DAN FLEVOR, Mganda anayetaka Kolabo na Wabongo!!

September 20, 2011

image

 

msanii kutoka Uganda anaitwa DAN FLEVOR ambae kwa sasa ameamua kuja Tanzania kwa lengo la kutengeneza fan base ya hapa TZ, pia anahitaji kujifunza kiswahili zaidi na kufanya kazi na wasanii wa TZ. Kati ya wasanii ambao Dan Flevor ana mipango ya kufanya nao kazi ni pamoja na Lady Jaydee na Linex. Wimbo huu ni hatua za mwanzo za kutimiza ndoto zake. wimbo umefanywa katika studio ya Tetemesha Recordz ya Mwanza chini ya producer Kid bwoy. Dan Flevor kwa upande wa Tz anasimamiwa kazi zake na Ujazo Entertainment.

 


Mabanga Style, Style mpya ya Kuimbwa inayoshika kasi Congo

September 20, 2011

 

Mabanga Style ni mtindo ambao kwa sasa umemea kwa kasi ya ajabu kwa wanamuziki wa Congo pale mtu mwenye pesa zake anataka kutungiwa wimbo mbali na kutajwa kama ilivyokuwa hapo awali. Hii imepelekea Albamu nyingi za Wanamuziki maarufu wa Congo kuwa na nyimbo nyingi ndani yake zenye majina ya watu fulani maarufu.

Kuna dadaangu mmoja aliuliza Allain Kutula ni nani ambaye Werrason amemtungia wimbo, Dadangu hilo lisikusumbue sana huyo Alain kutula atakua ni mtu mwenye vijisenti vyake ambae alimlipa werrason ili adedicate mwimbo kwa ajili yake, kinachotokea ambacho mimi naamini kinaushusha hadhi muziki wa congo kwa sasa ni hii mabanga style, ni kama nilivyosema hapo juu, yaani watu wenye pesa kuwalipa wanamuziki wawaimbe, tena ukiona mtu kaimbwa wimbo umepewa jina lake kabisa tofauti na kutajwa tu, ujue amemlipa mtu na pia kalipia gharama za studio za huo mwimbo, wanamuziki wa congo hii wanaipenda sana kwa sasa kwa kuwa inawarahisishia gharama ya kurekodi na pia inawapatia pesa nyingi na kubadilisha maisha yao, unaweza kuamini kijana mdogo kama Abraham Mignon wa BCBG juzi juzi kanunua na anaendesha JAGUAR Car! do u think jb anamlipa kiasi hicho? if u do u’re very wrong, hiyo ni pesa ya mabanga baada ya kumtungia mtu wimbo ndani ya album mpya wa bcbg.

We jaribu kufuatilia album za Jb, Werra, Koffi, Fally n.k.lazima utakuta nyimbo za mabanga, na kwa sasa naona Claudia Sassou (mtoto wa rais wa congo brazzaville) ndio hottest
mabanga maana anaimbwa karibu na kila mwanamuziki, mfano jb kalipwa pesa nyingi sana na huyu mama ikiwemo kununuliwa sports car kwa ajili ya wimbo huu hapa chini.


Bill Clinton alipovamia jukwaa la BCBG

September 20, 2011

Hii ilikua 2004/2005,Hiki kilikua ni kipindi ambacho uhusiano wa JB Mpiana na Werrason ulikua mbovu,Hapa Bill Clinton alipanda kwenye jukwaa la Wenge BCBG na kumponda bosi wake wa zamani werrason hadharani kwa hiyo rap yake anaposema “tata na bango **** malembele”.Wadau mnaionaje combination ya Bill Clinton na Genta (huyo rapper atalakuwa bcbg)hapo,mnadhani wakifanya kazi pamoja itakuwaje? toa maoni yako, jb anaweza kuyafanyia kazi.


%d bloggers like this: