TRA Jipangeni kwenye mziki tunapoteza

imageNafatilia sana mambo ya Burudani sana tuu na kwa takribani wiki mbili sasa habari za Msama kukamata wezi wa kazi za wasanii zimekuwa zikivuka kila uchao na vifaa kadha kukamatwa.

Ukiangalia zile kazi mfano zile zilizokamtwa huko Mambibo zilikuwa na thamani ya Milioni 24. Ni kweli kazi zile zilikuwa na thamani hiyo lakini je unajua ni ngapi ambazo zimeshaingia sokoni mpaka sasa.?

Mi nalaumu mfumo mzima wa soko la kazi za wasanii na hasa wasambazaji ambao wamekuwa wakilalamikiwa pia kuwa wananyonya wasanii. Lakini kwa hili naomba niwe specific kabisa kuwa nawalaumu TRA ambao wametufikisha hapa tulipo.

Unaweza jiuliza kwa nini TRA? Sinahakika na kodi inayokusanywa toka kwenye mauzo ya kazi za wasanii lakini nahisi TRA wangevalia njuga na kutengeneza sticker maalumu ambazo zitabandikwa kwenye kila CD inayouzwa ingelikuwa rahisi kujua ni copy ngapy zimeuzwa, pia kazi ya Msama ingelikuwa rahisi kwani angekuwa akiangalia sticker ya TRA na kwenye hili hata TRA wenyewe wangewasaidia Cosota na akina Msama katika kupambana na wezi hawa.

Kwa mtindo wa sasa si msanii wala TRA ambao wanauhakika na pato ambalo wanaambiwa ndio lililopatikana na wasambazaji, kwani si mimi wala msanii ambaye anakuwepo pale anapoambiwa kuwa albamu yako tumeuza nakala elfu moja tuu hivyo kwa kuwa mikataba inasainiwa na hawa wanamuziki wanachukua advance kabisa mara nyingi wakishachukua hutokemea na kuanza kujirusha wakifurahia mavuno, wakirudi baada ya wiki huambiwa tumeaza nakala 200 una saini unakula chako unatambaa.

Kwa mfumo huu sanaa itakufa kwani mfumo huu unatoa mwanya kwa watu wachache kujitajirisha badala ya wasanii wenyewe. Hili halihitaji kwenda nje kujifunza ni mikakati na uamuzi kama limewezekana kwenye pombe kwanini kwenye hili lisiwezekane?

Kiukweli hii ni njia rahisi na maridhawa ya kutatua matatizo kwenye industry hii hasa suala la usambazaji, Kipato kwa msanii, na kipato kwa Taifa (TRA).

Huu ni mtazamo wangu baada ya kujiuliza njia ambazo tunaweza kuzitumia ili walao wasanii waweze kufaidi pesa zao.

Ni mtazamo tuu

One Response to TRA Jipangeni kwenye mziki tunapoteza

  1. Hello! This is my first visit to your blog! We are a team of volunteers and starting a new initiative in a community in the same niche. Your blog provided us useful information to work on. You have done a marvellous job!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: