Waliomteka baba yake Obi watoa madai yao

Wateka nyara waliomchukua baba wa mchezaji wa Chelsea Jon Obi Mikel wametoa madai ya kutaka ‘kiasi kikubwa’ cha fedha za kikombozi, amethibitisa wakala wa mchezaji huyo.

Mikel

John Obi Mikel (kushoto) akiwa na Michael Essien

Lakini wakala huyo, kampuni ya SEM imekanusha taarifa kutoka kwa polisi wa Nigeria waliosema kiasi hicho ni naira milioni 20, takriban pauni elfu 80.

“Madai ya kiasi kikubwa yametolewa, lakini kwa sababu za kiusalama, hatuwezi kusema,” imesema kampuni hiyo kupitia taarifa iliyotoa.

Michael Obi, ambaye ana kampuni ya usafirishaji mjini Jos, hajaonekana tangu siku ya Ijumaa.

“Tunathibitisha kuwa Michael Obi ametekwa nyara, na kuwa waliomteka wamewasiliana na familia na wawakilishi wa familia na kuwa majadiliano ya kuachiliwa kwake yameanza,” imesema taarifa hiyo.

Siku ya Jumanne, familia ya Obi ilipigiwa simu mara mbili na wateka nyara ambao walisema Michael amepelekwa Lagos.

Waliwasiliana na familia hiyo tena siku ya Jumatano ili kuwasilisha madai ya kikombozi, lakini polisi hawajasema kuhusu majadiliano zaidi yanayofanyika.

Advertisements

One Response to Waliomteka baba yake Obi watoa madai yao

  1. The problems which u have discussed in this article is very much common nowadays . Thank You so much for giving me the tips

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: