Koffi wa Enzi hizo bana si mchezo

Huyo mrembo anaemshika mkono na pochi ndio George Weah Miley Kunde,msikie suzukii hapo anavyoingia,uzuri wa japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wake toka enzi hizo yuko flexible,akipiga rhumba anapatia akipiga sebene pia anaweza.

 

Msikie tena suzukii na Bouro Mpela hapa,hiki mi nasema ndio kilio kikosi bora kabisa cha koffi na QL kiujumla

na hapachini hizi 3 ni upande wa pili wa koffi, namaanisha sebene, ona mwenyewe, sitii neno tena.

 

Advertisements

14 Responses to Koffi wa Enzi hizo bana si mchezo

 1. mwaikasu,forest, mbeya says:

  kazi nzuri sana kaka,hongera kwa ubunifu,haya mambo yapo kwenye u tube lakini jinsi unavyoyawasilisha na kutuletea hapa inaleta raha ya aina yake kuliko kwenda u-tube kwanza wengine majina ya nyimbo hatuyajui licha ya kuzipenda,kama ungekua na kipindi kwenye redio au tv show ya mambo haya yaelekea ingekua bab kubwa na ya kuigwa bongo sio kama show za kina benny na maimatha…kwenye miti hakuna wajenzi..

 2. Mukubwa Shabani says:

  huyu bwege muziki anaujua sema maringo yake tu ndio yananikera,lakini mkuu nimekukubali pius,video quality imetulia sana no chenga no michirizi,i wish ningekua na video zenye quality kama hii in my library…naona hii ilichukuliwa kwenye master

 3. muddy washington says:

  suzuki 4×4 enzi hizo akiwa kipenzi cha koffi,jamaa alikua juu sana huyu,nakumbuka mara ya mwisho kumuona alikuja hapa bongo na jb mpiana,alifunika sana ukumbini siku ile,ndio maana hata jb alipoenda nae zenith baada ya kutoka hapa ukisikiliza ile live concert ya zenith utamsikisa jb akimwambia suzukii lia kama ulivyolia Dare es salaam bana Paris nao wakusikie…….

 4. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  wamama wa koffi olomide wa zamani walikua warembo sana..mimi nilikua nampenda sana huyo George weah na bonge zina,ambae niliwahi kusikia koffi alizaa nae watoto wawili,sijui kama ni kweli

  • local bar says:

   I would like to say great blog! I just stumbled upon your article. I seriously appreciate individuals that do what you are doing. This is helpful to anyone who reads it. Super helpful info particularly the last part.

 5. Sagudakitemo says:

  Mimi ni mpenzi sana wa jb mpiana,wapi alipo allan mpellla afande sasa hv

 6. MWANA NSUKA says:

  I LUV THIS DUDE KOFFI OLOMIDE JAPO SIPENDI ANAVYOWATREAT WACHEZA SHOW WAKE WA KIKE,ANAWATUMIA KAMA VYOMBO VYA KUMSTAREHESHA!

  OTHERWISE GOOD MUSIC QUALITY VIDEOS.NIME ENJOY A LOT LEO

 7. Hadj Le Jbnique says:

  Alain Mpela “afande” aliondoka wenge bcbg ya jb mpiana mwaka 2003,akaanzisha bendi ya iitwayo GENERATION A,akawaajiri vijana kadhaa wenye vipaji,walipiga concert yao ya kwanza ya uzinduzi Grand Hotel Kinshasa nakumbuka ilikua siku ya wapendanao 14/2/2004.

  Hata hivyo hakufanikiwa sana kutokana na yeye mwenyewe kutaka kushindana na kujilinganisha na wakubwa zake werrason na jb mpiana,hivyo akajiingiza kuishi maisha ya juu kama wakubwa zake hao,akivaa mavazi ya gharama,akiendesha magari ya thamani kama jb na werra wakati kipato chake hakikua cha kutosha kulingana na maisha hayo,matokeo yake wanamuziki wakaanza kumkimbia kutokana na maslahi duni na kukimbilia bendi kubwa mfano,Fabrice alienda maison mere kwa werra,pia miel de son,wengine wakaenda Quartier latin na bcbg.

  Baadae akaenda ulaya kusoma ila kwa sasa amerudi kinshasa nasikia amejiingiza kwenye siasa akitaka kugombea uongozi fulani kwenye uchaguzi ujao wa congo na pia ameanza harakati za kuifufua GENERATION A yake.

 8. flower says:

  Shukrani Kaka Pius yaani hii ni burudani tosha kwa weekend hii.Napenda sana sauti ya Koffi na jinsi anavyoibadilisha badilisha.Na Video zake kwa kweli ni nzuri sana.Na huyu Suzuki yaani nampenda basi tu…Nakutakia weekend njema

 9. Papa kiboko says:

  hiki kilikua kikosi bora kabisa cha wacheza show..sio hivi vitoto vya siku hizi hata nyama havina…hawa walikua wanawake wa kiafrika hasa!!ukiwatizama wanavyomwaga mauno na hii miili lazima mtu mzima haja ndogo ikubane!
  wako wapi hawa wamama siku hizi?

 10. Cherokee says:

  kweli kabisa papa kiboko,yani hizi video mimi zimenibamba kinoma…zimenipa mapumziko mazuri ya weekend na kunikumbusha enzi za silent inn club baada ya diamond sound kumaliza kutumbuiza kwenye saa nane usiku linafuatia disco la masebene mpaka asubuhi!

 11. Anonymous says:

  kuna mcheza show wa koffi alikuaga bonge kuliko wengine nilikua nampenda sana yule mwanadada,nasikia alikua chakula ya mzee koffi,hivi alikua anaitwa nani yule,hapo kwenye video hizo pia yupo

 12. Anonymous says:

  huyo ni mamaa mokonzi ZINA BILAO…ndio alikua kiongozi wa madancer wakike enzi hizo

 13. Might you someday tell us more about thistopic? I really wish you would be my best friend. Thank you for another awesome article. Keep it up.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: