Joseph Kusaga “Mwakani tunaipeleka FIESTA Kenya Rasmi”

image

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga amesema kuwa kuanzia mwakani 2012 msimu mpya wa Tamasha la Fiesta kwa mara ya kwanza litaanza nchini Kenya. Akiongea na kipindi cha Power Breakfast Bwana Kusaga amesema kuwa Kenya tayari wame confirm na amesema asilimia miamoja wataanza kuwarusha nchini Kenya, “…asilimia 100 tumesha fanikisha maongezi na wenzetu wa Kenya na kuanzia mwakani tunaanza rasmi Fiesta Kenya…” alisema Kusaga.

Pamoja na Mambo mengine Kusaga alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wale wote waliofanikisha tamasha hilo na kusema kuwa anaahidi kwa mwakani mambo kuwa zaidi ya hao. Mbali na hiyo Bwana Kusaga aliwataka wale wanaolipinga Tamasha hilo kufikiria tena na sio kuleta siasa kwani Tamasha hilo lina manufaa na ni kilele cha burudani kwa vijana na Taifa kwa ujumla huku akiwataja baadhi ya wanamuziki maarufu waliowahi kuburudisha kwenye Tamasha kama hilo kuwa ni  Shaggy, lil Kim, Kat DeLuna, Ja Rule na Ludacris pamoja na wengineo huku akiahidi kuwa kwa wale maarufu wachache waliobali nao pia wataletwa nchini.

Pia Kusaga aliwataka Halmashauri ya Jiji la Dar Es slaama na Manispaa ya Kinondoni kufikiria kupata sehemu ambayo itatumika kwa matamasha makubwa kama haya kwani sehemu pekee iliyozoeleka kutumia ni Leaders Club pale Kinondoni ambayo kwa sasa imeonyesha kuwa ni ndogo, “Tumeshawaomba wahusika na tumewatajia hata eneo watupatie sisi tutalifanyia kazi ili matamasha kama haya yawe yanafanyika huko, Uwanja wa Taifa umekaa kimpirampira zaidi na sio kwa matamasha…” aliongeza Kusaga.

Pia Kusaga alithibitisha kuwa washiriki wasanii wote walishalipwa pesa zao na kusema kuwa wale waliopatwa na misukosuko ya hapa na pale anawaomba radhi kwani kwenye wengi kuna mengi.

Advertisements

3 Responses to Joseph Kusaga “Mwakani tunaipeleka FIESTA Kenya Rasmi”

  1. sakina says:

    mnazingua tu nyie wezi clouds…..!

  2. sakina says:

    waaaaaaaaaaaaafuuuuuuuuuuuuuuuu fm!!!

  3. Pretty specified he’ll have a good study. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: