Zulema; Full Kipaji Tatizo “TEJA”

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Kwa sasa yuko na BCBG japo tatizo la dawa za kulevya limeendelea kumuandama hata ukimtazama usoni hapo chini utaligundua hilo.Tazama ataimba baada ya djino kumaliza

Advertisements

27 Responses to Zulema; Full Kipaji Tatizo “TEJA”

 1. MAMA TABU FATOU LA TANZANIANE says:

  Huyu mkaka tall sijui ndio Djino mi nampenda sana jamani sio siri anaimba vizuri sana…hawa ndio vijana jb anafaa awatumie sasa sio wazee kina Rio na kibens,hapa wasimame shai ngenge,huyo teja zulema,Fuji,Bogos bompema na jb mwenyewe

 2. Anonymous says:

  Jb sasa atumie vijana…kumbe ana vijana wazuri namna hii,hao wote walioimba kwenye hii video nilikua siwafahamu licha ya kuipenda bcbg kupita kiasi

 3. Didistone says:

  Zulema yuko juu sana…hebu wadau mfuatilieni hapa atakapoingia kumpokea djino tena,zulema funika bovu,jamani bcbg watakuja lini bongo,wakija wasimuache zulema na mwingine anaitwa sakoko,nae yuko juu sana,

 4. Didistone says:

  utamu wa ” teja” zuri zulema naona hapo juu ulikatika… unaendelea hapa chini

 5. Hadj Le Jbnique says:

  Zulema alitokea kwenye bendi inaitwa WATIKANYA B.T.B.G ya Congo Brazzaville nyumbani kwa Extra Musica,bendi haikufika mbali kutokana na kukosa wafadhili,JPS walijaribu lakini wakacjemka na kuwatelekeza kina zulema Paris wakasambaratika wengine wakarudi kwao Brazzaville zulema akabaki paris na baadhi ya wenzake,SIMON SIPE akasikia habari zao akatafuta awaingize studio,JPS kusikia hivyo wakamchukua haraka ZULEMA na kumkimbizia kwa werrason,JPS NA SIPE ni washindani wakubwa kibiashara na wote ni raia wa cameroon,hapa zulema alikua muimbaji kiongozi na pia ndio alikuwa atalaku mkuu,unaweza kumsikia sauti yake kipindi hicho akiwa fiti kabisa,pumzi ya kutosha na kila kitu

 6. mdau says:

  kaka mshawishini kusaga amlete rafiki yake jb mpiana bongo,long time now toka mwaka juzi tena kwenye club e ambako si wengine hatupata nfasi coz ilikua ni kwa waalikwa tu

 7. komba says:

  kweli huyo zulema anaimba vizuri sana halafu anaonekana mcheshi sana kwa wenzake maana naona kila mtu stejini anacheka akiwa anaimba

 8. mwana paris says:

  katika kumfuatilia huyu zulema leo katika pitapit zangu nimeifuma ACAPELA ya wimbo ZADIO KONGOLO ZK,Nikaipenda nikaona nisiwe mchoyo niwape na wengine tumsikie tena zulema,hii inaonyesha walikua kwenye interview studio

 9. mwana nsuka says:

  merci mingi sina la zaidi.niseme nini tena?

 10. mwajuma zungu says:

  Du!kumbe Zuli Zulema ndio huyu?basi mi niliua nadhania ni msichana flani mshabiki wa jb maana amekua akimtaja taja sana kwenye nyimbo zake.Mkaka kweli ana kipaji,hilo tatizo la madawa ya kulevya linanikumbusha wanamuziki wetu flani wawili wa bendi zetu hapa bongo,nao wako juu sana ila tatizo ni hizo dawa.

 11. John Kisukari says:

  Huyu Zulema hana kitu. Mnamsifia nini mbona hata sauti yake si nzuri? Acheni upuuzi wa kusifia vitu vya kijinga, Zulema si lolote si chochote. Kuna nini hapa zaidi ya kubwia unga?

 12. Anonymous says:

  unga mbali kuimba mbali….

 13. Anonymous says:

  mi nadhani sauti yake sio nyororo lakini nzuri na ina raha yake,ni kama sauti ya werrason,sio nyororo lakini ina mvuto wake,pia ya adolphe dominguez au blaize bula,hazikua laini kama ya jb,aimelia au mpela,lakini walikua wanaimba fresh na kusisimua ndani ya wenge.uteja wake wa unga tuweke pembeni,kipaji yuko nacho

  nawasilisha.

 14. John Kisukari says:

  Labda mnamuonea huruma tu, huyu yanki hana sauti yeyote. Acheni kusifia visivyo sirika jamani. MNAKUWA KAMA Clouds radio kufagilia kitu kisichofagilika?

 15. dj papa upanga says:

  Kaka umesoma vizuri lakini?au umekurupuka tu kucomment,mi mbona sijaona waliposema jamaa ana sauti nzuri?wanasema jamaa ana kipaji,sasa vipaji vipo vya aina nyingi,inaweza kuwa ana kipaji cha kutunga,ana kipaji cha kuimba.Zulema hana sauti nzuri kwa nyie mnaopenda waimbaji wa sauti ya kwanza,lakini anaimba vizuri na ni mtundu wa kuitumia sauti yake hiyo hiyo aliyo nayo.

  Tofautisha kati ya mtu mwenye sauti nzuri na mtu anaeimba vizuri,ni vitu viwili toafauti kaka

 16. Jules says:

  dj Papa Upanga sikia huyo jamaa hapo juu hajakosea ni kweli hata mimi sioni ujuzi ama utundu au hata hicho kipaji alichonacho huyu yanki Zulema zaidi ya kupiga kelele tu mpaka mishipa imetuna. Huu ni mzigo tu kwa Mpiana, Zulema nenda kabwie unga bwana achana na microphone za watu, zina wenyewe hizo!

 17. Fatuma Mtanga says:

  mwenyewe ni nani hasa?nyoshi sauti ya simba au…..

 18. Jules says:

  Sasa si bora sauti ya Nyoshi. Tena basi huyo Zulema hawezi kushindan na yeyote pale Academia katika sauti. Mzigo tu huyo, nenda kabwie kijana kwani hicho ndicho kipaji chako!

 19. Mwalimu Mkumbe,Muheza,Tanga says:

  Hamumfaham zulema nyie ndio maana mnaongea hivyo,mtu ambae alifaulu mitihani ya majaribio kwa werrason na kwa jb leo ukamfananishe na wapiga nyimbo za kukopi hao wacongo wenu wa bongo…si kosa lenu lakini,kwenu nyinyi muimbaji ni lazima awe na sauti kama mwinjuma muumini..au bitchuka wa sikinde ngoma ya ukae,mtu mwenye sauti nzito kama blaize bulla,adolphe,werrason,espe bass wa extra musica kwenu anakua sio muimbaji mzuri!!!!!!

 20. Jarod says:

  Zulema si kitu si chochote ni kelele tu. Msifagilie kitu kisichofagilika, huyo yanki wa hapo juu alikuwa sahihi aliposema mnakuwa kama Clouds radio kufagilia visivyofagilika. Zulema ana sauti gani? Upuuzi tu au kwa kuwa kaimba na Werrason na JB?

 21. voice of tabora says:

  mnakoasea sana ku comment,mbona hamna waliposema ana sauti nzuri?!wanasema ana anaimba vizuri.Ngoja niwaulize kitu,hivi mzee Franco Luambo Makiadi wa TP OK JAZZ alikua na sauti nzuri ama alikua anaimba vizuri tu…msichanganye mambo kwa makusudi wadau,kijana anaimba vizuri,muziki hauwezi kukamilika kwa kuwa na waimbaji wa sauti ya kwanza tu,walikuwepo kina Remmy Ongala,Kina Maxi Bushoke katika muziki wa dansi wa bongo,hawa hawakuwa na sauti nzuri kwa definition yenu ya sauti nzuri ni ile nyembamba lakini walikua wanaimba vizuri.

  Ni hilo tu nilitaka kuliweka sawa,mnaweza kuendelea kubishana.

 22. piusmickys says:

  Ni Mara chache sana huwa napenda kuingilia mijadala lakini Mchangiaji wa mwisho umenifurahisha sana kwani umegusa dhumuni la Post hii hasa kinachoongelewa ni UOMBAJI MZURI na Si SAUTI NZURI unajua Koffi ana Sauti nzuri, hata JB anasauti nzuri na kikubwa kati yao wanajua Kuimba, sasa wapo wanaojua kuimba na hawana sauti nzuri … Endeleeni kubishana

 23. Presidaa ya kasumbalesa says:

  Mu baelezee baelewe baache kutomboka maneno mingi di,mukongo bcbg ni ya libosoo,quartier latin ni ya mibalee,ya misatuu fally Ipupa, wmmm ni ya mine…bana wmmm baache kulobaloba mingi….kwanza werrason aza na maluku ya bana Rwandese…

 24. Neat, book-marked sit down and may present to my personal freinds who also have an itchy vagina.

 25. Thanks for your personal marvelous posting! I definitely enjoyed reading it, you could be a great author.I will remember to bookmark your blog and will eventually come back later in life. I want to encourage yourself to continue your great work, have a nice morning!

 26. I’m really enjoying the theme/design of your blog. Do you ever run into any internet browser compatibility problems? A handful of my blog visitors have complained about my site not working correctly in Explorer but looks great in Safari. Do you have any recommendations to help fix this issue?

 27. Out of my notice, shopping for technology online may be easily expensive, yet there are some guidelines that you can use to obtain the best offers. There are often ways to find discount offers that could make one to buy the best electronic products products at the cheapest prices. Great blog post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: