Nani anaratibu michango ya Majanga?

meli imezama

Imekuwa ni desturi yetu kila kunapotokea maafa kwa watanzania sehemu mbalimbali kuchangia walipatwa na janga, huu ni utaratibu mzuri hasa ikizingatiwa bajeti za serikali zetu huwa ni haba.

Nachelea kusema kuwa kila mara kunapotokea hili huwa nakuwa na wasiwasi kwani kuna ambao wanaweza kutumia nafasi hii kujitajirisha kutokana na misaada hii. Utaguna lakini huu ni ukweli usiopingika jamani haya yametokea na yanatokea kwani kwenye mengi kuna mengi.

Kungeanzishwa utaratibu ambapo idara ya maafa ikawa inaratibu hii michango/harambee kwa ajili ya janga lolote, ni rahisi ku monitor mathalani inayoendeshwa na makampuni ya simu kwa sababu ya Technology lakini wengine si rahisi, Mfano nani anaweza kuangalia na ku verify mapato yaliyoko Bank ambapo zimeingizwa moja kwa moja kwenye account husika.

Tungetegemea mwisho wa siku tuambie pesa zilizochangwa na waliochanga na kiasi kilichochangwa, inatia moyo kusikia mathalani Vodacom kupitia Red Alert namba yao wamechanga kiasi fulani nami kama mchangiaji najisikia vizuri. Chukueni hii kama changamoto na amini nakwambia katika dunia ya leo yote yanawezekana.

Advertisements

2 Responses to Nani anaratibu michango ya Majanga?

  1. Issa Mahmoud says:

    KAka umesema kweli kabisa watu watajinufaisha bureee

  2. Jestine Kelm says:

    Great information and facts, excellent and precious style, as share fantastic stuff with very good strategies and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: