LES MARQUIS DE MAISON MERE BENDI ILIYODUMU KWA MUDA MFUPI KULIKO ZOTE CONGO

Huu ni muendelezo wa Mfululizo wa Story yetu ya Sababu rasmi za kuvunjika kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya Werrason na JB Mpiana hii ni Sehemu ya VI

image

Baada ya kuitazama Wenge Maison Mere jinsi ilivyoanza mpaka kufikia kilele cha mafanikio licha ya kukimbiwa na waanzilishi wake wakuu wawili kati ya watatu nikiwa na maana ya kuondoka kwa “Le FondateurDIDIER MASELA na “Tata Mobitch Le Grand Sapeur Mokonzi ya Ba Wenge Tonya tonyaADOLPHE DOMINGUEZ, Leo tutazungumzia kuondoka kwa style ya uasi kwa wanamuziki wa kutegemewa ndani ya Wenge Maison Mere ya kwake “Le Roi De La Forret” Werrason na kuzaliwa kwa LE MARQUIS DE MAISON MERE bendi ambayo hata hivyo licha ya kuanza vizuri kwa kishindo haikufika mbali, kwanini? twende pamoja tutajua hapa hapa.

 

Ferre Golla Avujisha Siri ya Kikao cha Mapinduzi

Vuguvugu la kuzaliwa kwa bendi hii (Les Marquis De La Maison Mere) linaanzia mwaka 2001 kipindi ambacho bendi yake mama yani Wenge Musica Maison Mere  ilipopata kazi ya kupiga show ndani ya ukumbi wa Bercy huko Paris show ambayo ambayo tuliizungumzia huko nyuma. Mara baada ya show hiyo kumalizika kukajitokeza manung’uniko ya hapa na pale miongoni mwa wanamuziki wa bendi hiyo (WMMM) wakilalamikia kutolipwa kutokana na show hiyo, wakidai pesa pekee waliyopata ni dola 50 za kimarekani ambazo walipewa kabla ya show husika. Kutokana na manung’uniko hayo BABY NDOMBE akawakaza wenzake kitako kuwasomesha nini cha kufanya waweze kujikwamua na kuondokana na unyonyaji huo waliokuwa wakifanyiwa na uongozi wa bendi na hatimaye waweze kupata malipo yanayoendana na mchango wanaoutoa ndani ya bendi na kuifanya bendi iwe juu. Wajumbe katika kikao hicho walikua ni BABY NDOMBE mwenyewe kama mwenyekiti wa kikao, JAPONAIS, BILL CLINTON, CELEO, FLAMME KAPAYA, JDT na MIMICHE. Katika kikao hicho ndipo BABY NDOMBE akalitoa wazo la kuanzisha bendi yao ili weweze kujitawala, wote wakawa wamekubaliana na wazo hilo na JDT ndio akapendekeza jina, akasema Bendi yao hiyo mpya waiite LES MARQUIS, jina ambalo pia liliungwa mkono na wote kikaoni na kikao kikawa kimefungwa kwa kukubaliana waanze kuiuza idea yao hiyo kwa wafadhili mbalimbali. Kwa bahati mbaya siri za mazungumzo hayo zikavuja, yote yaliyozungumzwa katika kikao hicho yakadakwa na mfuasi mtiifu wa WERRASON wakati huo FERRE GOLA ambae alimfikishia taarifa WERRASON. Je baada ya DE LA FORRET WERRASON kufikishiwiwa ujumbe huo wa uasi kundini mwake alichukua hatua gani dhidi ya vijana wake hao waasi? je aliwafukuza? twende pamoja hapo chini.

 

Werra awaangukia vijana wake na kufanikisha Zenith Concert

Werrason and WMMM Live in Zenith

Wakati huo Werra akiletewa habari hizo ikumbukwe album yake binafsi ile ya KIBUISA MPIPA ndio ilikua iko mbioni kuanza kurekodiwa,Hivyo baada ya kupata taarifa hizo za uasi kwenye jeshi lake toka kwa mwanajeshi mtiifu kwake FERRE GOLA, Mzee mzima WERRASON akawa na options mbili tu; option ya kwanza  asimame kiume na kuchukua “uamuzi mgumu” wa kuwasimamisha washiriki wote wa kikao hicho “haramu” cha uasi na kuiweka KIBUISA MPIPA yake rehani au ajishushe chini kwao na kujaribu kuwabembeleza kwa kuwa walikua tayari wamemshika pabaya. Hapa WERRASON akaonyesha ukomavu wa uongozi na busara za hali ya juu, akachagua option namba mbili, akaamua kujishusha chini na kuwabembeleza akiwaahidi magari na wengine nyumba.Baada ya makubaliano hayo wakarudi Paris kufanya kazi ya kurekodi KIBUISA MPIPA. Mambo yakatulia kidogo; lakini mwaka 2002 wakati wa ile concert maarufu ya WERRASON Zenith licha ya kupiga Double vijana hawakulipwa stahili zao inavyopaswa, chokochoko zikaanza tena, lakini WERRA akashtuka akazituliza kiaina japo manung’uniko yaliendelea chini chini.

 

Baby Ndombe asimamishwa WMMM kwa uasi na kuhudhuria sherehe ya JB Mpiana

imageMwaka 2004 wakati wa tour nyingine ya wenge maison mere ulaya, kikafanyika kikao kingine haramu cha uasi kikilalamikia tatizo lilelile la maslahi duni kwa wanamuziki licha ya kujitoa sana kwao kwa ajili ya bendi. Ikumbukwe adha na shida zote hizi walizokuwa wakizipata wanamuziki wengine hazikumhusu kabisa FERRE GOLA kwa kuwa yeye alikua bwana mkubwa pale kwenye bendi, alikua Chef  D’Orchestre hivyo alikua na advantages kuliko wenzake ndio maana alikua mbali na uasi mara zote. Katika kikao hiki cha uasi cha mwaka 2004 muasisi wa uasi BABY NDOMBE safari hii hakuwepo kwa sababu wenzake wakisafiri kwenda ulaya kwa ajili ya tour hii ya ulaya ya mwaka 2004 yeye  alibaki nyumbani KINSHASA kwa kuwa alikua amesimamishwa kwanza kwa kujaribu kuanzisha uasi ule wa mwaka 2001 na pili alikwenda kuhudhuria sherehe ya J.B. MPIANA; hapa pia ikumbukwe kuwa hali ya mahusiano kati ya J.B.MPIANA na WERRASON kabla ya mwaka 2005 ilikua mbaya sana, hivyo kitendo cha BABY kuhudhuria sherehe hizo kilionekana ni usaliti mkubwa sana kwa WERRA. Kwa hiyo kikao hicho cha 2004 huko Paris kilihudhuriwa na wajumbe BILL CLINTON, FLAMME KAPAYA na MIMICHE ambao walikua tayari kuondoka MAISON MERE ya WERRASON, Mwanamuziki mwingine PAPY KAKOL licha ya kushawishiwa sana na BILL akakataa kuungana nao kutokana na kusoma alama za nyakati na kujua hii inaweza kuwa nafasi nzuri kwake kuukwaa u Chef D’Orchestre kutokana na mabadiliko ya uongozi yakayofanywa na WERRA baada ya FLAMME kuondoka.Lakini bahati nzuri kwa WERRASON taarifa za kikao hiki nazo zikavuja, marafiki zake wakampelekea taarifa kwamba  BILL na wenzake wako mbioni kutimka kundini, WERRA akawafuata na kuwabembeleza lakini safari hii akawapata  CELEO na FLAMME KAPAYA tu ,akamuahidi CELEO atamnunulia JAGUAR na FLAMME KAPAYA akaahidiwa nyumba tena (ahadi ambazo hakuna hata moja iliyokuja kutekelezwa na ndio ikaja kuwa moja ya sababu ya Flamme kapaya  kuondoka, pia zipo sababu nyingine za flamme kutimka hapa sio mahali pake).

 

Werra amnunulia Celeo Genereta ili abaki WMMM

image

DIDI KINUANI nae katika kuongeza ushawishi kwa CELEO na waimbaji wengine kundini wakati huo kama AIMELIA, HERITIER, JITROIS na wengine wote akawapatia kiasi kikubwa cha pesa ili wasishawishike kujiunga na waasi kina BILL CLINTON ambae alikua na hasira pia kwa sababu ya TINDIKA LOKITO ambayo yeye na CELEO waliitunga. Werra ili kumdhiti zaidi CELEO asiondoke na TINDIKA LOKITO kumfuata BILL wakaifanye kwenye bendi mpya akamnunulia Generator kwa ajili ya umeme ambao unashida sana Congo kama Bongo. Ferre Gola wakati huo alikua anaishi Paris Ufaransa baada ya kufanikiwa kupata makaratasi baada ya kuoa Mfaransa na huku hali ya mahusiano kati yake na WERRA ilishaanza kulegalega.

Hivyo basi wakiwa huko huko Paris kina BILL CLINTON wakamshawishi FERRE waanzishe nae bendi, kikao kikafanyika kati ya FERRE, BILL, MIMICHE, JAPONAIS na JDT wakimjumuisha pia SERGE MABIALA aliyekuwa amejichimbia Ulaya akihofia kuuwawa kama akirudi KINSHASA kutoka na watu wenye hasira waliokuwa wakimsubiri atie mguu KIN kutokana na kumuua rafiki yao kwenye ajali ya gari! mambo ya Congo hayo, nadhani bana congo mnaelewa vizuri hapa. Je nini kiliafikiwa mwisho wa kikao hicho? je Ferre alikubali kujiunga nao kina BILL kuanzisha bendi? tutajua.

12 Responses to LES MARQUIS DE MAISON MERE BENDI ILIYODUMU KWA MUDA MFUPI KULIKO ZOTE CONGO

 1. Mamaa President says:

  H
  Hee!makubwa……yani werrason ndio alikua akiwachezeaa hawa vijana kiasi hicho licha ya kazi nzuri waliyokuwa wakimfanyia!pesa bwana..

 2. Jules Suley says:

  Hii kitu ipo sana Congo. JB, Kofi Olomide, Nyoka Longo, na Papa Wemba wote wanafanya hivi kwa wana muziki wao. Ila kiboko ni Kofi kati ya wote hao maana yeye ulala na wacheza show wake na asiye wataka anawaambia wajiuze wapate pesa na wakipata wanampa Koffi kisha yeye anawagawia posho ya kujiuza. Congo hiyoo!

 3. Mukubwa Shabani says:

  Lakini werrason kwenye mambo ya pesa anakuwaga na shida sana jb mpiana kipindi cha wenge musica walikua wanakwaruzana nae sana kuhusu kuwapiga panga wanamuziki wadogo kwenye bendi kwa kuwa yeye werrason ndio alikua mkuu wa masuala ya fedha pale,sometimes ilikua inabidi jb atoe pesa zake kuwapa wanamuziki ambao walikua wanaona ni rahisi zaidi kuongea na jb mambo ya pesa akawaelewa na kuwafikishia ujumbe kwa werrason

 4. MAMA TABU FATOU LA TANZANIANE says:

  masikini baby ndombe kumbe ndio yaliyomkuta hayo!wa2 roho mbaya tu sasa kwanini walizuia passport yake kama walikua hawana shida nae si wangemuacha aende zake ulaya werrason ana roho mbaya sana ndio wanadai sio mcongo ni mnyarwanda !

 5. mpenda miziki ya bana congo says:

  Flamme kapaya yuko wapi siku hizi,nasikia aliondoka maison mere lakini sijui yuko wapi na anafanya nini kwa sasa naamini kupitia mtandao huu ndio naweza kupata jibu la swali hili…

  Ushauri:nadhani sasa umefika wakati kwa redio stations zetu hapa bongo zitafute watu waliobobea katika muziki huu wa bana congo na kuwaajiri wafanya kazi kama inayofanyika hapa ya kupasha habari kama hizi ambazo watu wana kiu nazo…ushauri huu kwanza naupeleka clouds fm kwa mh.joseph kusaga,najua yeye ni mdau wa muziki wa congo na bila shaka anapita pita humu…yani ukiacha zuberi msabaha wa radio free africa na kipindi chake cha bolingo time hakuna redio au tv station unaweza kupata habari hizi,sofia kessy alijaribu kidogo kipindi cha bambataa,bora hata enzi za amina chifupa alikua angalau anajitahidi japo si kama hapa kwako kaka

 6. Jules Suley says:

  Clouds ni radio feki hata radio free africa bora hata redio one, kwani zote hizi nilizozitaja hapo juu wao kazi yako kutuwekea nyimbo za kizungu tu ama fleva isiyo na kichwa wala miguu li mradi tu dj kapata 20,000 ya mwanamuziki basi anampigia wimbo wake redioni asikike na kuua muziki wenye ujumbe wa uhakika. To hell with Bongo radios. Bongo mnapitwa hata na wanyarwanda redioni? Wanyarwanda wanaweka nyimbo zao za asili ili ziwafikie diaspora nyie mnaweka nyimbo za nje (90 %) wakati nchi yenu wanaongea kizungu ni asilimia 1 na nusu, si haibu hii? Haibu kweli.

  • Fatuma mtanga says:

   Naunga mkono hoja kwa aslimia mia moja….uncle kusaga sikia hii

   • John Kisukari says:

    Kumbe kuna watu wanaoona hii kitu? Mi nilifikiri ni mimi tu naona kuwa Clouds na redio nyingi za Bongo ni za kipuuzi. How the hell unaweka ama kupiga nyimbo za kizungu 90% redioni? Hata fleva is rubbish, sisemi hivi kwa kuwa mi ni mpenzi wa nyimbo/muziki wetu wa asili ila kwa kweli fleva inaboa na haina radha yeyote. Uncle Kusaga sikia: Utakapozidi kuweka ama kuajili feki presenters redioni ujue you are doomed to kill your redio station. Ajili presenters wenye kujua kazi yao.

   • Anonymous says:

    namimi naongezea hii,kwa sisi wapenzi wa nyimbo za kiafrika uncle kusaga ajue alituumiza sana kwa kuichakachua africa bambataa,popote alipo asikie kilio hiki japo hatuna la kumfanya kwa kuwa ni redio yake ila tunajaribu kuonyesha hisia zetu tu kwa kuwa we are people na wao wanajiita the people station,watusikilize kilio chetu,tuko tayari kushiriki kushauriana nae jinsi ya kuanzisha kipindi bora kabisa tanzania cha muziki wa kiafrika na tunamuhakikishia kitapata sponsors mpaka mpaka wengine atawakataa,mbona ni kazi rahisi

 7. Old Persian says:

  Thanks for sharing your thoughts on thermel. Regards

 8. Eric bed'af says:

  Nashukuru RFA
  Ila masolo iliyo hapa congo siku hizi niya FALLY IPUPA. mimi ni eric bed’af wa hapa congo kivu, kamituga.

 9. I do accept as true with all the ideas you’ve introduced in your post.
  They’re very convincing and can definitely work.

  Still, the posts are very brief for beginners. May jhst
  you please lengthen them a bit from subsequent time? Thanks for the post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: