“Serikali haiungi mkono Big Brother” Nchimbi

imageSerikali imesema kuwa haiungi mkono mchezo wa Big Brother ambao unaonyeshwa na kituo kimoja cha Television si tu Tanzania bali sehemu kubwa ya Ulimwengu.

Akihitimisha hoja za bajeti ya Wizara yake 12/08/11 Dr. Nchimbi amesema kuwa kipindi cha Big Brother ni kero na serikali haikuingi mkono. Wakati akisema hayo wabunge wengi walionekana kupiga madawati yao ikimaanisha kuwa wanaunga mkono.

Nchimbi alikuwa akijibu swali tpoka kwa Mheshimiwa Mbunge aliyetaka kujua msimamo wa Serikali juu ya suala hilo.

Kipipndi cha Big Brother kinaandaliwa na kurushwa live kwa takribani miezi mitatu kwa masaa 24 huku kikionyesha washiriki wakiishi kwenye jumba moja ambapo wasichana na wavulana huchanganyika na kutakiwa kuishi pamoja humo kwa muda wote huo.

Mchezo huu umekuwa na mapokeo tofauti huku vijana wengi wakiufurahia na kuunga mkono na baadhi ya watu wazima wakiupinga kwa vile mambo ya humo hayaendani na mila na desturi zetu.

Mheshimiwa Nchimbi amesema kuwa Serikali haiungi mkono “… na ndio maana huwa hatuendi kuwapokea, ni vile tu mualiko wa washiriki unafanywa kwa kuitana kwenye internet …” alisisitiza Nchimbi huku akishangiliwa na wabunge.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: