TAMKO RASMI KUTOKA KWA RUGE MUTAHABA KUHUSU MBUNGE WA MBEYA MJINI-CHADEMA MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI (MR II)

imageLeo asubuhi mida flani kati ya saa tano na saa sita, Tanzania imeshuhudia kitendo ambacho kwa mtazamo wangu na kwa jinsi ninavyo elewa na ninavyo heshimu bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania….ni kitu ambacho tukikifungia macho, basi tutakuwa tunaruhusu bunge hili kutumukia kama sehemu ya watu kumalizia matatizo yao binafsi na watu au kundi la watu….
Itafika mahali, mbunge wa Bunge letu akiwa na chuki zake binafsi tu akaamua kutumia jukwaa alilopewa kumuanzishia kashfa yeyote ile kwa hata muuza machungwa wa kibanda ambacho hakipendi kila siku, hadi mwisho wa siku watu wakaanza kuamini hizo kashfa na ghafla uongo ukaanza kufanana na ukweli. Hayo unategemea yatafanywa na wahuni, watu wanafiki lakini sio wabunge wetu.
Hapa nazungumzia kitendo cha mbunge wa mbeya mjini bwana j mbilinyi kuchukua nafasi yake kama mbunge ndani ya bunge hili kuikashifu kampuni ya clouds media, asasi isiyo ya kiserekali ya tht na kwa kiwango kikubwa na katika hali ya kusikitisha, kunikashfu mimi binafsi….
Naomba ieleweke kwamba mimi kama mimi, sina tatizo lolote na kashfa ambazo bwana mbilinyi amekuwa akizilimbikiza kwangu kwa kuwa kwanza licha ya ubunge wake, sugu ni mdogo wangu na daima kaka huwa ana busara pale ambapo inonekana mdogo wake anatoka nje ya mstari….cha pili, style yake ya kutolea kashfa zake kwa kutumia matusi kwenye facebook, kurekodi cd zenye matusi, kutishana kwenye blogs sio style yangu. Angeweza kuweka hoja mezani, kwa sababu wote ni Watanzania ningezijibu ila kwa style hiyo nikijibu na mimi narudi kwenye level hiyo ya Kihuni.
….sababu ya tatu ni kwamba sidhani kwamba sugu anatoa kashfa hizo kwa kuwa ana chuki binafsi na mimi bali ni mtu ambae ana ndoto flani ambazo kwa njia moja au nyingine ana hisi daraja rahisi la ndoto hizo ni kupitia kunichafua mimi…na kwa hilo, nimemuomba Mungu muda mrefu anipe ustahimilivu wa kupokea matusi na kashfa zake zote ili mradi sehemu kubwa ya wananchi kwa namna sahihi wanafahamu au watafahamishwa ukweli na vyombo husika. Mi sitazizungumzia hoja alizozitoa kwa undani kwasababu hakuwa anazielekeza kwangu bali kwa Waziri mwenye dhamana, Mh Emmanuel John Nchimbi ambaye kutokana na majibu yake nitatoa ufafanuzi wa hoja ambazo zinahitaji ufafanuzi zaidi.
Kinacho niuma zaidi ni pale kijana wa kitanzania, sugu, anatumia fursa aliopewa na vijana wa kitanzania wa mbeya, kuwa kashfu vijana wa kitanzania ambao wanashiriki kwa hiari kwa njia moja au nyingine katika tamasha la fiesta kama wasanii au waajiriwa wa kazi mbali mbali zitokanazo na tamasha hili ambalo liko katika mwaka wake wa kumi. Tamasha hili liko chini ya kampuni binafsi kwa jina primetime promotion, kampuni ambayo iko chini ya kampuni mama clouds media group, ambayo pia humu ndani zipo redio station 3, clouds fm, choice fm, coconut fm na cloud tv. Kwa kuwa ni kampuni binafsi, hapa sio sehemu ya kutangaza utaratibu wake wa kufanya kazi lakini kw akuwa ni kampuni iliosajiliwa kihalali hapa nchini, basi mtanzania yeyotea anaeniskiliza sasa hivi ajue kwamba inaendeshwa chini ya sheria za nchi hii na kama ingekuwa inafanya chochote kinyume na sheria za nchi hii basi vyombo husika vingekuwa vimechukua mkondo wake..
Bwana sugu kwa jazba na hasira ambazo kwa mtazamaji wa kawaida wa matukio ya bungeni, ni kitu nadara sana kuona muheshimiwa akikifanya, alidiriki kuishambulia asasi isio ya kiserekali ambayo mimi ni muanzilishi, Tanzania house of talent. Naomba bwana sugu aeleze watanzania ni nini walimkosea vijana hawa wa kitanzania ambao wanajaribu kujikwamua kutoka maisha ya dhiki kupita vipaji vyao ndani ya nyumba hii ya vipaji. Kwa kuwa mimi sio msemaji wala manager wa tht, nasubiri tht waje wamjibu sugu kuhusiana na tuhuma zake ingawa imenishangaza inakuwaje mbunge anashindwa kufanya utafiti kidogo tu wa kugundua kuwa THT ina nyumba mbili inazotumia na zote zinalipiwa kodi. Kwa miaka mitano sasa sijapata hiyo bahati aise…..kodi, umeme, maji wote unalipwa na THT yenyewe.

Sasa hebu jiulize, mbunge anachukua maneno barabarani na bila hata kutafiti anayapeleka bungeni…hiyo ndo hali inayonitia wasiwasi kidogo. Sio mixtapes, interviews , blogs na hata face book…joseph mbilinyi amekuwa akitutukana wazi wazi mimi pamoja na wote hapa clouds fm….tht na hata wasanii wengine anaowaita masnitch sababu wamefanya Fiesta kwa ujumla…tumekaa kimya muda wote huo kwa kuwa tulikuwa tunampuuzia lakini kitendo cha mtu huyu kutumia nafasi yake bungeni kuwapotosha watanzania walio wengi kuhusiana na swala la mastering studio, pango la THT, tamasha la fiesta na kadhalika ni jambo ambalo tukilifumbia macho mwishoe atatukania wazazi wetu..

Pamoja na kwamba umekuwa unawalalamikia TFU kwa ujumla, naomba nikupongeze kwa walau kutumia baadhi ya vipengele ambavyo TFU waliambatanisha katika maombi kumi na mmoja walio wasilisha kwa raisi. Maombi hayo ni pamoja na TRA kuhusika katika kutoa sticker ambazo zitatambulisha kazi halali za sanaa Tanzania, kuundwa kwa mamlaka ambayo itasimamia haki za wasanii na sio COSOTA. Kwa kuwasilisha hoja hizo, ulionyesha chembe chembe ya kile ambacho natumai ndicho kilichowapelelkea wakazi wa mbeya mjini kukupa hsehima ya kukuchagua kama mbunge wao.
Kwa kumaliza, nasema, siku zote naamini binadamu hatuna haters ila tuna a bunch of confused admirers.

RUGE MUTAHABA.

Advertisements

4 Responses to TAMKO RASMI KUTOKA KWA RUGE MUTAHABA KUHUSU MBUNGE WA MBEYA MJINI-CHADEMA MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI (MR II)

  1. […] ya pale Bwana Ruge alitoa Tamko ambalo kwa walipata kumsikiliza utakubaliana na mimi alionyesha kukerwa sana na kilichotokea na […]

  2. Thanks for the marvelous posting! I seriously enjoyed reading it, you will be a great author.I will be sure to bookmark your blog and may come back in the future. I want to encourage continue your great work, have a nice weekend!

  3. Whats up! I just wish to give a huge thumbs up for the great info you have got right here on this post. I can be coming back to your blog for more soon.

  4. We absolutely love your blog and find many of your post’s to be exactly I’m looking for. Does one offer guest writers to write content for yourself? I wouldn’t mind publishing a post or elaborating on a number of the subjects you write regarding here. Again, awesome weblog!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: