Mchango wa Teknohama kwenye Uchaguzi wa 2010

facebook1
Wagombea mbali mbali wakiwa kwenye kurasa zao za Facebook

Na Pius Mikongoti

Kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) kumeiwezesha dunia kuwa kama kijiji, hii imesababishwa na mapinduzi makubwa ya kiteknolojia ambapo habari sasa zinasambaa kwa haraka na uwepesi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Nchi za dunia ya tatu hasa Afrika inasemwa kuwa nyuma kwenye mapinduzi haya kutokana na miundombinu ya kiteknolojia inayosababishwa na umasikini uliopo kwenye nchi hizi.

Hii imepelekea mapinduzi haya ya kiteknolojia kuonekana hasa sehemu za mijini na miji mikuu huku pole pole mapinduzi yakiingia mikoani, wilayani, na hatimaye vijijini.

Uwepo wa makampuni mengi ya kutoa huduma hizi ikiwemo za simu na internet kumeleta ushindani wa kibiashara na kumefanya soko kupanuka na kuongeza watumiaji kwa kiasi kikubwa na huduma hizi kupenya hadi vijijini.

Hapa nitajaribu kuangalia jinsi wagombea walivyoweza kuwafikia wapiga kura wao kwa kutumia Teknolojia hii ya Habari na Mawasiliano hasa kipindi cha kampeni na hatimaye uchaguzi mkuu.

Wakati Kampeni zinaanza niliwahi kuandika juu ya nyenzo hizi za bure chini ya mwamvuli wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) Zinavyoweza kutumika kama njia mbadala wa kuwafikia wagombea na mgombea akafanikiwa. Hatimaye kampeni zimeisha na wapo walioshinda, na wengine kushindwa, si neno kwani kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa.

Leo napenda kuzungumzia jinsi wagombea waliotumia nyenzo hizi kuwafikia wapiga kura wao na kufanikiwa kujenga hoja ambazo zilichambuliwa na nyingine kufanikiwa kubadili mawazo ya wapiga kura wao.

Tutajaribu kumuangalia mmoja mmoja na mchango wa teknolojia hii alivyoutumia.

 

Mh. Rais Mteule Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mheshimiwa Kikwete ambaye alisimama kwa tiketi ya CCM yeye alitumia vizuri sana Mtandao wa kijamii kama Facebook ambapo alikuwa na Account yake na kuwa anawapa wapenzi/washabiki na wanachama wa CCM kile alichofikiria kwa wakati huo ni muafaka kuwaeleza.

Mara nyingi kwenye Status za Dr. Kikwete alikuwa akielezea Sera za CCM na Mafanikio ya miaka yake mitano huku akijiegemeza kwenye Afya, Elimu, Maji na mengineyo ambayo alifikiri ni mahitaji muhimu kwa watanzania.

Akiwa na wafuasi zaidi ya 31,605 kwenye ukurasa wake wa facebook inatosha kuwafikishia ujumbe ambao wao kwa nyakati tofauti wanaweza kuwa wapiga debe wazuri wa hizi sera ambazo yeye alikuwa akizinadi.

Kura 31,605 ni nyingi sana kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wowote ikizingatiwa tofauti ya kura hata moja inatosheleza kumnyima mtu ushindi.

Pamoja na kuwa Busy na shughuli za kujenga serikali yake mfano status yake ya mwisho aliitoa ni kuwashukuru wote kwa ushindi walioupata kupitia ukurasa wake wa facebook, “…Tumeshinda pamoja. Namshukuru kila mmoja kwa nafasi yake kwa kile alichofanya kuhimiza umoja na mshikamano wa kitaifa katika kipindi cha uchaguzi pamoja na ushindi huu.Tuendelee kufanya kazi pamoja,kutimiza yale tuliyoahidi na kupambana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kwa maendeleo ya taifa letu.Asanteni sana.”

Hii inamfanya mtu ajisikie Rais yupo karibu naye na amethamini mchango wake kwa njia moja ama nyingine.

Aidha Dr. kikwete hakusita kuwatuliza mashabiki wake na kuwataka wawe wapole kwenye kipindi ambacho walikuwa wakisubiria matokeo.

“…Huku tukiendelea kuyapokea matokeo ya uchaguzi;popote tulipo kama watanzania tuendelee kufanya kazi kwa bidii tukitambua kuwa shabaha yetu ni kuistawisha Tanzania zaidi.Safari yetu bado ni ngumu lakini ni kazi ya pamoja ambayo tunaweza kufika mahali tunapotaka na haraka zaidi kwa sababu wenzetu wameweza“.

Awali nilijiuliza ni wangapi wanatumia mitandao hii lakini nikagundua kuwa hawa watu elfu 18 kwenye huu mtandao wa facebook tu wanatosha kuwa mabalozi wa Mheshimiwa Kikwete na kumuongezea kura kwa kiasi kikubwa sana.

Mh. Kikwete anajua umuhimu wa hii mitandao na ndio maana akawa na Account ya Tweeter pia ambapo si tu kutoa sera na kuomba kura bali kuna wakati alipokea changamoto kama zilivyo kaririwa na Mtandao wa Global Voice walipokuwa wakifanya tathmini ya mitandao ya kijamii katika uchaguzi, Kama ambavyo mwananchi huyu alivyoonyesha mchango wake kwenye suala zima la CCM kukimbia midahalo na Mh. Kikwete akajibu.

AmbapoKikwete2010 alijibu:

(Mimi binafsi nafikiri CCM kama chama huru kina haki ya kuchagua kishiriki kwenye midahalo ipi na ipi kisishiriki.)

Utaona Rais alijitahidi kwa kiasi gani kujibu hoja si tu za waliomshabikia bali hata waliomchallenge kwa namna moja ama nyingine.

Kampeni za kwenye Mtandao kwa tiketo ya CCM hazikuishia kwa Kikwete tuu bali hata Mgombea mwenza wake Dr. Bilal naye alikuwa na Wavuti wake maalum kuripoti habari zake kila anapopita akinadi sera za CCM na kuwanadi wagombea wa CCM kwa ngazi za Ubunge na MAdiwani gonga hapa kuona.

Dr. Wilbroad Slaa.

“…Ndugu Watanzania nia na malengo yetu kwa taifa vipo palepale kabla na baada ya uchaguzi. Kuna page mpya ya Chadema ikiwa na lengo la kufuatilia na kuratibu halamashauri zote zinazoongozwa na CHADEMA katika kuhakikisha utendaji wake ni wa ufanisi. Tujiunge huko ili kupata fursa ya kutoa mawazo na kukosoa utendaji wa halamashauri hizi. Tuonyeshe mfano wa yale tuliyokuwa

Hii ni status ya Mh. Dr Slaa akiwahabarisha mashabiki.Hakuna research rasmi iliyofanywa ila ukurasa wa Mh. Slaa kweye Facebook unawanachama/Mashabiki 17,230 ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimpa mawazo na mchango wao hasa kipindi cha Kampeni michango ambayo inawezekana kwa namna moja ama nyingine imesaidia kwa mafanikio waliyofikia.

Wagombea wengi wa Chadema walikuwa na Page zao kwenye Wavuti huu wa Facebook na wanachama wao walikuwa wakiwasiliana na kubadilishana mawazo moja kwa moja.

Mfano Fred Saku akishauri chama akisema

“Naomba viongozi wa juu wa chadema kuelewana na kuteua mtu wa kambi ya upinzani bungeni ili kuweka ukumavu wa chama na kuondoa matabaka yanayotaka kutokea. Naomba mtu kutoka kanda nyingine ndio awe kiongozi wa upinzani na siyo kaskazini.” Kama mwanachama ameona kuna haja ya kuondokana na hisia kuwa Chadema ni Chama cha kikanda, hili linaweza kuwa ni tija na likaleta hamasa kwenye chama kwa uongozi pia. Lakini kila mmoja ana mawazo yake kwenye hilo hilo wazo la Saku mwanachama mwenzie

Herbert Mzuyu aliyeonyesha kutoridhishwa nalo akisema “Ukichagua kanda mwisho utachagua na dini na kabila.kikubwa kuepuka ukabulu ni kuteua mtu mwenye vigezo na sifa.”

Michango kama hii ina umuhimu wake kwenye uhai wa Chama na kiukweli kabisa Chama kinahitaji sana michango ya wasomi na vijana ambao kwa kiasi kikubwa ndio wapiga kura.

Vyama vingi vinajitahidi sana kuimarisha jumuiya zao hasa Jumuiya za Vijana. Mfano UVCCM ni moja ya nguzo imara sana za chama tawala huku kwa miaka na chaguzi za karibuni kimeonyesha kutoa msimamo na dira ya Chama kwenye wagombea huku wanachama wake wakijitokeza kuwania majimbo na wamekuwa aggressive sana. Ni wazi kuwa kama chama hakitaimarisha jumuiya yake ya Vijana nafasi ya chama hicho inakuwa finyu sana na vijana ndio watumiaji wakubwa wa mitandao.

Nafasi ya Kampeni za Teknohama kwa Chaguzi zijazo.

Ni wazi kuwa Kampeni zijazo zitakuwa na changamoto kubwa sana huku kampeni za mitandao zikiwa na nafasi kubwa kwani asilimia kubwa ya vijana kwa sasa wana account kwenye hizi wavuti za mitandaoni, wanashiriki midahalo ya kwenye mitandao hasa kizazi hiki cha Teknohama.

Mathalani ukiangalia Uchaguzi wa 2015 watoto ambao kwa sasa wana miaka 14 hadi 17 watakuwa wamefikia umri wa kupiga kura, hawa ni wengi sana na hata vijana walio kwenye umri wa miaka 30 huko bado watakuwa active na wengi wao kwa sasa hasa walioko vyuoni au makazini (wenye elimu) wanatumia Teknohama. Hawa ukiwatumia vizuri wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko na kuleta mageuzi kwenye siasa za majukwaani.

Ni wazi kuwa watumiaji wa mitandao ni wachache na wako mijini, lakini ikumbukwe kuwa kura moja ni Almasi kwenye sanduku la Kura na inaweza kuleta mabadiliko, Kama kwenye chaguzi iliyoisha juzi kuna walishinda kwa tofauti ya kura hamsini hadi elfu mbili au tatu, Fikiria hawa wafasi wa Dr. Slaa kwenye ukurasa wake 17,000 ni machango kiasi gani wametoa kwenye box la kura?

Ninachotaka kusema hapa wengi wa vijana ambao ni wasomi hawapendi kwenda kwenye mikutano ya Kampeni mwisho wa siku wanaishia kulishwa habari zinazoandikwa kwenye magazeti lakini vijana hawa ndio watumiaji wa mitandao hii na Teknolojia hii ya Habari na Mawasiliano, Hivyo basi kama vyama vitaimarisha mitandao yao na kuzitumia hizi Social Networking vizuri vitajenga uhusiano wa kudumu si kipindi cha kampeni tu bali wakati wote ambapo wanachama wenye uwezo wa kuwasiliana nao kwa teknolojia hii waweze kutumika.

mfano Mwana Blog na Mwanaharakati wa muziki wa kizazi kipya Mac Temba anaushauri kwa Mh. Joseph Mbilinyi “

kiukweli wakati mwingine si rahisi kukutana na mgombea lakini kwa njia kama hizi, unweza kumfikia kiongozi wake kirahisi na kuleta imani kwa chama chako na ugombea wako pia.

Matumizi ya SMS

CCM iliongoza kwa kufanya kampeni za Teknohama huku wakitumia kila njia ambayo walifikiri ingewawezesha kunadi sera zao na kushinda.

Hii ilikuwa mara ya kwanza ambapo tulishuhudia hilo. CCM walifanya kampeni za Majukwaani, Nyumba kwa Nyumba hata Kitanda Kwa kitanda kwani kwa kutumia ujumbe wa SMS walisambaza Sera za Chama Chao na kuwahamasisha wanachama na wasio wanachama kumchagua mgombea wao.

Zipo kampuni nyingi ambazo zinatoa huduma ya “Bulk SMS” ambapo unaweza kununua sms kwa idadi, mfano Ose Technology  wao wanachaji sms 100,000 kwa Tsh. 4,000,000/= ikiwa ni sawa na sh. 40 kwa sms.

Ukifanikiwa kutuma sms 100,000 hiyo ni kampeni ya kutosha, kuwafikia watu 100,000 kwa sekunde si mchezo. Kwani hao 100,000 matahalani tuseme nusu yao wameforward sms hizo kwa marafiki zao huoni kuwa hiyo ni njia rahisi sana ya kuwafikia wanachama.

Hizi zilikuwa ni juhudi binafsi za Chama kunadi sera zao na si juhudi za mgombea mmoja mmoja. Hivyo basi kuna haja ya vyama kubadilika na kutumia huduma hizi za Teknohama kwenye kampeni zao.

Blogs

Nia hasa ya WordPress kuanzisha blogs ilikuwa kufungua midomo ya wale ambao walikuwa hawana jukwaa la kuongelea na ndio maana huduma hii ikawa ni bure.

Hivyo wagombea walikuwa na uwezo wa kuwa  na blogs zao ambazo wangeweza kuwafikia wapiga kura wao pasi kutegemea kubebwa na vyombo vya habari ambavyo vingi vilikuwa vikitumia pesa na resources zao binafsi kutujuza yanayojiri kwenye kampeni hizo.

Kulikuwa na ombwe kwenye habari kwani wengi walijikita kwenye wagombea walionekana wana nguvu na kuwaacha wagombea wadogo wakisubiri huruma za wahariri habari na picha zao zitoke mara moja moja.

Hili lingeweza kupunguzwa na wagombea wenyewe kama wangejipanga kutumia vitu kama Blogs kwa ajili ya kuelezea sera na kuwa fahamisha watanzania nini wanafanya kwa wakati huo.

Mathalani pamoja na mambo mengine Mh. Mohamed Dewji (Moe) amekuwa akiitumia Blog yake kwa ajili ya kuwahabarisha wanachama wake nini kinaendelea jimboni kwake.

Halikadhalika ukiingia kwenye Blog ya Zitto na Demokrasia utaona mchango wake kuhusi matukio tofauti na hata habari za uchaguzi ambazo anahisi watu wangependa kuzijua.

Hii inawapa nafasi wafuasi wake kujua nini kinaendelea na nini anawaza kiongozi wetu.

Sio lazima uwe na Blog yako kwani Blog maarufu kama ya Michuzi inatoa nafasi kama unalolote ambalo unafikiri ni la manufaa kwa umma wa Watanzania kuwekwa pale. Hii ni fursa ambayo waliobahatika na kuijua waliitumia, tukubali tukatae hizi Blogs zinamchango mkubwa kwenye siasa zetu ambazo wasomi wananafasi kubwa.

Mitandao kama Facebook, Hi5 na mingineyo ni bure kutumia kama unauwezo tumieni inasaidia ku add value kwa wanachama wenu. Tukubali tusikubali Teknohama ina nafasi kubwa sana kwenye dunia Tandawazi ya leo.

Nikiwa kama mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mifumo ya Mawasiliano nawapongeza wagombea kwa hatua kubwa waliyofanya ya kutumia mitandao hii kuwafikia baadhi ya wapiga kura, kwa namna ya pekee nampongeza Mh. Kikwete, Mh. Slaa na Mbunge wa Chadema Zitto Kabwe ambaye anatumia muda wake wakati mwingine kukaa na kuchat na wanachama wake Online huku akijibu hoja mbali mbali. Ni wazi kuwa kila mtanzania anaoaswa kufikiwa alipo kwa njia tofauti na ndio maana wa vijijini walifatwa na helikopta.

Advertisements

2 Responses to Mchango wa Teknohama kwenye Uchaguzi wa 2010

  1. peter says:

    MIZANI…..

  2. […] pia niligusia jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kuwa chachu ya ushindi. Ukitaka kujua zaidi soma hapa Mchango wa Teknohama/Mitandao Jamii kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 Share this to:ShareFacebookEmailPrintTwitterDiggStumbleUponLike this:LikeBe the first to like this […]

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: