tuambie labda werrason ali hit album ya SOLA LA BIEN mpaka ikapata GOLDEN DISK AWARD. Au nani mpaka leo ana kaweka record ya kujaza watu BERCY au ZENITH.

  Haya mambo ya fulani alilala na fulani ndiyo maana ugomvi ukatokea kati ya werrason na kusangila sisi inatusaidia NINI?

  • Quartierlatinique forever says:

   Hee kwa hiyo unataka aweke mambo unayotaka kuyasikia wewe tu!basi itakua kazi kama kila mtu aki demand kama wewe….kumbuka habari ambayo hukuwahi kuipata hata kama ni yake bado ni news!kaka we endelea kufukunyua mambo achana na hawa jamaa waliojifungia kwenye chumba kidogo cha ushabiki mpaka wanashindwa kuwa independent katika kutoa maoni hasa wanapohisi mtu wanayempenda kaguswa….hii wanayo sana mashabiki wa werra na mpiana,watajibeba we tuletee sisi hatuangalii nani ni nani,tunataka kujua habari za wanamuziki wote na anaefanya vizuri tutamsifia akiharibu tunaponda,mbona hawa watetezi wa werrason ulipoweka zile generique mbili za album mpya ya mpiana ile sayons serieux na ya werra malewa 2 hatukuona wakichangia kutoa maoni ipi ni nzuri,leo mapumbu malembele kuwekwa hadharani wanalia lia!

 4. Anonymous says:

  wadau wawili hapo juu mmecheza chini ya kiwango, hivi bila historia kweli utafika unapotaka kwenda?? jamani ya kale ni dhahabu na pili huo ni mtiririko wa mheshimiwa pius wa kutueleza jinsi wenge bcbg ilivyoparaganyika na ndio maana anaelezea hayo ya kale. mbona ameelezea kama Jean Bediel mpiana ametoa album mpya na sinapatikana pia na wakati huo huo akatuwekea clips zake. jamani jamani wadau. wengine tunaburudika na haya mambo. tupo pamoja wote!

 5. peter says:

  Mimi nawashaangaa wadau wanaopinga History!! WENGE BCBG imejengwa kwa history.Mwanzisha topic anamaana kubwa kubwa sana kwamba GENTA ambaye ALIIBULIWA na Mkandarasi ni moto wa kuotea mbali. Kwa Pius ninacho mlaumu anaubaguzi kwa sisi mashabiki wa MAN U……..

 6. Anonymous says:

  Wewe anon wa 8:53 Bill Clinton ni Rais wa Bendi ni ndoto za alinacha kutumbia kwamba eti atahamia Wenge BCBG kwa wakati huu . Ni kupoteza muda bure.

 7. Anonymous says:

  Jb naona hapo kwenye video alikua anafurahia jinsi werrason alivyokuwa anadhalilishwa na huyu kijana,maana kwenye video anaonekana mara kadhaa akimtuma huyo kijana mweupe ambae nadhani Boguys Bompema aende kumng’ata sikio Bill clinton ili arudie hiyo rap yake,na baade jb anaonekana akiicheza na bill style hiyo…..

 8. Anonymous says:

  Lakini tuache utani,huyu dogo Bill ni mkali sana…naona hata tutu kaludji hapo kwenye video kanywea,huyu ndio alikuja kumaliza zama za tutu kaludji kuwa nambari one in congo,maana dogo alikuja na style ya kipekee kabisa,ila ningekuwa na uwezo wa kukutana nae ningemshauri ajiunge na bendi kubwa kama bcbg,quartier latin ama hata bendi ya wazekwa kama si kurudi maison mere,muziki wa congo ni mgumu kwa kijana kusimama peke yake,ameweza fally na ferre kidogo

 9. peter says:

  ….tatizo ni ubcbg na uwerasonikeee …..LAKIN tukiimba KALAY BOING …….WOTE TUPO PAMOJA

 10. Richard MALEWA says:

  Peter umesema kweli kabisa Kalay Boieng ni tunda asilia kabisa la Wenge linalotuunganisha ingawa “Kichwa” Ngiama Makanda alikuja kukiboresha WMMM. Wengi wetu sisi wa Africa Mashariki tulikuja kuijua Wenge Kupitia Kibao hiki na wala siyo Mulolo kama wale wa kule jikoni Kinshasa kama wanavyotamba baadhi ya watu hapa. Na ndipo tulivyokuja mjua Ngiama Werrason ni nani na hasa ilipokuja kutoka ile kitu Surprise Kapangala pamoja na Kinebouge.

  Kusema kweli Wenge ilikuwa ya hawa Majemarali, Werrason, JB Mpiana, Makaba, Blaise Bula, Masela na Domininguez. JB Mpiana alikuwa kama kiongozi wa jukwaa sababu ya uwezo wake wa kuchekesha na style zake za kipndi kile. Lakini Mamula wa Wenge au King Makers walikuwa nyuma yake.

  Lakini Baada ya JB Mpiana kutoka solo na albam ambayo wengi wanaijua kama ndombolo ya solo na baadaye kuja Titanique baada ya utengano na baadaya kidogo TH. Huo ndiyo ukawa mwisho wake.

  Werrason walianza kidogo kidogo kumbuka mtu anayeanza from scratch lakini chuma chake kilikuja kuwa moto na kuwashika kabisa.

  Hebu angalia alivyoanza na Rapide de Intervention na kurudia kibao cha Kalay Boieng na vibao kama PDG Makambo tuliokuwa tunacheza TAZARA kipindin kile mnakumbuka sana.

  Ikaja SOLOLA BIEN niwakumbishie kidogo tu Heli ….Helicopter ..ezaaa …ezaaaa koya .. tulirusha sana mikono na kuzungurusha vichwa……na hiii ALBUM ilishinda GOLD DISK. ndani ya hiii album kulikuwa na vitu kama VITA IMANA, KOFFI AINA. Na asikuambie mtu hapa ndipo hata mapigo ya bendi zetu zikabadilika ikawa siyo tena kama wenge ile ya zamanii angalia wakati Twanga Pepeta wanaanza Kisa cha Mpemba, angalia zile ghani za kina Banza kama Mtaji wa Masikini nguvu zake mwenyewe ninyi wenyewe mtakuwa mashahidi.

  Then kukaja ALBUM murua ya KIBUISA MPIPA, ndani kuna vitu vitamu kama Operations Dragon, BLANDINE, NOSTALGIE. Ukitaka kuijua vizuri hii album Tanzania angalia tuu moko naitwa Lucas Mkenda, Mr. Nice jinsi alivyoishika Africa Mashariki na TAKEO. Lakini ukiangalia kwa makini angalia LIVE WERASSON ZENITH ile ya akina BONGE ( Baby Ndombwe), Watanabee walivyokuwa wakicheza ile Kooooo Kooooo Kooooo koyimbi kooooo! kiuno kinakatwa sideways siyo ile ya kizamani ya kuzungusha bakuli.

  ALBUM ZINGINE Zilikuja kuwashika sana na hata hapa Nyumbani ni SOUS A SOUL .Humu kuna vitu kama ALERTER GENERELALE . ukiitaka kuijua hiii album ni pale Werrason alipolete kitu kipya Kabisa amabayo Muziki mmoja unakuwa na nyimbo kama nne na RAPPERS kama wanne. Hii KITU ilifanya onyesho kubwa ambalo halijawahi kutokea Congo huko Kikwit watu kama 800,000 waihudhuria. Ndiyo maana ika ile concept nimewaacha nyuma KILOMITA 800 wengi wameimba hapa kama akina Bela etc.

  Kuna vit vitamu kama MAYASIKA wengi wameiga hapa kama Stono Musica wakajiita kabisa jina hilo hilo na vingine kama TINDIKA LOKITO iliyosababisha Werrason aachane na hiyo bia kuidhamini na Kuingia bia ya PRIMUS kama ya JB Mpina baada ya mdhamini kumzunguka na kwenda kumpatia hela nyingi Bill Clinton ili kuiharibu WMMM maana alifikiri WMMM ni Bill Clinton kumbe ndiyo akaja kutoweka kabisa kwenye chati kabakia kupiga vichochoroni.

  Werrason Haishiwi MAMBO siku zote analeta MAMBO ninyi wenyewe mashahidi amekuja kutoa TECHNO MALEWA 1. Hata vijana utawasikia wanaimba MALEWA! MALEWA! ni ubunifu mpya wa mirindimo na uchezaji stage show ya bendi zote zinacheza hii style unakuwa kama unatingisha mabega unateremka chini unapanda juu! Ukitaka kuijua ALBAM hiii angalia wazee wa mjini na MATHEMATICS MECHANIQUE AU MAHEMBA! MAHEMBA! MAHEMBA!

  Sasa kuna TECHNO MALEWA 2 ambayo nyote mnaisikia WERRASON ANALETA MAMBOOOO ANALETA MAMBO HEEEEE! LEEEEEE! LEEEEEE! LEEEEEEE! Wazee wa Kizigo Extra Bongo wamenyunyizia kwa rappings zao

  Na sasa kuna kitu kitu Moto kinakuja Sytle yake Kama ya Kuwasha PikiPiki hizi miguu miwili halafu unaambaaa ambaaaa nayo.

  Sasa nani unatasema yupo juuu na bado anazidi kuwashika na amewaacha wenzake kilomita 800,000! Mtaendela na Kalagha Bao zenu ilikuwa hivi ilikuwa vile. Wajanja tunajua wapi tupate Burudani ya Ukweeeeeeeeeeeeeeeeeee…..

  • piusmickys says:

   Richard Malewa nimefurahi kukuta hapa anyway tunakutanaga kule kwa Wacongo kwenye Vibe de Afrique
   Merci Mingi Papaa karibu sana.

  • mgosingwa,muheza T.A. says:

   TATA NA BANGO MAPUMBU MALEMBELE….MAPUMBU MALEMBELE…..aaah mzee wa malewa hii rap unaionaje mbona hujaitaja si ni ya kijana wenu wa zamani

 11. Mpunda Forever says:

  bwana malewa sasa tuko huku…sio titanic wala TH tena,naona unaongea mambo ya zamani,sasa ni mambo ya chamuvumaa…. eeeeh de la Patria eeh…eeeeh de la patria eeeh..liiiibooo…liboko yoyoooo…papaa cheri liboko liboko nzambe.. na hiyo pikipiki yenu ya miti ole wenu msije kuiga style yetu ya kurusha mikono kwenye mpunda,maana naona kama ndio mnakoelekea kuiga kijanja na kubadili jina eti pikipiki!we are watching u guyz this time hatujalala tuko macho,

 12. Richard MALEWA says:

  Sisi si watu wa shari kama unakumbuka vizuri

  tulimwambia Bill Clinton KISANOLA!

  Tunaimba na kufurahi na Baba yetu LE ROI DE LA FORET!

  Pitisha chanuo kwenye sehemu zako zilizofungana NYWELE!

  Kisanola! Kisanola! Kisanola!

 13. mpenda miziki ya bana congo says:

  wadau mtapoteza muda kubishana na watu wa dizaini ya kaka malewa na wale wanaojiita die hard fan wa mpiana,hawa wanashida moja,tatizo wamejifungia katika kachumba kadogo ka ushabiki kupita kiasi kwa wanaowapenda…ushabiki ambao unawafanye wasiwe huru kuona mengine zaidi ya yale ya wanamuamini na kuapa kufa nae,wao kwao hata mtu alietofauti na wanamuamini afanye kitu gani huwa hawaoni,kwanza sidhani hata kama wanapotezaga muda wao kununua ama kusikiliza muziki wa m2 tofauti zaidi ya wanaempenda..wako wengi wa hivi hata kwenye mitandao mingine ya nje huko tunakutana nao.Kiufupi Bill clinton anaijua kazi yake kama tutu caludji enzi zake alivyokua anaijua,lakini hawa jamaa leo wanaweza kuwakataa hawa watu waliowabeba watu wao mpaka pengine wao wakawajua.

  ujumbe wangu kwao:nyie werrasonique na bcbgque fungueni macho,muwe open minded na kutoa maoni independent,msifungwe na ushabiki wa kitoto.

 14. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  mpunda ya bcbg nzuri,nimeikubali inachezeka kirahisi,binafsi nimeshaifanyia mazoezi ya kuicheza,hainisumbui tena,kwa upande wa huyu bwana mdogo bill clinton,hana adabu na amekosa shukurani kwa werrason,hivi wadau mnajua werra alikomtoa huyu kijana?leo hakua m2 wa kumtengenezea rap ya kumtukana eti hana balls!matusi makubwa sana kwa m2 aliyekutoa kimuziki,haya sasa yuko wapi…usitukane wakunga bwana mdogo..utaishia kuvamia majukwaa ya watu hivyo hivyo kupiga deiwaka..wamuangalie mwenzao fally ipupa anavofanikiwa,ni kwa kuwa anaheshimu wakubwa zake kama kina jb,koffi n.k.na mara kadhaa amekua akimhusisha koffi na mafanikio yake

 15. Michele says:

  I like the helpful information you provide in your articles.
  I’ll bookmark your blog and check again here frequently. I’m quite sure I’ll learn lots of new stuff right here! Best of luck for the next!

 16. sdkd3ofdksa online casino eroiuh32hbjsdk casinos online slj2k9fhjkasjudew casino
  online swlkj4jhdfk

 17. a lot of wonderful details and inspiration, both of which I have to have, thanks to supply this kind of a valuable info here.

 18. lots of terrific data and inspiration, the two of which I have to have, thanks to offer you this kind of a helpful details here.

 19. Appreciating the commitment you put into your website and in depth information you provide. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Great read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

 20. Admiring the persistence you put into your website and in depth information you offer. It’s awesome to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed material. Fantastic read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: